Wanaume acheni ubinafsi mnatesa watoto wenu!

Wanaume acheni ubinafsi mnatesa watoto wenu!

KadogooCate

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2017
Posts
484
Reaction score
1,101
Straight to the point...

Kuna bro wangu mmoja alikuwa na mahusiano na dada mmoja akazaa nae mtoto mmoja, wakaachana, bro akachukua mtoto kwa kisingizio cha mama hajatulia hawezi kulea mtoto (nahisi dada alicharuka baada ya misuguano ya kumfumania bro mara kwa mara).

Baadae akapata binti mmoja mrembo akaamua kuoa, akaoa ndoa kubwa ya kanisani na ubwabwa tuulikula. Baada ya muda mambo yakaanza kwenda mrama. Bro akawa anarudi usiku wa manane, saa zingine asubuhi au harudi kabisa. Mke akihoji anapewa kipigo cha nguvu. Ukimuangalia huyu bro wangu anavyoheshimika huko nje utashangaa na anayoyafanya aisee. Alimkataza mke asifanye kazi kwamba anakosa nini wakati anahudumiwa. Matokeo yake mke akawa omba omba, hela akipewa leo mpaka miezi ipite ndo atapewa tena. Akikutwa na kitu chochote iwe nguo ama mafuta ya kupaka atapigwa na kutukanwa juu kwamba kaanza umalaya ndo anapewa hvyo vitu na wanaume..

Wifi akaanza kutafuta msaada wa mawazo na ushauri kanisani kwa wazee wa kanisa na mchungaji lkn bro akiitwa hatokei, vituko ndo vilizidi. Huko kazini kwake bro anabadili mabinti kama nguo ( wafanyakazi sasa). Sasa akaja kupata binti huyo funga kazi. Binti kahakikisha bro amemuacha wifi ( maana ilifikia hatua bro anachukua watoto anawapeleka kwa hawara, na wakati mwingine hawara anatumia simu ya bro kumtukana wifi na kumtambia kwamba anapendwa yeye)

So mwisho wa siku bro kamtelekeza wifi na mwanae ( alizaa nae mtoto mmoja) na kwenda kuishi kwa hawara! Huyu bro wangu ni mkubwa 40+ ana kazi ya kueleweka lkn mpaka umri huo hana hata kiwanja cha 20×20! Kazi yake pombe na wanawake kama amechanjiwa!

Back to my point! Kama kusingekuwa na ubinafsi basi watoto wa bro wangelelewa na wazazi wote wawili. Namaanisha hv, sawa umepata chombo kipya cha zamani hukitaki, je umeshawaza khs hatma ya watoto wako? Je kwa umri walionao unapoamua kuwaacha na kwenda kwengine, watakuwa katika mazingira yapi? Nani atawasaidia kufikia umri wako wewe? Watasomaje? Watalelewaje? Hv ni sawa kula bata wakati hujui wanao kama wamekula ama la? Huu ni ubinafsi, yaani unajifikiria wewe, furaha yako basi, hufikirii kabisa kama unayaweka maisha ya watoto wako katika hali mbaya, hali ya kutangatanga na kuhangaika!! Watoto hawana hatia, wanateseka kwa makosa ya baba na mama, yaani wanalipa uovu wa wazazi kwa sababu ni wabinafsi! Wazazi wengi sana wanajiangalia wao, wanajijali wao ndio maana ndoa zinavunjika sana. Laiti tungewaweka watoto kwanza, tungejali furaha na future ya watoto basi tungeheshimiana na kuheshimu viapo vya ndoa.

Sasa hivi tunasikia bro anamnunulia nyumba huyo mpenzi/hawara! Badala ya kuwatengenezea watoto wake kesho yao anamtengenezea hawara!!! Kama watu wote tungeacha ubinafsi ndoa zingekuwa na furaha na amani sana, hata watoto wa mitaani wangekuwa wachache!!

Nswasilisha!
 
Hongera wifi unayewatetea mawifi zako.

Wanaume wa hivyo wapo ila nikuambie mwanaume anaweza kubadilika kutokana na tabia za mke...tena rahisi saana hii.

Mwanaume mke akiwa pasua kichwa na kama mjuavyo wengi watabaki upande wa mwanamke basi utapoteza ramani.
 
Umeandika ukiwa kama vile na wewe una kawivu kwa mbaaaali kwa huyo wifi wako mpya.
Anyway, badala ya kuja kuyasimulia mambo ya familia yenu hapa, nadhani ungetumia muda huu kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki ili wafanye kile kitakacho kufurahisha wewe na bro wako asiendelee kuwatia aibu.

Na hata huyo wifi wako nae kiazi tu, maana anaonekana alikubali kugeuzwa ngoma na huyo bro wako, na hata ungemshauri aondoke angekuona wifi nuksi unataka mharibia ndoa yake.
 
By the way.....
Una kaka bwege sana aiseee... Na sisi wanaume huwa hatufanyi hivyo, maana watoto ni baraka na baraka hutoka kwa Mungu. Ungelikuwa na bro mwenye timamu, ningesema hata afanye kama mimi. Lakini sasa ni ngumu kidogo hata kumshauri mtu ambaye hajitambui na wala hajawahi kuwaza kuwa na shelter kama ulivyo tusimulia.....
Anyway, hivi wewe umeolewa..?? Maana usije ikawa tunajadili mambo mazito na mtu hata ambaye hazijui changamoto za kwenye ndoa.
 
Hongera wifi unayewatetea mawifi zako.

Wanaume wa hivyo wapo ila nikuambie mwanaume anaweza kubadilika kutokana na tabia za mke...tena rahisi saana hii.

Mwanaume mke akiwa pasua kichwa na kama mjuavyo wengi watabaki upande wa mwanamke basi utapoteza ramani.

Ni kweli lakini hakuna justification yoyote katika kutowajali watoto
 
Hongera wifi unayewatetea mawifi zako.

Wanaume wa hivyo wapo ila nikuambie mwanaume anaweza kubadilika kutokana na tabia za mke...tena rahisi saana hii.

Mwanaume mke akiwa pasua kichwa na kama mjuavyo wengi watabaki upande wa mwanamke basi utapoteza ramani.
Uko sahihi kabisa ndo maana mwisho nikasema tuache ubinafsi tuweke mbele maslahi ya watoto.

Ukiacha ubinafsi basi utakubaliana na mapungufu ya mwenzako na kuyabeba, utasamehe na kutafuta suluhu panapobidi.

Inawezekana kabisa mke ndo sababu ya mume kuchepuka, lkn je kuchepuka ni suluhu au unaongeza mpasuko kwny ufa?
 
Sasa mwanamke mjinga kama huyo hiyo si ni haki yake tu?, yaani wanawake siku hizi bhana mtu anashindwa kuvumilia ugumu wa maisha ila anavumilia kipigo cha kila siku na ugumu wa maisha ukiwa palepale
Ujinga wake ni nini mkuu?
 
Umeandika ukiwa kama vile na wewe una kawivu kwa mbaaaali kwa huyo wifi wako mpya.
Anyway, badala ya kuja kuyasimulia mambo ya familia yenu hapa, nadhani ungetumia muda huu kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki ili wafanye kile kitakacho kufurahisha wewe na bro wako asiendelee kuwatia aibu.

Na hata huyo wifi wako nae kiazi tu, maana anaonekana alikubali kugeuzwa ngoma na huyo bro wako, na hata ungemshauri aondoke angekuona wifi nuksi unataka mharibia ndoa yake.
Asante mkuu
 
Bora,
Ila kina dada msitaman taman tu maisha ya ndoa, bila kujua unae ingia nae kwenye ndoa ni mwanaume wa namna gani.

Kuna binti nilikua namsihii sana hila hakua hakinielewa kabisa,
Yeye anaangalia tako lake tu anajua lazima apate mume wa maana,
Na anawaza kuwa akiwa na ndoa ya kisheria basi mwanaume hawezi kumpelekesha kitu,

Ukiwa mzuri wa Sura na akili pia zitafuteni jaman.
Amerudi kwa wazazi wake
 
Kuna watu walipaswa kuwa tasa kabisa ili wafurahie maisha bila kubughudhi watoto. Unaleta watoto duniani kuwatesa ili iweje.

Watu wa hivi ni BURE kabisa
Yaani wakati mwingine huwa najiuliza kwa nini anazaa sasa kama bado anakula bata?
 
Sasa mwanamke mjinga kama huyo hiyo si ni haki yake tu?, yaani wanawake siku hizi bhana mtu anashindwa kuvumilia ugumu wa maisha ila anavumilia kipigo cha kila siku na ugumu wa maisha ukiwa palepale
Kuoachana au mke kuondoka tu baada ya kadhia za mme sio rahisi hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom