Wanataka kuachana kisa jina


Ameshiriki vipi kulea mimba wakati binti bado anaishi na wazazi? Hata kishika uchumba (posa) hajatoa? Ningekuwa mzazi wa huyo binti ningemweka lock-up huyo dogo kwa kumlaghai binti yangu.
 
halafu jamaa anatunisha misuli kuwa anamuacha,

hata posa hajatoa

kiufupi hafahamiki wala hana uzito hata kama alitoa nauli ya cliniki


Hii kali kweli, kibongo bongo kitendo tu cha kumpa mimba binti yangu bila kumuoa kwangu mimi ni tusi sembuse kumtafuta ashiriki kutoa jina?
 
huyo jamaa yako ni mtoto na hajakua......

na wala hakua na nia ya kuoa


 
Vp kama yana bahati! Hutaki abebe bahati zote.. Japo sikubaliani na urithishwaji wa majina ya babu/bibi/ndugu
Kama ni jina la sifa may it will be ok, but to me hata kama alikuwa malkia au mfalme mwanangu ni lazima awe na jina lake pekee ambalo sisi wazazi tutaridhia. Wanangu wa kiume niliwachagulia majina na wa kike mama yao. Of course tunakuwa na options za majina, tunayajadili na kupatikana moja au mawili. Mfano kila mtoto wangu ana majina mawili mawili. Mfano John Bosco, Erick Xavery, Mary Rose, Mary Theresia, Mary Blessings, etc.
 

Hujanielewa kabisa mkuu wangu, kwanza sina demu na kwa umri huu sina sababu ya kuwa naye na kuzaa haramu nje. Lingine nimesema majina tunakubaliana mimi na mke wangu, hakuna ndugu, wala mzazi aliyetusaidia kuzaa watoto na zaidi wa kiume huwa nawachagulia majina options nyingi na mwishowe tunachagua mawili na wa kike mke wangu anachagua options na tunakaa tunakubaliana majina matatu official kwa ubatizo na cheti cha mtoto. Si eti kwamba eti nachaguliwa ukweni, hakuna kitu kama hicho. Huyu jamaa mleta mada inaonekana huwa hawako karibu na huyo aliyezaa naye!!! Ni matatizo ya kuzaa watoto kabla ya ndoa!!! Mke kwa wazazi, kijana kwa wazazi!!! Sasa hapo si unategemea kuchaguliwa jina tu na wajomba na maanti. Chunga kuzaa kabla ya ndoa.
 
mkuu hii inanipa shaka kuna binti nimezaa nae ila japo hatuja owana plan nikwamba tutafunga ndoa.tatizo ni hilo jina nilimchagulia mwanangu jina la kislam na tukakubaliana tatizo yeye kamuita mtoto jina tofauti kabisa namuuliza lina maana gani anasema la mcheza mpira na kila nikimuomba cheti cha kuzaliwa mtoto lazima ugovi...smtime nahisi na pigwa mchanga
 

Sawa, lakini sasa mkuu majina mawili yote yanini wakati mnaweza kubaliana na mkeo mkampa mtoto jina moja tu

Walau lingekuwa moja hayo majina yenu ya kizungu lingine jina asilia; mtoto anaitwa john bosco yote yakupewa duh! Hivi kuna hata mzungu anaitwa Wema Bahati kweli!
 
wampe tu jina lolote lakini wasimuite mtoto "SNURA!"
 
Unajua kwenye mahusiano kuna pressure. Za chini kwa chini sasa linapotokea jambo dogo ndio watu hupata sababu ya kuonyeshana misuli au kutapika nyongo zao

Mimi ningeacha tu hilo jina walilompa ukifika wakati wa ubatizo nambatiza kwa jina tutalalokubaliana na mkewangu

Saa nyingine kuepusha zogo ni busara tu ndio itumike na kuepusha wapambe kujiingiza kwenye maswala binafsi
 
kama wamempa theresa na baba anataka kumwita irene,,,, amuna shida ni kufanya hivi unamwita irenetheresa High Vampire ugomvi unakuwa umeisha hivyo
 
huyo jamaa yako ni mtoto na hajakua......

na wala hakua na nia ya kuoa



mkuu yawezekana unaweza ukachukulia kitu kidogo ila kwa wengine kinakwaza hebu jiulize mahali imeshapanga na next wk tunaenda kutoa mahali kwa nini asishirikishwe jamaa anajiuliza yawezekana mtoto wa mwingine ndio alimewahi kutoa jina na kingine mama mtu ndio anasauti anahofu wakioana yeye atakuwa kama pambo
 
huyo jamaa zuzu, apeleke kwanza mahari ndio alete ubabe wake wa kizamani
 
Ameshiriki vipi kulea mimba
wakati binti bado anaishi na wazazi? Hata kishika uchumba (posa)
hajatoa? Ningekuwa mzazi wa huyo binti ningemweka lock-up huyo dogo kwa
kumlaghai binti yangu.

tulia wewe nyinyi ndio mnaokuja kuwa wazee nuks.kama jamaa alikuwa anatoa fedha ya matumizi huko ndio kulea mimba afterall jamaa hana haja ya kupanic coz mtoto kama ni wakwake atakuja tu siku hizi hakuna kugombania watoto.
 

ndugu yangu siyo kila mtu anapenda kuzaa nje ya ndoa na si vyema kumuita mtoto wa nje haram please.usiongee kwa kuwa hayajakukuta.
 
tulia wewe nyinyi ndio mnaokuja kuwa wazee nuks.kama jamaa alikuwa anatoa fedha ya matumizi huko ndio kulea mimba afterall jamaa hana haja ya kupanic coz mtoto kama ni wakwake atakuja tu siku hizi hakuna kugombania watoto.

Aoa kwanza, uzae mtoto wa kike halafu ndo uje ufikiri namna hii. Yaani lijitu limekaa mahali kazi yake ni kuharibu watoto wa watu ati anatoa pesa ya matumizi? Ujinga mtupu!
 
Kama hajatoa mahali hana mamlaka na mtoto upande wa kikeni ndo unamamlaka hadi atapotoa hiyo mahali.
 
ndugu yangu siyo kila mtu anapenda kuzaa nje ya ndoa na si vyema kumuita mtoto wa nje haram please.usiongee kwa kuwa hayajakukuta.

Du kweli, nimekuwa bias bila kufikiria jamii nzima. Pole sana if offended by this. Na wengine poleni pia. Ila sema ndilo jina la Kiswahili linalotumika and I did not mean to heart anyone. Again, sorry mkuu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…