Issue hapa ni, wanaume wengi tunatamani kwanza, then kupenda kunakuja baadae. Sasa kwenye kutamani huko, ndiyo tunajikuta tunasifia hata pasipohitajika kusifiwa.
Mwanamke siyo avae Dela ama Baibui ndiyo apate wa kumtamkia ndoa, kuna mavazi mengi sana ya kusitiri sehemu muhimu za mwanamke, na ikumbukwe hata hayo madera na mabaibui, yapo mepesi na mazito, mepesi tena wanayabana kidizaini, na bado sehemu nyeti hasa kwa nyuma zitaonekana tu. Ni sisi wanaume kuamua tunataka nini, ili ndoa iwepo.
Ila la kushangaza, bado kuna makabila duniani, wanafunika sehemu chache tu za mwili, zengine zote wazi, na bado wanaoana. Mfano, mikoa yenye kujaliwa kuwa na maziwa (maji), hasa wilayani huko, bado wanaume wanaoga karibu kabisa na wanawake, na maisha yanasonga. Wewe ukifika oga uondoke. Ukifika huko wewe uliyekulia mijini, utajikuta una hati hati ya kubaka, wenyeji watakushangaa tu jinsi unvyohangaika.
Ila cha muhimu, ni wote kuamua nini mnataka, na taasisi yenu ya ndoa mtataka iweje.
Ahsante!