amu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2012
- 16,103
- 30,992
I know your not for this honey but kuona mtu ambae ni rafiki yangu upo na kimahusiano hiyo ni vita ya 3 ya dunia ujue kwanza nimekumbuka marafiki zangu wote wapo kwenye ndoa haitotokea
Nimeuliza mswali mengi sana ambayo hujayajibu.
Ni wazi ukiwa na rafiki wa karibu aliyehusika kwa mengi kuna attachments nyingi ambazo zinaweza kufanya mahusiano naye yasiwe jambo zuri.
Hata kama unataka kuepuka drama tu.
Lakini hujajibu maswali yangu mengi sana.
Mathalani, vipi kuhusu rafiki anayeona kilichotokea si haki na akaamua kuvunja urafiki na rafiki yake huyo ambaye kamuona hayawani, na kuanzisha uhusiano na mwanamke kwa nia nzuri?
Huoni kwamba kukataza mahusiano hapo kunamnyima haki mwanamke ambaye atahitaji mahusiano na mwanamme ambaye atahitaji mahusiano, wakati pingamizi la urafiki halipo (mwanamme kashavunja urafiki).
Nilikuwa naangalia sinema moja, bosi alimpenda binti mmoja, lakini yule binti alikuwa muajiriwa wake. Bosi alipomtongoza binti, binti akakataa, kwa vile yule binti ni muajiriwa wa bosi . Na kanuni za kazi zinakataa mahusiano kati ya bosi na muajiriwa (dada zetu wengine chukueninsomo la kuheshimu kanuni za kazi hapo). Bosi akasema umesema vizuri. Jiuzulu kazi, nakufungulia biashara. Tuendeleze penzi. Kwa minajili hiyo, utakuwa moenzi wangu halafu pia nitakuwa sijavunja kanuni za kunitaka nisiwe na mahusiano na muajiri wangu.
Bosi alivunja kipingamizi kwa kumtoa binti kwenye ajira.
Rafiki akivunja kipingamizi kwa kumaliza urafiki wake, hapo itakuwaje?
By the way, I am analyzing this conceptually. I am not saying I am for this or that.