Wanasiasa na viongozi wa mkoa wa Kagera ni JANGA

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Ukifatilia historia ya nchi hii Tanzania mkoa wa Kagera ni mmojawapo wa mkoa iliyotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kuanzia Elimu,Siasa,Uchumi,Utamaduni na Wasomi wenye weredi.

Mkoa huu kwa kipindi kirefu ulitegemea kilimo, uvuvi, ufugaji,biashara pamoja uchukuzi mfano kilimo cha mazao kama kahawa,pamba,miwa na chai.
Kuna viwanda ambavyo vilikuwa vinatoa ajira kama Bukop, Tanica, Mamlaka ya Chai, Kagera Retco na KCU lakini cha ajabu mitaji hii imekufa na viongozi wote hamna mwenye kuonesha njia ya kutatua matatizo ya wananchi.

Wanakagera wengi hawana ajira rasmi, wengi wamejikita kwenye boda boda na kuuza viroba vya konyagi kutoka Uganda.
Wanakagera wengi hawana uwezo wa kupata maji safi na salama,umeme ndo usiseme,bidhaa ziko juu kuliko sehemu nyingine hapa Tz na wengi wanategemea bidhaa kutoka Uganda wakati Uganda hainunui any raw material kutoka Tz,sukari inayozalizwa mkoani humu inauzwa bei ya njuu mpaka 2500 kwa kilo,mafuta ndo usiseme.

Hii dhairi kabisa kuwa viongozi wa mkoa hawafai kwani hawana ata dira ambayo itaweza kuwakwamua wanakagera.
Rai yangu ni kuwa mkoa huu wananchi wasipo hamua kufanya mabadiriko hasa ya viongozi wa kisiasa wasahau maendeleo kabisa kwani ata UNSHOMILE HAUNA MAANA TENA

Wanajanvi thread imekuwa ndefu saana ila ninaomba uvumilivu na ninawasilisha.
 
Mkuu ni kweli kabisa,Kagera bado hasa wilaya za Bukoba vijijini, Misenyi, Ngara na Muleba bado wameikumbatia CCM kama ndugu zetu wa mikoa ya kusini! Heri kidogo Bukoba mjini na Karagwe. Kuna umuhimu CDM kufanya operesheni maaalum ktk mkoa wa Kagera. Binafsi ni mwenyeji wa mkoa huu,lakini unanitia aibu. Siyo kama enzi za miaka ya 60 na 70 ambako mkoa wetu ulikua na wanasiasa mahiri na wapenda maendeleo.
 
Back
Top Bottom