dokta ukienda na mkeo
anakwambia tupishe,,nenda nje,,
halafu kabla hujatoka anamwambia mkeo vua nguo ulale kitandani..
halafu unamlipa pesa..
unaweza huyo kukuta huyo mwanamke mpaka anakuvulia nguo
ulitumia pesa nyingi,,,,
yeye anavuliwa bure na kulipwa juu...
inaumaaa....
The Boss..umenichekesha sana kwa post yako
Kwenye nchi zilizoendelea, unaweza ukakaa kwenye examination room mkeo akiwa anahudumiwa, ama hata akiwa anajifungua. Pia unaweza kushirikishwa katika kila hatua, kwa kuwa kuna nafasi na infrastructure inaruhusu. Fikiria kama katika hali ya kawaida ingewezekana Amana ama Temeke, ambapo kunakuwa na daktari mmoja anayesubiriwa na akina mama 20 walio tayari kujifungua, yeye anatakiwa afanye vipimo vyote, na ahakikishe wanajifungua salama. Je mtu huyu katika hali ya kawaida anaweza vipi kukaa na mmoja kwa muda mrefu?..pia fikiria katika hali ya kawaida, wakina mama 20 wote wako uchi wakiwa wanasubiri kujifungua, katika chumba kimoja, je inawezekana vipi Baba akubaliwe kuingia ndani kutoa support?. Hata kama wangeruhusiwa isingewezekana katika hali ya kawaida. Pili, huduma ya uzazi, japokuwa inahusisha watu wawili, yani baba na mama, ila muhudumu anapaswa kuhakikisha kwanza mama yuko tayari kwa mtu mwingine hata kama ni mume wake kuwepo eneo la tukio. Kule Labor ward kuna mambo mengi sana ya siri, ni siri za mama na muuguzi wake, ambazo hata baba hutakiwi kuzijua. Ni siri ambazo muuguzi na daktari wanazitunza na muuguzi ameapa kutozitoa. Kuzitoa ni kosa kubwa la maadili.
Finally, Ni kweli kwamba daktari hawezi kukumbuka umbile la mkeo hata kama atamuhudumia mara kumi, ukitoka hapo ameshasahau hata rangi ya nje tu, wanaona wengi sana, tena wenye maumbile tofauti tofauti, na sio rahisi kumkumbuka hata mmoja haswa nyeti zake. So kusema kwamba wanafaidi na wanalipwa, ni kuwaonea bure,..actually, inapunguza sana hamu ya kujamiiana hata na wake zao,..you can imagine!
stun