mwanasiasa ambaye kazi yake ni kuchekacheka tu, kupiga makofi tu, hayuko serious, yeye kila kitu ndio kisa kimetoka upande wa chama chake ni bingwa wa kuzomea, akipewa nafasi kuongea basi yeye anakimbia wajibu wake wa kuikosoa, kuishauri na kuisimamia serikali, matokeo yake anakuwa mjibu hoja wa serikari, kwani wajibu hoja wa serikali hawapo? unakuwa msifiaji wa serikali, nini kinakutekenya, unatafuta nini? ubunge waliokupa wananchi haukutoshi, mbona unashusha hadhi ya bunge kwa tamaa zako, unafanya hivyo ili ,,uonewe huruma katika fursa mbalimbali, acha kuwa mbunge oppurtunist, unakatisha tamaa vijana, hufai kurudi tena bungeni, inatakiwa ukawe msema chochote (mc) huko sigimbi, ni aibu! mbunge umekaa kusifia tuuu! serikali acha mara moja! kwani mtu akifanya vizuri watu si wanaona au kuna sehemu wamesema mbunge kazi yake mojawapo ni kusifia serikali, we mbunge wa namna hii unajiaibisha, unaaibisha familia yako na jimbo lako pia, usitumie fursa ya wananchi wengi kuwa wajinga uamua kuongea au kufanya mambo ambayo siyo wajibu wako, usikubali kutumika la sivyo tuchunguze Elimu yako au tukakupime.