Wanaume mnaopaka mafuta mwili mzima mwache tabia za kike

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Kwa masikitiko makubwa nawakanya wale wanaume wanaopaka mafuta mwili mzima kama wanawake waache hizo tabia za kike.

Unakuta umekaa zako geto na mshikaji pale ametoka kuoga anaanza kujipaka mafuta mwili mzima mpaka kwenye makalio kwa kweli inasikitisha sana.

Sasa kama unajijua wewe unatabia hii acha mara moja nasio vinginevyo
 
Kuna mtazamo na Sheria.
Hapo umeongea kwa mtizamo wako, ambao Watu watau-judge Kwa Akili na upeo wao wa kufikiri.

Wenye Akili kubwa watakuona hamnazo,
Matajiri na wenye vipato watakuona mpuuzi Kwa sababu unaishije chumba kimoja na Mwanaume mwenzako.
Wenye Akili ya kawaida watakupuuza,
Wenye Akili ndogo wataungana na wewe.

Ukijenga hoja inayohusu mtazamo wako lazima uitetee Kwa hoja madhubuti,
Hujaeleza ni Kwa nini mwanaume hapaswi kupaka Mafuta Mwili mzima ikiwemo matakoni, hujaeleza kisayansi, kimila wala kidini.

Ninyi ndio mnafanya Watu wa mikoani tuitwe Washamba
 
Nilikuwa nafanya huo ujinga wa kutojipaka mafuta vizuri hadi siku nilipopata ajali ya pikipiki,

kwenda hospital navuliwa suruali nimepauka kwanzia kwenye mapaja, mgongo, tumbo. Niliona aibu na nilijiona fala sana.

Kutojipenda hakukufanyi uwe mwanaume rijali, kama sio sio tu
 
Back
Top Bottom