Wanaume hii kitu ni sawa?

Wanaume hii kitu ni sawa?

Anna pita

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
227
Reaction score
427
Hi kitu imekaaje?

Mwanaume miaka 37 ameoa na anafamilia kua na urafiki na kijana wa miaka 25. Tena urafiki ule wa close kabisa kila sehem wako wote ikifika jion jamaa akitoka kazini kijana anaenda nae kwake wanakaa mpaka saa 4 usiku kijana anaondoka. Kama jamaa haendi kazini basi rafiki kijana ataenda kwa jamaa asubuh saa 3 mpaka usiku saa 4 Kama kutembea. Wanaenda pamoja

Mimi nauliza, je kwa mliioa hii nikawaida?
 
Huwa inatokea. Sometimes unakuta kijana yupo matured kiasi kwamba amekutana na huyo brother sasa wamekuwa match kiakili dogo anamtumia huyo brother kama mentor wake na brother anamuona huyo dogo kama protégé wake....


So sioni cha ajabu. Watu wanakuzwa malezi tofauti kuna ambao makuzi yao yanawafanya wanaexperience mambo makubwa sana na majukumu kiasi kwamba akikaa na rika lake wanakuwa wanamfanya anajihisi yupo na watu wasio level yake ya upeo wa kufikiria.

So nothing wrong.
 
Sometimes unaweza kukuta wanabet na kufatilia live score pamoja yaani hapo hata saa saba usiku watafika. Wengine ni addicted kwenye magame so huenda wanacheza games pamoja.

Mimi Nina miaka 35 lakini siku za weekend nashinda home tu na madogo wa 30-23 yrs toka SAA tatu mpaka SAA tano tunalinda mikeka.

Au huenda wanafuatilia season pamoja ambayo hawataki kumiss vipande, si mnajua season ukiifuatilia unakua na alosto!

Huo upuuzi mnaowawazia uondoeni vichwani mwenu.
 
Naona Watu wengi wanakomenti bila kufikiri?jiulize Kwanza urafiki ni kulingana umri au kulingana mitazamo na tabia?ukishapata jibu ndio utaweza kumjibu mtoa mada.

Binafsi nina scenario kama hiyo,kuna dogo kitaa alikuwa bright shuleni na akili za kiutu uzima,sasa sisi tulikuwa Watu watatu tunasoma chuo yeye yupo form one lakini alikuwa mshikaji wetu haswa,yani hata tukienda bar tuko nae.

Yule dogo amepiga kitabu mpaka uchina huko,sasa hivi anaishi kabisa huko na ndiye anatupa michongo ya kutuweka mjini.Sasa utaniambia nisiwe na rafiki Kama huyo kisa nimempita miaka mingi?Acheni upumbavu
 
Hi kitu imekaaje?
Mwanaume miaka 37 ameoa na anafamilia kua na urafiki na kijana wa miaka 25
Tena urafiki ule wa close kabisa kila sehem wako wote ikifika jion jamaa akitoka kazini kijana anaenda nae kwake wanakaa mpaka saa 4 usiku kijana anaondoka
Kama jamaa haendi kazini basi rafiki kijana ataenda kwa jamaa asubuh saa 3 mpaka usiku saa 4 Kama kutembea
Wanaenda pamoja
Mi nauliza je kwa mliioa hii nikawaida??
Ni kawaida, mimi kuba brother flani tulitokea kuwa marafiki akawa ananielewa sana toka nasoma chuo na nilikuwa kwenye twenties yeey kipindi hicho alikuwa kwenye 38 hivi na kaoa. Nilipokuwa likizo nilikuwa namsaidia biashara zake akatokea kunielewa sana. Nimemaliza chuo tukawa marafiki sana sana tukajikuta tuna hobbies zinafanana sote wapenda movie na series zinafanana. Nikaanza ishi peke yangu, akawa akijua niko home atakuja mapema asubuhi, lakini kilichokuwa kinamleta ni movies maana kwake alikuwa hawezi kutazama movies anazopenda kwasababu ya familia, so mimi nilikuwa na external ina movieskama gb 500 na nimeconnect kwenye screen. Atashinda sebuleni kwangu asubuhi mpaka jioni.

Tulikuwa na mengi in common, tukajikuta tumeconnect. Hivyo ni kawaida sioni ajabu watu waliozidiana miaka kuwa marafiki. Ila personally, siwezi kwenda kwa mtu asubuhi nikae mpaka jioni. Na pia sipendi mtu anitembelee asubuhi mpaka jioni ananiharibia ratiba zangu. hata huyo bro nilikuwa sometimes namwambia sipo nyumbani ili mradi tu kumkwepa.
 
Back
Top Bottom