Jinsi ya kuishi kwa amani na mwanamke aliyekuzidi kipato na kuifurahia ndoa

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,129
32,821
Habari za muda huu wapendwa,

Bila ya shaka sisi sote kwa namna moja au nyingine ni wahanga wa hili jambo kwenye jamii au ndoa zetu lakini ni wachache sana walio we za kuvuka salama salimini kwenye mtihani huu mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia angalau kuishi na amani na mke kipindi ambacho huna kazi au amekuzidi kipato.

1) JIAMINI

Mwanaume asiyejiamini ni udhaifu mkubwa sana mbele ya mwanamke hii humfanya mwanamke asijihisi kuwa yupo salama mbele yako so kujiamini kwako kunamfanya awe na natumaini na wewe.

2) USIBADILI SANA RATIBA ZAKO

Kipindi ambacho huna kazi muda mwingi sana unakuwa idle hii hupelekea mwanamke kukuona kama wewe ni mtu ambaye umeshapoteza natumaini na umeshakata tamaa na maisha kwani huna jitihada tena za kuinuka tena hali hii humvunja moyo mwanamke na kumfanya ajihisi amebeba mzigo nzito sana hali ambayo huzaa msongo wa mawazo inayompelekea awe na hasira muda wote.

3) Mpe haki yake ya ndoa kwa utimilifu.

Umuhimu wa tendo hili unafahamika kwa wanandoa kwani huondoa stress na kufanya mwili kurelax hivyo basi hakikisha purukushani zako za kujikwamua kiuchumi wakati huu kwa kiasi kikubwa zisikuathiri utendaji wako wa chumbani.

4) Msaidie kuvaa asubuhi akitaka kwenda kazini.

Jambo hili humuondolea stress na kumfanya ajione yeye ni wa kipekee na ajione kuwa alifanya uchaguzi sahihi kuolewa na wewe (kumbuka wanawake wanafurahia mambo madogo ambayo kwa macho huwa yanaonekana hayana maana).

5) JIZUIE SANA KUTUMIA HELA YAKE KWA MAMBO YAKO BINAFSI

Nawasilisha
 
Hili swala ni mwiba kwa ndoa nyingi. Mume hana kazi lakini mke akitoka kibaruani anamkuta baba kwenye kochi na remote, anapokelewa na matusi kwamba amechelewa kwa mabwana zake; mama anavumilia anaingia ndani anaanza kwa kutandika kitanda. Uvumilivu una mwisho. Akichoka hilo timbwili lake usiombe. Wanawake wana maneno makali kuliko ncha ya kisu. Hiyo point ya kujiamini ni muhimu sana kwa wanaume, na kujiamini si kujihami kwa kuwa mkorofi.

Pia waume wanapokosa kazi wanakuwa na msongo kwa hiyo wakati mwingine anaweza asijipende wala kupenda maisha. Hivyo si ajabu mke kurudi nyumbani na kukuta nyumba hovyo na mume ana hasira hasira kama mjamzito. Wote wawili wakipatwa na msongo mgongano unakuwa mkubwa sana. Kila mmoja anamwona mwenzie kuwa ndo tatizo.

Mwisho kabisa kukosa kazi kuwe ni kwa mpito jamani. Kuna wanaume wana maudhi!!! Mke atajitahidi kumfungulia biashara hii na ile, kumtafutia kazi huku na huku mwanaume hataki. Kuna mke mmoja akaona waandikishe gari Uber mume akishamshusha aendelee kupiga kazi ya kutoa huduma ya usafiri. Mke anakuja kugundua mume hafanyi ile kazi kama walivyokubaliana. Anampa kijana wa huko mtaani aendeshe yeye anaenda gym na kuangalia TV nyumbani. Hili zigo jamani bora hata mtoto mdogo utamtuma dekio au chumvi. Mungu awatie nguvu waume na wake wanaopitia hili jaribu.
 
Kwakweli ni kipaji.
 
Ukiweza kuishi na mwanamke aliyekuzidi kila kitu..

urefu,pesa,elimu,ubonge,ndevu,smartphone na ikiwezekana umri na ndoa ikawa na amani basi wewe unastahili tuzo nobel na zingine.

Na vikitokea vita vya 4 vya dunia tutakuhitaji uwe msuluhishi.
 
hahaha huyo atakuwa mwanaume wa nguvu aisee
 
Ukiweza kuishi na mwanamke aliyekuzidi kila kitu..

urefu,pesa,elimu,ubonge,ndevu,smartphone na ikiwezekana umri na ndoa ikawa na amani basi wewe unastahili tuzo nobel na zingine.

Na vikitokea vita vya 4 vya dunia tutakuhitaji uwe msuluhishi.
 
Hela ya mwanamke ni sumu kwa mumeee

Hela ya mke ni sumu kwa mume gunia la misumari. Kuna wanaume wastaarabu sana pamoja na kipato chao duni wanajua ku-handle mke. Hakuna biskuti ngumu kwa chai. Hakuna mwanamke asiyeyeyuka mbele ya upendo wewe. Unakuta mume hana kazi lakini hafuji hela ya mkewe kama ambavyo asingependa yake ifujwe, anashiriki shughuli za malezi ya watoto kama kusimamia homework na kufatilia maendeleo shuleni, kitu kikiharibika nyumbani mke ana mume wa kumtegemea, wakianzisha mradi wa familia kama ujenzi mke ana imani na usimamizi wa mume. Sasa ukute mwanaume kinyume na hapo lazima hela ya mke iwe sumu. Kwanza anadai hela kwa mabavu utafikiri alimkopesha, anataka aishi maisha ya juu kama mwanaume anayefanya kazi bila kujali mazingira, hajishughulishi na chochote wala lolote, halina hata mahaba. Mama wa watu ukimwuliza mara ya mwisho alibusiwa au kukumbatiwa lini anakwambia "siku tuliyosimamia harusi ya Ngosha tukaambiwa na MC tubusiane wakati wa kulishana keki."

Nimeishi kwenye familia ambayo mama alikuwa akijishughulisha na kilimo na ufugaji na baba alikuwa dereva. Kipato cha mama kilikuwa kikubwa lakini sikuwahi kuona wakikoseana heshima au mama kulalamika (wamama wengi hulalamika kwa watoto wakiwa jikoni). Swala la wanawake kulisha familia na taifa halijaanza leo na ndiyo uhalisia hasa huko vijijini na sasa hivi mijini linakuwa kwa kasi, ila swala la wanaume kubweteka na kusubiri mke alete ni jambo jipya linaloshika kasi. Nithubutu kusema ni jinsia mpya imeibuka maana hatuwezi kumuita mwanaume binadamu dume anayeamka saa 4, anakula kifungua kinywa, anaenda saluni ya karibu kuzogoa, anarudi nyumbani kula, anaenda gym, anatoka hapo anaenda bar kucheki mpira, wikiendi anasindikiza wanaume saiti za ujenzi au mashambani. Anachukua hela za mkewe anaenda bar au hoteli za gharama anapost picha na akiwa kule anachangia story za mambo makubwa anayotarajia kufanya lakini hafanyi hata moja. Akiotea hela ananunua nguo, simu au gari la kueleweka halafu uliza nani ataweka mafuta. Wengine wanajiongeza zaidi nao wanadanga wanawake wenye uwezo kuliko wake zao. Hii ni jinsia mpya. Siyo -ke wala -me. Sasa huu uzi utakuwa na wachangiaji wa jinsia zote tatu. Nitakuwa makini na miandiko.
 
KUMSAIDIA KUVAA AENDE KAZN? YAN UNAGEUKA MKE? LOH, HAIWEZEKAN

Kuwa mke au mume ni nafasi/majukumu na si aina za vikojoleo/maumbile waliyo navyo wahusika. Hata hivyo wanandoa kusaidiana kuvalishana ni ishara ya kupendana na kujaliana tu na si jukumu la kisheria la mwanandoa wa kike. Kumvalisha mtoto ndo jukumu kwa sababu hajiwezi na umechukua jukumu la kumlea.
 
Hela ya mke ni sumu kwa mume gunia la misumari. Kuna wanaume wastaarabu sana pamoja na kipato chao duni wanajua ku-handle mke. Hakuna biskuti ngumu kwa chai. Hakuna mwanamke asiyeyeyuka mbele ya upendo wewe. Unakuta mume hana kazi lakini hafuji hela ya mkewe kama ambavyo asingependa yake ifujwe, anashiriki shughuli za malezi ya watoto kama kusimamia homework na kufatilia maendeleo shuleni, kitu kikiharibika nyumbani mke ana mume wa kumtegemea, wakianzisha mradi wa familia kama ujenzi mke ana imani na usimamizi wa mume. Sasa ukute mwanaume kinyume na hapo lazima hela ya mke iwe sumu. Kwanza anadai hela kwa mabavu utafikiri alimkopesha, anataka aishi maisha ya juu kama mwanaume anayefanya kazi bila kujali mazingira, hajishughulishi na chochote wala lolote, halina hata mahaba. Mama wa watu ukimwuliza mara ya mwisho alibusiwa au kukumbatiwa lini anakwambia "siku tuliyosimamia harusi ya Ngosha tukaambiwa na MC tubusiane wakati wa kulishana keki."

Nimeishi kwenye familia ambayo mama alikuwa akijishughulisha na kilimo na ufugaji na baba alikuwa dereva. Kipato cha mama kilikuwa kikubwa lakini sikuwahi kuona wakikoseana heshima au mama kulalamika (wamama wengi hulalamika kwa watoto wakiwa jikoni). Swala la wanawake kulisha familia na taifa halijaanza leo na ndiyo uhalisia hasa huko vijijini na sasa hivi mijini linakuwa kwa kasi, ila swala la wanaume kubweteka na kusubiri mke alete ni jambo jipya linaloshika kasi. Nithubutu kusema ni jinsia mpya imeibuka maana hatuwezi kumuita mwanaume binadamu dume anayeamka saa 4, anakula kifungua kinywa, anaenda saluni ya karibu kuzogoa, anarudi nyumbani kula, anaenda gym, anatoka hapo anaenda bar kucheki mpira, wikiendi anasindikiza wanaume saiti za ujenzi au mashambani. Anachukua hela za mkewe anaenda bar au hoteli za gharama anapost picha na akiwa kule anachangia story za mambo makubwa anayotarajia kufanya lakini hafanyi hata moja. Akiotea hela ananunua nguo, simu au gari la kueleweka halafu uliza nani ataweka mafuta. Wengine wanajiongeza zaidi nao wanadanga wanawake wenye uwezo kuliko wake zao. Hii ni jinsia mpya. Siyo -ke wala -me. Sasa huu uzi utakuwa na wachangiaji wa jinsia zote tatu. Nitakuwa makini na miandiko.
Shikamoo Nandera. Umeongea kila kitu. Naomba upewe shahada ya heshima kwa hii post.
 
Back
Top Bottom