Wanaume kuweni na huruma

maimatha

Senior Member
Mar 2, 2013
129
161
unakua na mwanamke unamkuta na maisha yake mazuri na furaha tele!!! unamwambia unampenda na ahadi kibao mpaka kwenu unampeleka ikibidi hata anapoishi unamuamisha na kukufata wewe kama na kazi/ biashara zake anasitisha na kurudi nyuma ili tu akufate ulipo!!!! baada ya kumpa ujauzito unamwambia haumtaki wala haumpendi tena umepata mwingine tena unamtamkia maneno hayo mazito akiwa na ujauzito miezi saba! humuonei hata huruma na hali yake jmn!!! hata mtoto humuonei huruma.. hata hufikuriii tayar mwenzio umemrudisha nyuma kimaendeleo, mbaya zaidi ni wewe ulikua unamlilia kila siku unaham na mtoto !!!!
kumbuka aliacha kila kitu kwa ajiri yako kuweni na hofu ya mungu jaman.. kumbukeni mungu yupo tu!!!!
 
Kila kitu na sababu yake. Kuna mengi nyuma ya pazia. Unaeza ukahadithia kwa hyo njia tukaona huruma ila na huyo mwanaume akiongea unaweza kuona wanawake washenzi.

One sided story
 
wanaume wachache sana wa kufanya hivyo... kama ni damu yake mwenyewe hawezi mkataa ila kama na we mwanamke hukutulia anakua na wasiwas wa kupakaziwa!!!
 
unakua na mwanamke unamkuta na maisha yake mazuri na furaha tele!!! unamwambia unampenda na ahadi kibao mpaka kwenu unampeleka ikibidi hata anapoishi unamuamisha na kukufata wewe kama na kazi/ biashara zake anasitisha na kurudi nyuma ili tu akufate ulipo!!!! baada ya kumpa ujauzito unamwambia haumtaki wala haumpendi tena umepata mwingine tena unamtamkia maneno hayo mazito akiwa na ujauzito miezi saba! humuonei hata huruma na hali yake jmn!!! hata mtoto humuonei huruma.. hata hufikuriii tayar mwenzio umemrudisha nyuma kimaendeleo, mbaya zaidi ni wewe ulikua unamlilia kila siku unaham na mtoto !!!!
kumbuka aliacha kila kitu kwa ajiri yako kuweni na hofu ya mungu jaman.. kumbukeni mungu yupo tu!!!!

Tatizo letu sisi binadamu tunapenda kudanganywa, na kwenye maswala ya mapenzi tunatumia hisia/feelings badala ya akili kwenye kutafakari. pole sana mdada, maisha hayana fomula!
 
Mtu akiwa honest kuwa hataki commitment ni just good times mnamuona wa ajabu kumbe hadi mkutane na vimeo ndo mjifunze

Sio hvyo tu mwingine anaweka commitment kwa kumaanisha hawataki,mtu akiwa mkweli hawataki,akiwadanganya wanataka . Suluhisho ni kuwadanganya tu na kufake maisha ndio wanapenda,akija kushtuka jua linakua limechomoza.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta dunia ndo ilivyo kuna binadamu wema na wabaya. Lakini umeelezea upande wa jamaa tu hujatuambia wewe ulibugi nini mpaka ikawa hivyo. Inawezekana chanzo cha matatizo ni wewe japo sio utu pia kwa jamaa kukuacha katika hali ya ujauzito. Pole sana.
 
Mtu anakuambia anataka mtoto na wewe unakubali kuzaa wakati wewe unataka ndoa...?

Ukiambiwa nataka mtoto mwambie afuate procedure unless na wewe uko tayari kuwa single mother...

Pole...rudi kwenye biashara zako ujitafutie pesa umlee mwanao...

Ila siku nyingine usiache biashara kumfuata mwanaume...
 
Hadithi hii nikwapande zote mbili mwanamke na mwanaume

Mimi namfahamu mwanamke aliyetelekeza nyumba yake na watoto akaenda kwa mchepuko na mmewe alimfuma zaidi ya Mara tano kila Mara alikuwa anamsihii aachane naye kagoma Leo anajuta anawayawaya mjini

Kusalitiwa kupo pande zote
 
unaacha kazi/biashara kisa kumfuata mwanaume ambaye sio mume wako??

unaambiwa nataka mtoto na wewe unakubali kuwa pakacha la kubebea watoto wake??

pole sana, jambo la msingi jipange upya toka na utafanikiwa, tupa ya nyuma anza upya ni changamoto ndogo sana hii kama ukitaka iwe ndogo ila ukitaka kuikuza itakuweza manake hutoweza kustahimili.
 
ukiwa na mapenzi ya kweli mara nyingi unafall kwa wrong person. Maisha ya mapenzi ni full utata tu
 
Unaacha kazi/biashara kisa mwanamme? Tena hata hamjaoana rasmi? Pole, uli bug meeen.
 
unakua na mwanamke unamkuta na maisha yake mazuri na furaha tele!!! unamwambia unampenda na ahadi kibao mpaka kwenu unampeleka ikibidi hata anapoishi unamuamisha na kukufata wewe kama na kazi/ biashara zake anasitisha na kurudi nyuma ili tu akufate ulipo!!!!
Hayo mengine yote inawezekana ikawa sawa lakini kitendo cha kukubali kuzifanya biashara zako zirudi nyuma ni tatizo
Ungeweza kufanya hayo na bado usiruhusu biashara zako zisiharibike

Jifunze hilo,hapo tatizo ni lako na sio la huyo jamaa
baada ya kumpa ujauzito unamwambia haumtaki wala haumpendi tena umepata mwingine tena unamtamkia maneno hayo mazito akiwa na ujauzito miezi saba!
Duh! ....

Pole sana dada yangu,hapo kuna haja ya kukubaliana na mtokeo na kuendelea na maisha yako,kuna watu wana roho za ajabu sana,hapo unachotakiwa kufanya ni kuendelea na shughuli zako na kuachana na huyo mng'aa

Next time usibebe ujauzito ukiwa na mategemea ya kupata msaada kutoka kwa mtu mwingine
humuonei hata huruma na hali yake jmn!!! hata mtoto humuonei huruma.. hata hufikuriii tayar mwenzio umemrudisha nyuma kimaendeleo, mbaya zaidi ni wewe ulikua unamlilia kila siku unaham na mtoto !!!!
kumbuka aliacha kila kitu kwa ajiri yako kuweni na hofu ya mungu jaman.. kumbukeni mungu yupo tu!!!!
Wenye hofu ya Mungu tupo wengi sana ila tatizo lenu na nyie ni ma bandidu sana,utadhani mmepitia chuo cha kuwatenda wanaume

Pole sana na endelea na maisha yako tu dada yangu!
 
Mtu anakuambia anataka mtoto na wewe unakubali kuzaa wakati wewe unataka ndoa...?

Ukiambiwa nataka mtoto mwambie afuate procedure unless na wewe uko tayari kuwa single mother...

Pole...rudi kwenye biashara zako ujitafutie pesa umlee mwanao...

Ila siku nyingine usiache biashara kumfuata mwanaume...

Anaweza kukuacha hata kama mmefunga ndoa

Ni bora tu kutafuta njia ya kuhakikisha kuwa huyo ulienae sio kimeo basi!
 
Back
Top Bottom