Wanaume kuishi na Mwanamke aliyekuzidi kipato/wadhifa/umaarufu ni kama kujishusha

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,836
Habari zenu wana.Maisha yanaenda kwa kasi sana. Halafu kwa kushangaza wanawake sikuizi ni Kama wamestuka ki design flani wanajitafutia pesa hawataki kuwa tegemezi tena.

Wanawake wenye kipato kikubwa wamekuwa wengi sasa hivi wenye uwezo wa kumudu kabisa mahitaji ya familia bila mwanaume kutia mkono.

Tuchukulie mfano katika siasa kwa Mfano Mama Samia (Makamu wa Raisi) nina uhakika ana kipato kikubwa kuzidi mumewe Ila wanaishi pamoja. Nadhani hata kumpiga kofi au kumkoromea wakati mwingine inashindikana ndani ya nyumba.

Kwasababu kwanza anakuwa Kama msemaji wa familia na majukumu makubwa Anaweza kuwa yeye ndo anayatekeleza sasa utamtisha vipi.
Hata mkiachana ana uwezo wa ku move on.

Mi nahisi unakuwa unadhalaulika wakati mwingine hata kupajua kwako watu wanapafahamu kwa jina la mkeo "Pale ni kwa mama Samia"hawasemi "Pale ni kwa Baba Flani"

Hii inakatisha sana tamaa unaweza ukahisi upo kwenye jamii ya Matrineal kumbe wala upo Patrineal Ila kwa jinsi unavyochukuliwa unakata tamaa.
 
Hiyo dhana ndiyo inawafanya wanaume kuwaogopa wanawake waliofanikiwa kimaisha na kielimu.

Kikubwa mwanamke anayejielewa akifika ndani ya nyumba yake mafanikio, mamlaka na vyeo vyake vinaishia getini. Maisha ya kifamilia ni tofauti kidogo, wadhifa wake unabaki kama mama na mke. Asiyejielewa ndiye analeta ubabe home.

Kuhofia kufahamika kwa mkeo kuliko wewe ni kawaida tu, cha msingi mahitaji yote unayapata kama mume au natimiza majukumu yake kama mama?

Swali: Mfano ukamzidi mkeo kwa kila kitu ila ukampa biashara inayompa umaarufu kiasi nyumba na mtaa wako unafahamika kwa jina la mkeo, utamuacha?
 
Mkuu uzi ujao uandike... JF unaishije na wanachama wanaokuzidi kuanziisha nyuzi?

Maana mzee baba/mama unazichapisha haswa..hongera.
 
We endelea na ligi yako ya mchangani, hao ni kama UEFA, tuachie sisi tusiowaogopa.
Alafu unataka wao wasiolewa au wasiwe na wanaume!?
 
Mwanamke hata akimzidi mwanaume pesa, mali na elimu kama mwanaume anaijua nafasi yake kwenye nyumba hawezi ogopa.
Heshma ya mwanaume ni muhimu sana na hii heshma haiombwi wala kudaiwa kwa nguvu... inakuepo kutokana na vile anavyocheza na nafasi yake ndani ya mji wake yeye kama yeye
 
Yaani unazidiwa kila kitu na mwanamke kasoro maumbile alafu eti heshima ibaki pale pale kweli
 
Ndoa ni taasisi ambayo imejengwa katika makubaliano katika kutekeleza yaliyomo ndani ya taasisi.

Tafsiri ya watu wa nje juu ya namna ndoa za watu zinavyoendeshwa ndio chanjo ya hofu na uoga ambao unawafanya watu wengi kuzikwepa.

Lakini ukweli ni kuwa tafsiri sahihi ipo kwa waliopo kwenye ndoa, vijana acheni woga na tafsiri za kifikirika.
 
Yaani unazidiwa kila kitu na mwanamke kasoro maumbile alafu eti heshima ibaki pale pale kweli
Kama unamhudumia yeye binafsi familia kama mume na baba bila kulegea nakuhakikishia hata hicho unachosema ni chakwake atakuomba umsaidie kusimamia
Ila kama umebweteka sababu mke ana pesa lazima pachimbike..... Jitahidini kuishi nao kwa akili
 
Sasa si ndo ugumu unapokuja unajitahidi kuishi naye kwa akili kumbe hata hiyo akili yenyewe anakuzidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom