Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,891
Kwema Wakuu,
Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa kumuomba hela mtu aliyeajiriwa ni rahisi tofauti na aliyejiajiri. Yaani hata Kama Aliyeajiriwa analipwa pesa ndogo Mfano laki tatu, wataona ni Kheri kwani wanajua fika ifikapp mwisho wa mwezi utakuwa na laki 3.
Wakati ukijiajiri hawajui mapato yako, sio ajabu wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wakawa wanakupigia kelele uajiriwe, ni kwa sababu wanataka uhakika wa kuomba hela kwako.
Waliojiajiri ni rahisi kukimbia misumari na vibomu vya waombaji na wengi husema mambo ni magumu sana, waombaji huelewa.
Hata kutembelewa na ndugu, ni rahisi ndugu kumtembelea ndugu aliyeajiriwa kuliko anayefanya ujasiriamali, hata Kama mjasiriamali anapata pesa nyingi kuliko muajiriwa, Siri ni kuwa Aliyejiajiri mapato yake hayafahamiki.
Sio ajabu ukiajiriwa halafu ukatangaza kuoa mapema unaweza zua balaa kubwaπππ ndugu kukuzingua, huku wengine wakimpa taabu Mke/mume wakoπππββοΈπββοΈ
Nawasilisha