Wanasiasa Bhana! Hivi ni One Stop Center au ni business as usual?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Wiki jana nilikuwa Posta DAr kwenye hicho kituo ambacho wanasiasa wanakisifia eti ni "one stop center" ambacho kinahusisha Maafisa Biashara, watu wa Brela, RITA, TRA, NIDA, Benki ya CRDB na taasisi zingine.

Ukweli hao watu baadhi yao wana maneno yale yale kama ambavyo walikuwa kwenye Ofisi zao.

Sidhani hawa watu kama wanapata incentive za ziada ili kuwafanya wafanye kazi kwa kuacha mazoea. Wako slow na baadhi yao ambao wanaonekana wako active ni wale tu ambao wanatoka Taasisi zinazolipa vizuri lakini wengine ni zero kabisa.

Leo nimetembelea Dodoma One Stop Center bahati nzuri hapo hapajawa na mlundikano wa wateja kama Dar lakini wafanyakazi wake bado hawajaonekana kama wapo tofauti na wale waliopo kwenye ofisi husika. Ninachokiona sisi bado sana yaaani.

Huduma ambayo nilianza nayo Dar nikitegemea itaisha ndani ya majuma mawili sasa inaoenekana itaisha baada ya miezi mitatu au mine.

Ninarudi Dar bila mafanikio ya asilimia 100. Bongo yetu hiyo - siasa mingi sana!
 
Huu upuuzi ndio ulimuondoa yule bwana wa Kigamboni. Upigaji juu ya upigaji na fedha za mradi zilitoka nje.
 
Mkuu hawanaga jipya, bongolala ni vituko mwanzo mwisho.....ngoja tuone uongozi wa machifu chini ya chifu hangaya kama utaleta uelekeo mpya.
 
Back
Top Bottom