Wanaume jamani badilikeni basi mnapooa huh!

Wanaume jamani badilikeni basi mnapooa huh!

mtu mzinzi akikubali kutubu dhambi zake na kuokoka ndipo atapewa uwezo wa kushinda uzinzi na atakuwa mtu mwema mithali 28.13, yohana 1.12, luka 1.77
 
Ila visingizio vingine bana! Mtu anavaa saa la gharama na halivui......tena si ajabu upande mwingine ana pete kali tu ya madini, ila nayo haivui! Sasa ndo kusema hao vibaka wanafata pete za ndoa tu?? Aisee!!!

Mada pete ya ndoa
 
Kwanini sasa huwa hamzikatai hizo pete na kumwomba padri awaapishe kwa utashi wa kila mmoja wenu?

pete sio compulsory kwa imani zote. ni kitu ambacho kimekuja tu, kama alivyosema Safari ni Safari, tumekiiga tu. hata tunapozungumzia suala la imani ya kikristo kwa mfano; sioni sehemu yoyote katika maandiko tunapoagizwa kwamba tunapofunga ndoa na pete iwepo, kwakweli sijaiona...

ndoa inapoanza kuota nyufa, pete inafanya role gani? na je mambo yanapokuwa mazuri tena kwenye ndoa, is it thanks to the pete? vitu vingine vimeletwa na dini ila...

mtu akiamua kufunga ndoa na pete iwepo haya, lakini hata isipokuwepo haipunguzi wala kuongeza chochote. tukisema kwamba labda mwanamke aliyeolewa huonekana vzr kwa watu kwasababu amevaa kitambulisho kile, sawa, ila haizuii yeye kutongozwa na watu, maisha yameharibika kiasi hicho mkuu. ila hata ambaye hajavaa, akitongozwa, kama anaiheshimu ndoa yake, anajua cha kufanya ili aitunze ndoa yake mbele ya mume wake na Mungu wake pia. uimara wa ndoa hauwi determined na pete hata kidogo.

uimara wa ndoa ni utashi wenu ninyi wawili na Mungu pamoja na ninyi.
 
wale tunaofanya kazi ktk ajira rasmi yaani maofisini je wanawake wangapi ambao wameolewa wana pete zao lkn wanatembea na mabosi wao, wakiinamishwa katk vyoo na masofa katika ofisi za mabosi wao, je pete zao zimewasaidia nini? si bora watembee bila pete

naaam naam naam...sema bwana maana it's like pete inafanya kitu veeery significant wakati wala...ingekuwa mtu akiivaa pete ya ndoa inacreate password kwenye vikojoleo vyetu, labda ningekuwa convinced
 
...hii story imenitouch. Yamenikuta mie jana, nimeoa na nipo ndoani kama miaka kumi hivi. Na kama mjuavyo ndoa ina mabonde na milima. Jana nipo kwenye ndege nikachezea pete yangu, nikaitoa kidole cha pete nikaivalisha kwenye kile kidogo..ilipwaya lakini ilitosha. Nikaendelea kutafakari mahusiano yangu na mwenzangu, safari ikaendelea.

Nashuka chomboni, napita immigration..naangalia kidoleni pete siioni. Nafika home namkuta mwenzangu, nampa story haelewi...ananambia kuna mambo yako umefanya ukavua pete, ukaisahau. Eti na yeye ya kwake anataka kuweka kabatini! Mie sikuwa na nia mbaya ati...haya tuendelee
 
Yani gold ndo zilivyo...ukileta za vua vaa vua vaa; lazima ipotee tu.


Ndio maana kuna wanao connect na majini.


Ila na wewe. Mh. Eti umevaa kidole kidogo...hata mi ningekutilia shaka aisee. Endelea ku explain; labda ata buy it.
...hii story imenitouch. Yamenikuta mie jana, nimeoa na nipo ndoani kama miaka kumi hivi. Na kama mjuavyo ndoa ina mabonde na milima. Jana nipo kwenye ndege nikachezea pete yangu, nikaitoa kidole cha pete nikaivalisha kwenye kile kidogo..ilipwaya lakini ilitosha. Nikaendelea kutafakari mahusiano yangu na mwenzangu, safari ikaendelea.

Nashuka chomboni, napita immigration..naangalia kidoleni pete siioni. Nafika home namkuta mwenzangu, nampa story haelewi...ananambia kuna mambo yako umefanya ukavua pete, ukaisahau. Eti na yeye ya kwake anataka kuweka kabatini! Mie sikuwa na nia mbaya ati...haya tuendelee
 
anavua kwa sababu kuna mahala kadanganya hajaoa, atamuoa yeye....
 
Mbona siku hizi hata na hizo pete watu wanachitika tu?
Nadhani wanaovua wanaogopa dhamira zao kwa vile wanavaa wakiwa hawamaanishi ila kwa kuwaogopa wenzi wao inabidi wavae tu. So, kwa kuogopa macho ya watu wanaona ili wawe safe wanaamua kuzivua. Mie tangu mwanzo sikuyataka ya kuvaa mipete..mapenzi yangu yako moyoni kwisha habari yake. Muislamu sio lazima ajenge karibu na msikiti bana.
 
Back
Top Bottom