Wanaume Kenya waoongoza kwa uzinzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume Kenya waoongoza kwa uzinzi

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Pdidy, Nov 16, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,434
  Likes Received: 5,691
  Trophy Points: 280
  Wanaume Kenya waoongoza kwa uzinzi
  Written by Administrator
  Monday, 16 November 2009 10:18
  NAIROBI,Kenya

  UTAFITI mpya umeonesha kuwa wanaume nchini Kenya wanakuwa na vimada zaidi ya watatu katika kipindi cha maisha yao tofauti na inavyokuwa kwa wanawake.

  Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti uliofanywa hivi karibuni na taasisi ya Kenya Demographic Health Survey (KDHS) wastani wa asilimia 6.3 ya wanaume wanavimada ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya wanawake.

  Ripoti hiyo ilieleza kuwa wanaume kutoka mikoa ya Kati ndio wanaoongoza kwa kuwa na asilimia 8.3 ya nyumba ndogo ikifuatiwa na mikoa ya Magharibi mwa nchi ambayo ina asilimia 8.1

  Wanaume kutoka Mikoa ya Pwani wameripotiwa kuwa na wastani wa asilimia 7.8 ya vimada wakati mikoa ya Rift Valley imeonesha kuwa na asilimia 6 ya wanaume wenye nyumba ndogo huku maeneo ya Nairobi na Nyanza yakifuatia baada ya kubainika kuwa na asilimia 5.6.

  Utafiti huo ambao ulifanyika mwishoni mwa mwaka jana na mapema mwaka huu uliwahusisha wanaume 2,633 na ukaonesha kuwa idadi ndogo ya wanawake ndiyo inakuwa na mpenzi wa nje.


  Katika Mikoa ya Kati imeonekana kuwa idadi ya wanawake wanaokuwa na wapenzi zaidi ya mmoja katika maisha yao ni wastani wa asilimia 2.7 wakati wanawake katika mikoa ya Magharibi na Mashariki ina wastani wa asilimia 2.3 ya wanawake.


  Ripoti hiyo ilisema kuwa wanawake na wanaume walioolewa na kuoa ndio wanakuwa na wapenzi wawili ama zaidi ikilinganishwa na wale ambao hawajaolewa ama kuoa au waliotengana katika ndoa.


  Katika ripoti hiyo imeelezwa kuwa wanandoa waliotengana ama wajane wanakuwa na wapenzi wawili.

  Imebainika pia katika utafiti huo watu wenye umri kati ya miaka 40 ni wachache wanaojihusisha na masuala ya uzinzi.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,434
  Likes Received: 5,691
  Trophy Points: 280
  pamoja na hayo tanzania bado inaongoza kwa vvu east africa,hamwoni hawa watu ni wazuri tuwaite waje kueleimisha nini siri ya mafanikio kuwa wa tatu pamoja na sherreeerrrii zote
   
Loading...