Wanasiasa na anasa: tumeliwa!


Rungu

Rungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2007
Messages
3,925
Likes
1,070
Points
280
Age
68
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2007
3,925 1,070 280
Wabunge wanapotunza fedha wacheza utupu - 1


Katika ukumbi maarufu wa muziki au kwa jina jingine ‘club' (jina linahifadhiwa) uliopo mjini hapa mengi yanatokea. Watu wanaingia mmoja mmoja, wengine kwa makundi na baadhi wapo nje wakipunga kwanza upepo kabla ya kuingia. Siku hii, wanawake wanaingia bure au kwa jina jingine ‘ladies free' jambo linalosababisha ukumbi huu ufurike watu. Katika ukumbi huu, yapo maeneo mawili. Kuna sehemu ya kawaida ambayo kiingilio chake ni kuanzia Sh5,000 hadi Sh10,000 kutegemeana na matukio au burudani ya siku hiyo.

Pia kuna eneo jingine ambalo ni kwa watu maalumu ama waweza kusema ni ‘VIP' ambapo wateja wake hutakiwa kulipa Sh20,000.

Ukumbi wa VIP upo juu na ule wa kawaida upo chini. Hata hivyo maeneo yote haya hujaza watu kwa kiasi kikubwa. Mwananchi limefika katika ukumbi huu wa VIP saa tano usiku, hata hivyo bado watu ni wachache katika eneo hili ukilinganisha na kule kwa watu wa kawaida.

Ukumbi wa VIP si mkubwa kieneo . Kuna kaunta ya vinywaji, makochi madogo madogo aina ya sofa yenye meza mbele yake, viti vilivyoizunguka kaunta na katikati ya ukumbi huu kuna meza mbili za duara zenye mti wa chuma katikati.
Kadri dakika zinavyojongea, ndivyo watu wanavyoendelea kumiminika mmoja baada ya mwingine.

Saa saba za usiku ndipo Mwananchi liliposhuhudia kiongozi mmoja wa kitaifa ambaye hekima zake zinategemewa na Serikali na hata chama chake akiingia katika ukumbi huu akiwa na mabinti wadogo watatu. Alipata nafasi ya kuketi, katika moja ya sofa zilizokuwa katika ukumbi huo, akaagiza vinywaji na kuendelea kunywa.

Muda wa saa saba, alitokea msichana aliyevaa sidiria na kisketi cha kujimwaga kifupi sana ambacho hata hivyo kiliuonyesha mwili wake waziwazi. Msichana yule alipanda katika moja ya meza za duara zenye chuma na kuanza kucheza muziki uliosikika katika spika za ukumbi huo.

Baada ya kucheza kwa zaidi ya nusu saa, alivua kisketi cha rangi nyeusi alichokivaa na kukirusha… akabaki na nguo ya ndani aina ya ‘bikini' ya rangi nyeupe, kisha akaendelea kucheza kwa kupandia vyuma katika meza hizo za duara. Baadaye alivua sidiria, akaendelea kucheza na kadri watu walivyokuwa wakimtunza fedha aliendelea kuonyesha ujuzi wake katika kucheza.

Baada ya muziki huo kukolea, msichana huyo alibadilisha mchezo, akalala kifudifudi na kuishusha nguo yake ya ndani hadi nusu ya makalio yake.

Wanasiasa waliokuwepo katika ukumbi huo pamoja na watu wengine walionekana kumpa fedha kwa kumwekea katikati ya makalio msichana huyo kadri walivyofurahishwa na uchezaji wake.

Uhondo wote upo hapa:
Source: Mwananchi

 
A

afwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Messages
4,087
Likes
111
Points
160
A

afwe

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2010
4,087 111 160
Pole mwandishi, ila kumbuka kuwa hao unao waita wanasiasa upo wakati pia huwa ni wananchi kama wengine walivyo na huhitaji kufurahia na kuona yale unayoyaona wewe hasa muda kama huo uliowaona.
 
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,115
Likes
649
Points
280
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,115 649 280
Kwa namna muandishi alivyoreport inaonekana hata yeye aliburudika kwelikweli.
 
Wingu

Wingu

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Messages
4,324
Likes
37
Points
145
Wingu

Wingu

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2011
4,324 37 145
Ndio huko huko wanakowapata wa kuzaa nao nje ya ndoa
 
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
3,304
Likes
48
Points
145
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
3,304 48 145
Ulikula kwa macho mwandishi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
S

salasala

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
219
Likes
8
Points
35
S

salasala

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
219 8 35
Acha wivu, hata wao ni binadamu kama wewe.
 
grafani11

grafani11

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Messages
15,526
Likes
370
Points
180
grafani11

grafani11

JF-Expert Member
Joined May 24, 2011
15,526 370 180
Huyo Mheshimiwa ukimkuta bungeni utasikia anavyopiga vita nguo fupi zisizo na heshima kwa utu wa mwanamke. Na wabunge wengine wa KE na ME wanampigia makofi na kuunga mkono hoja. LOL!
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
36,078
Likes
392
Points
180
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2011
36,078 392 180
He he he, ziz iz when private parts zikiwekwa usoni.
Wee mwenyewe ulikuwa unatizama ila hukuwa na hela ya kutunza.

Ungeziacha private kuwa private ungekuwa wa maana vinginevyo zinafaa udaku.
Ujue hata mtu awe na hekima na busara kiasi gani, ukiona na mtoto jua kuna mahali alichojoa.
 

Forum statistics

Threads 1,273,817
Members 490,485
Posts 30,492,935