MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,238
- 50,414
Huu ni ujinga ambao umenikera hadi basi, taarifa kwamba baadhi ya wanasiasa wetu wanakwenda Tanzania kutafuta nguvu za kishirikina ili kuwawezesha kushinda uchaguzi. Laana ya ovyo hii na maeneo mengine ya nchi yetu yataendelea kuwa nyuma miaka yote.
Bora ningeskia mnavuka mpaka kwenda kujadili uashirikiano wa kibiashara na mengineyo maana, mtailemaza nchi hadi lini, maeneo kama Migori ambayo yanaongoza kwa huu upuzi bado yapo nyuma kiuchumi.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Vifaa vya uchawi. Picha/MAKTABA
Na ELISHA OTIENO
Imepakiwa - Monday, May 22 2017 at 17:40
Kwa Mukhtasari
HUKU siku ya Uchaguzi Mkuu ikizidi kukaribia, idadi ya wawaniaji kutoka kaunti za Migori na Homa Bay wanaosafiri hadi Tanzania kusaka huduma za waganga imeongezeka lengo likiwa moja; kutwaa ushindi baada ya Agosti 8.
Wanasiasa hao wanaowania viti mabalimbali wamekuwa wakisafiri hadi miji ya Tarime, Musoma na Mwanza kutafuta usaidizi wa 'nguvu za kiza’ kuwawezesha kupata ushindi bila jasho.
Inadaiwa waganga hao wamekuwa wakiwapa wanasiasa hirizi ili kuwapokonya wapinzani wao wapiga kura. Wengi wa wawaniaji hao walianza kumiminika nchini Tanzania mwezi Februari kabla ya michujo kufanywa.
Ripoti ya 'Taifa Leo’ inaonyesha kuwa wanasiasa hao wanaamini kuwa waganga wana uwezo wa kuwahakikishia ushindi katika kinyang’anyiro cha Agosti.
“Wengi wa wawaniaji wanaamini kuwa hawawezi kupata ushindi bila usaidizi wa nguvu za kishetani. Tumekuwa tukiwaona wengi wao wakipitia hapa na kuingia Tanzania,” akasema Bw George Ogwang’, wakala wa ukaguzi wa mizigo katika eneo la mpakani la Isebania.
“Ninamjua mmoja wa wanasiasa ambaye alipokea huduma za waganga hao na bado akabwagwa kwenye mchujo,” akaongeza.
Bw Mohammed Yaya ambaye ni mganga wa mjini Tarime aliambia 'Taifa Leo’ kwamba ni kawaida kwa biashara kunoga kila mara Kenya inakaribia Uchaguzi Mkuu.
“Wao huja kupata huduma zetu na wanalipa pesa zozote ambazo tunawaitisha,” akasema.
Wasaidizi wa karibu wa wanasiasa mbalimbali walikiri kuwa waajiri wao huamini usaidizi wa waganga.
Itakuchukua saa nne kusafiri kutoka Migori hadi Mwanza lakini ni dakika 50 tu kwa gari la kibinafsi kusafiri hadi Tarime.
Bw Yaya alisema kuwa wanamtoza mwnasiasa pesa kulingana na kiti ambacho anawania lakini kiasi cha pesa hizo huweza kujadiliwa na kuafikiana.
Utumizi wa waganga ulianza wakati wa demokrasia iliyoruhusu vyama vingi nchini na visa hivi vimekuwa vikiripotiwa katika kanda zote za nchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Mnamo Novemba 1994, waziri wa zamani Musikari Kombo alipoteza kiti chake cha Ubunge wa Webuye baada ya mahakama kumpata na hatia ya kutekeleza kosa la uchaguzi kwa kusaka huduma za waganga.
Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha Ford-Kenya alishtakiwa kwa kuwalipa waganga wawili ili kuwapa wapiga kura kiapo kinachojulikana kwa lugha ya Kibukusu kama 'khulia silulu’ (kinamaanisha kula kitu chenye uchungu).
Kicheko kilizuka mahakamani wakati maelezo ya jinsi kiapo hicho kilipeanwa yalitolewa mbele ya majaji watatu waliosikiza kesi hiyo.
Maaskofu na makasisi wakiongozwa na kasisi wa kanisa la Deliverance Mark Kariuki wamewaonya wanasiasa dhidi ya utumizi wa uchawi, uganga na nguvu za kishetani katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti.
Walisema baadhi ya wanasiasa husafiri mataifa ya Kusini na Magharibi ya Afrika kutafuta hirizi.
Wanasiasa Wakenya wamiminika Tanzania kusaka ushindi Agosti