Wanasiasa wengi hawapohuru.Nikwamanufaa ya nani?

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,370
3,143
Awali ya yote nianze kwa kusema sijawahi kushabikia chama chochote cha siasa bali nashabikia hoja za wanasiasa bila kujali itikadi zao

Naomba nijikite kwenye mada ya leo kwa ufupi.
Nimekua najiuliza hivi nikwanini kundi hili maalum lililopewa majukumu mazito yahusuyo maisha ya wananchi (wengi wao)hawapo huru?

Kundi hili la waja wa Mungu kwaasilimia kubwa hawana uhuru wa kuongea/kutoa mawazo yao yanayokinzana na maelekezo ya vyama vyao.Ninasema hivyo kwasababu mara nyingi wabunge wengi wanasema natufanyeni hivi kwa manufaa ya chama chetu,kwamaelekezo ya mwenyekiti nk
Kibaya zaidi nipale ambapo kundihili la watu muhimu(wanaojiita waheshimiwa)wanajikita zaidi katika propaganda kuliko mahitaji na matarajio ya walio watuma(rejea mijadala mbalimbali kama vile maazimio ya bunge ya Richmond,Downs nk)Utaona mijadala hiyo kwaasilimia kubwa ilijikita kivyama zaidi kuliko uhuru wa mawazo isipokua kwa wachache waliopo guru kwanza kisha ndio vyama vyao

Kituko kikubwa ni juu ya mikataba ya kuliangamiza taifa kiuchumi ambayo ilipitishwa na kundikubwa la watu hao na wachache wakibaki kama walalamikaji,leo hii baada ya fikra mpya za mwenyekiti kuona tunaibiwa wale waliopitisha makubaliano hayo wamegeuka nakuwa sehemu ya utetezi wa wanyonge,heeeee jamani wananchi sio wasahaulifu kiasi hicho.Kinachoshangaza zaidi nikwamba mambo yamekua kisengere nyuma kwani waliopinga dhuluma hiyo mwanzoni leo wanaonekana ndio sehemu ya wanamakinikia,jamani hii sio haki

Nimalizie kwakusema kwamba wanasiasa msiteke mijadala kwa kigezo cha uwingi wenu na pia wachache wasinyamazishwe na viongozi kwakuatu ni wachache.Pia kueni watu huru kimawazo,misimamo na vyama vyenu ndipo vifuate kwani vyama vitapita bali Tanzania yetu itabakia

Nimetimiza wajibu kwakuisemea nchi yangu nisishambuliwe mimi ni mtu huru

Alamsiki
 
Ukiona mtu anaongelea sana uchama badala ya nchi,huyu sio mzalendo...
 
Back
Top Bottom