Wanaume acheni hii tabia sio nzuri

Wanaume acheni hii tabia sio nzuri

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,586
Reaction score
8,389
Usione mnapendana na mpenzi wako kumbe nyuma kuna watu wanaombea mvurugane na mahusiano yenu yavunjike

Wanaume ambao wapo karibu au wanafahamiana na mpenzi wako huwa si wazuri hakika wana tabia ambayo sio nzuri hasa kama mwanamke ni mrembo na anavutia

Wanaume wa sasa mara tu uhusiano unapovunjika ndo utaanza kuwaona wanakupigia sim au wanakualika maeneo mbalimbali ili mpige stories ili uwe karibu wakuondolee stress za kuachwa kumbe ndo mbinu ambayo anatumia ili akunase na wewe

Unashangaa mwanaume ambaye alikuwa karibu na mpenzi/ mume wako ndo anaanza kukuhurumia na kuanza kukuhudumia na kuwa karibu na wewe na mara anaanza kukutongoza na kuanza kukwambia" Nashangaa mwanaume yule ameanzaje kukuacha ulivyo mrembo hivi,ulikuwa umepotea kumpenda yule jamaa,nakuahidi ukiwa na mimi hutajutia,ingawa jamaa alikuwa ni mtu wangu wa karibu ila usihofu hilo ,nitakupenda na kukutunza mpaka jamaa ajutie kukuacha"

Hivi kwa nini wanaume wa siku hizi wanasubiri mwanamke aachwe ndo anaenda kukutongoza na huku walikuwa ni marafiki na mpenzi wako
 
Ndio kazi zetu "Wadaka chozi"

Tunasubiria bebee aumizwe tu,tunatumia fursa hiyo
 
Sijaelewa.

Ulitaka watongoze kabla mwanamke hajaachwa?
 
Kwa kanuni ya mahusiano
Hapo hujajibu kitu. Kanuni ipi ya mahusiano? Inasemaje? Uhalali wa kanuni hiyo unatokana na chimbuko gani?

Ngoja ninyumbulishe.

Kuwa na mahusiano na ndugu yako wa karibu ni jambo baya.

Kwa kanuni za misingi ya kidini. Limekatazwa. Mtu anakataa kwa sababu za dini.

Hata kama mtu hakubali dini kama mimi, kanuni za kibaiolojia zinatoa sababu za kutokuwa na uhusiano na ndugu yako wa karibu, kwa sababu mnahatarisha genetic pool watoto kuwa na magonjwa.

Hivyo ni wazi kwamba, kiutu, ukaribu wa undugu unavyozidi, ndivyo jamii inavyoona mahusiano ya kimapenzi yanakuwa hayafai.

Hivyo basi, kuna sehemu hapo ukaribu huo unafifia mpaka mahusiano hayo yanaanza kuonekana yanaruhusiwa. Ndiyo maana kuna tamaduni nyingine, baadhi ya waarabu kwa mfano, unaruhusiwa kuoa au kuolewa na binamu yako.

Sasa, ukaribu huu wa kutokuwa na mahusiano unaishia wapi? Na unapotaka kuwajumuisha rafiki za mume/mpenzi wako wa zamani, unawajumuisha kwa minajili gani? Kwa uhalali gani?

Ndugu wanajulikana ni ndugu wa maisha. Hivyo katazo la kuwa na uhusiano na ndugu wa karibu ni la maisha. Hao rafiki wa mume/mpenzi wako wa zamani, wakisema wanavunja urafiki naye ili wawe nawe utawakubali? Vipi kuhusu rafiki zake wa zamani uliowajua ambao hana urafiki nao tena? Vipi kuhusu rafiki zake wa zamani ambao hukuwajua ambao wamepoteana hawana mawasiliano muda mrefu? Vipi kuhusu rafiki zake waliopoteana kutoka darasa la kwanza? Vipi kuhusu rafiki za kaka yake ambao si rafiki zake? Vipi kuhusu rafiki za rafiki zake? Vipi kuhusu rafiki za rafiki za kaka yake?

Uchunguzi wako wa nani atakufaa kwa minajili ya kutokuwa rafiki wa mume/m penzi wako wa zamani utaanzaje na kuishaje? Utaanzia wapi na kuishia wapi? Utajiridhishaje? Vipi mtu akikutongoza mtaani humjui, utaanza kwa kumpa hojaji ya kuonesha uhusiano wake wote yeye kumhusu huyo mume/ mpenzi wako wa zamani? Vipi kama yeye si rafiki wa mume/ mpenzi wako wa zamani, lakini ana rafiki ambaye ni rafiki yake?

Vipi kuhusu wajane? Mwanamme akifa napo rafiki zake hawaruhusiwi kumuoa mke wa rafiki yao aliyefariki? Au wanaruhusiwa? Kwa sababu gani?

Watu wengine wanaishi katika jamii ndogo ya vijiji ambavyo watu wote wanajuana na kila mtu ni rafiki wa kila mtu.

Na hawa nao utataka wakiachika wasiolewe au kuwa na mahusiano na kijiji kizima? Wahame kijiji kwa sababu wameachika?
 
Last edited:
Hapo hujajibu kitu. Kanuni ipi ya mahusiano? Inasemaje? Uhalali wa kanuni hiyo unatokana na chimbuko gani?

Ngoja ninyumbulishe.

Kuwa na mahusiano na ndugu yako wa karibu ni jambo baya.

Kwa kanuni za misingi ya kidini. Limekatazwa. Mtu anakataa kwa sababu za dini.

Hata kama mtu hakubali dini kama mimi, kanuni za kibaiolojia zinatoa sababu za kutokuwa na uhusiano na ndugu yako wa karibu, kwa sababu mnahatarisha genetic pool watoto kuwa na magonjwa.

Hivyo ni wazi kwamba, kiutu, ukaribu wa undugu unavyozidi, ndivyo jamii inavyoona mahusiano ya kimapenzi yanakuwa hayafai.

Hivyo basi, kuna sehemu hapo ukaribu huo unafifia mpaka mahusiano hayo yanaanza kuonekana yanaruhusiwa. Ndiyo maana kuna tamaduni nyingine, baadhi ya waarabu kwa mfano, unaruhusiwa kuoa au kuolewa na binamu yako.

Sasa, ukaribu huu wa kutokuwa na mahusiano unaishia wapi? Na unapotaka kuwajumuisha rafiki za mume/mpenzi wako wa zamani, unawajumuisha kwa minajili gani? Kwa uhalali gani?

Ndugu wanajulikana ni ndugubwa maisha. Hivyo katazo la kuwa nanuhusiano nanndugu wa karibu nibla maisha. Hao rafiki wa mume/moenzi wako wa zamani, wakisema wanavunja urafiki naye ili wawe nawe utawakubali? Vipi kuhusu rafiki zake wa zamani uliowajua ambao hana urafiki nao tena? Vipi kuhusu rafiki zake wa zamani ambao hukuwajua ambao wamepoteana hawana mawasiliano muda mrefu? Vipi kuhusu rafiki zake waliopoteana kutika darasa la kwanza? Vipi kuhusu rafiki za kaka yake ambao si rafiki zake? Vipi kuhusu rafiki za rafiki zake?

Uchunguzi wako wa nani atakufaa kwa minajili ya kutokuwa rafiki wa mume/moenzi wakonwa zamani utaanzaje na kuishaje? Utaanzia wapi na kuishia wapi? Utajiridhushaje? Vipi mtu akikutongoza mtaani humjui, utaanza kwa kumpa hojaji ya kuonesha uhusiano wake wote yeye kumhusu huyo mumeo/ moenzi wako wa zamani? Vipi kama yeye si rafiki wa mumeo/ moenzi wako wa zamani, lakini ana rafiki ambaye ni rafiki yake?

Vipi kuhusu wajane? Mwanamme akifa napo rafiki zake hawaruhusiwi kumuoa mke wa rafiki yao aliyefariki? Au wanaruhusiwa? Kwa sababu gani?

Watu wengine wanaishi katika jamii ndogo ya vijiji ambavyo watu wote wanajuana na kila mtu ni rafiki wa kila mtu.

Na hawa nao utataka wakiachika wasiolewe au kuwa na mahusiano na kijiji kizima? Wahame kijiji kwa sababu wameachika?
Kanuni ya mahusiano inasema mtu ambaye si ndugu wa damu mnapokuwa karibu kwa muda huo huyo anahesabika ni ndugu na huyo rafiki anakuwa ni msuluhishi wa migogoro pale unapotokea

Kwa nini anakuwa rafiki awe msuluhishi wa migogoro kuliko ndugu ili kusiwepo biasness

Unapokuwa na mtu kwenye urafiki huku ukiwa na wazo la kumchukulia mke au mume wake umekuwa umevunja kanuni ya mahusiano ni bora usingekuwa na mahusiano na huyo rafiki yako coz kupitia kwake ndo umenifahamu so bora umheshimu
 
Kwasababu wanapenda vitu vinyonge vilivyokufa !!

Pia kwasababu atatumia madhaifu ya jamaa yule

Kwasababu Mwanamke akiachana na mtu wake, Hatendi kwa Akili bali Hormone

kwasababu, anajua mwanamke sasa hayupo sawa kiakili kwaiyo nirahisi kumla.

Yotee kwa yotee, wanaume wengi wanapenda slope a.k.a mtelemko yaaan wanapenda vitu vinyonge ,visivyowasumbua!!
 
Kanuni ya mahusiano inasema mtu ambaye si ndugu wa damu mnapokuwa karibu kwa muda huo huyo anahesabika ni ndugu na huyo rafiki anakuwa ni msuluhishi wa migogoro pale unapotokea

Kwa nini anakuwa rafiki awe msuluhishi wa migogoro kuliko ndugu ili kusiwepo biasness

Unapokuwa na mtu kwenye urafiki huku ukiwa na wazo la kumchukulia mke au mume wake umekuwa umevunja kanuni ya mahusiano ni bora usingekuwa na mahusiano na huyo rafiki yako coz kupitia kwake ndo umenifahamu so bora umheshimu
Nimeuliza mswali mengi sana ambayo hujayajibu.

Ni wazi ukiwa na rafiki wa karibu aliyehusika kwa mengi kuna attachments nyingi ambazo zinaweza kufanya mahusiano naye yasiwe jambo zuri.

Hata kama unataka kuepuka drama tu.

Lakini hujajibu maswali yangu mengi sana.

Mathalani, vipi kuhusu rafiki anayeona kilichotokea si haki na akaamua kuvunja urafiki na rafiki yake huyo ambaye kamuona hayawani, na kuanzisha uhusiano na mwanamke kwa nia nzuri?

Huoni kwamba kukataza mahusiano hapo kunamnyima haki mwanamke ambaye atahitaji mahusiano na mwanamme ambaye atahitaji mahusiano, wakati pingamizi la urafiki halipo (mwanamme kashavunja urafiki).

Nilikuwa naangalia sinema moja, bosi alimpenda binti mmoja, lakini yule binti alikuwa muajiriwa wake. Bosi alipomtongoza binti, binti akakataa, kwa vile yule binti ni muajiriwa wa bosi . Na kanuni za kazi zinakataa mahusiano kati ya bosi na muajiriwa (dada zetu wengine chukueninsomo la kuheshimu kanuni za kazi hapo). Bosi akasema umesema vizuri. Jiuzulu kazi, nakufungulia biashara. Tuendeleze penzi. Kwa minajili hiyo, utakuwa moenzi wangu halafu pia nitakuwa sijavunja kanuni za kunitaka nisiwe na mahusiano na muajiri wangu.

Bosi alivunja kipingamizi kwa kumtoa binti kwenye ajira.

Rafiki akivunja kipingamizi kwa kumaliza urafiki wake, hapo itakuwaje?

By the way, I am analyzing this conceptually. I am not saying I am for this or that.
 
Back
Top Bottom