Wanataka kuachana kisa jina

unayosema ni kweli
but,hiyo sababu inatosha kumuacha mzazi mwenzie? labda kama kuna mengine
 
Aseme alikuwa anatafuta sababu ya kumwacha huyu mwanamke. Yaani jina tu unahangaika? Ni mtoto wa kike au kiume? Tena kama ni wa kike mama ampe jina kabisa ili asijebandikwa jina la x girl friend na wa kiume baba ampe jina asijebandikwa jina la x. Tatizo mnataka kuwapa majina mazito ya mababu zenu na mabibi watoto wenu!!! wanaasili hata yale majini waliofuga!!! Watoto wangu hakuna hata mmoja ana jina la kurithi!!!! Vivyo hivyo alifanya baba na mama yetu na alituasa kabisa kutorithisha watoto majina, mengi yana mikosi kwa hiyo anabeba mikosi yote.
 

kwani mtoto si anaweza kupewa hata majina mawili au matatu! ampe jina takalo liwe la pili.au akiwa kwake atamuita hilo na kumzoesha ana akienda kwa bibi yake ataitwa la awali.
 
Kama wamemuita jina la ukoo hapo wamekosea ila kama ni ya kizungu hamna shida ili mradi isijekuwa demu kaita jina la mpenzi wake wa zamani.
 
Achen utani baba ndie mwenye nafasi ya kutoa jina au akishindwa anatoa idhin kwa mwanamke ili wampatie jina kinyume na hapo ni dharau na hata wakifanya lolote bado dam ya mtu haipotei hata cku moja ipo siku atawambia mm namtaka baba yangu. Kama ningekua mm naachana nao mwisho wa siku akikua namchukua kilain.
 
aisee! Chukua tano kabisa. Hata ningekuwa mm hapo nikuachana naye tu....... Wantapaje jina wakat baba wa mtoto yupo?! Kitendo cha kumpa wao jina inamaana wao ndio waliompa mimba mwanao........ Wakwe wengne sijui wakoje

mama mkwe kamaliza kumpigia simu jamaa anauliza baba mnakuja lini kutoa mahali jamaa katulia tu
 
Au afanye hivi siku ya mwanamke kwenda clinic ampatie jina alitakalo yy ndio liandikwe kwenye kad mfano Happy Daud badala ya Wema daud hapo ndio dawa.
 
Kama wamemuita jina la ukoo hapo wamekosea ila kama ni ya kizungu hamna shida ili mradi isijekuwa demu kaita jina la mpenzi wake wa zamani.

Hapo ndo huwa mitanzania inanishangaza kukimbilia kutoa majina ya kizungu utadhani kuna mzungu anaitwa jina la Kiswahili!!
 
Hapo ndo huwa mitanzania inanishangaza kukimbilia kutoa majina ya kizungu utadhani kuna mzungu anaitwa jina la Kiswahili!!

Hata jina liwe la Sum mnyama au majani kinacho takiwa litoke kwa baba au upande wa baba hata wakitoa shangazi zake bibi zake au wadogo zake kikubwa litoke upande wa baba. Kwa heshma na taadhima.
 

Vp kama yana bahati! Hutaki abebe bahati zote.. Japo sikubaliani na urithishwaji wa majina ya babu/bibi/ndugu
 
jamaa hata akikubaliwa kutoa jina , ndugu wa mke wataendelea kumwita jina lao!
Ni sawa na mke wa kakangu kwao wana jina lao wanalomwita na sisi tunalo letu yaan alilotoa mumewe!
 
mama mkwe kamaliza kumpigia simu jamaa anauliza baba mnakuja lini kutoa mahali jamaa katulia tu

ukweli ni kwamba jamaa yako wamemdharau sana, na inatakiwa awe na msimamo kama mwanaume asikubali kubuluzwa na wakwe
 
wanaume hamkosagi sababu, mtoto kubadilishwa jina haichukui hata siku , si akimhalalisha atampa jina alitakalo
 

utaratibu hauko hvyo mkuu. Baba wa mtoto anatakiwa ndiyo ampe jina au atoe idhin kwa mkewe au ndg yeyote atoe jina..... Hayo unayosema ww ni miongon mwa wanaume wachache wanaoburuzwa na wakwe zao ndio wanaweza kufanyiwa kama mawazo yako yanavyowaza, unaonesha kuwa ww hata dem akija kwako na ukamgonga leo halafu kesho akakwambia nina ujauzito wako na ww ukakubali
 
wanaume hamkosagi sababu, mtoto kubadilishwa jina haichukui hata siku , si akimhalalisha atampa jina alitakalo

Tatizo wanawake wa siku hizi sijui mkoje mnapenda kujipa madara ili muonekane mambo yakiharibiaka utasikia samahan hakuna hiyo ni dharau komaa mwanangu haiwezekani hopo tu bado hajamuoa akiowa si ndio atampanda kichwani. Achen kurahisisha mambo kiasi hicho bwana huu ni utan.
 
Kama alikuwa bado hajamuoa huyo mwanamke, hana haki ya kutoa jina ashirikishwe kutoa jina yeye kama nani?

kama nani?...kwani huyo mwanamke aliji.t.ia vidole ndio akapata huyo mtoto,unajua ni muda kiasi gani na pesa kiasi gani iliyomgharim kuhudumia hiyo mimba mpaka kutokea huyo mtoto...kama kuoa ndio case na kuwa hatambuliki kisa hajamuoa kwanini mlikuwa mnapokea matunzo ya mimba kutoka kwa huyo mwanaume?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…