Wanasheria Wapiga dili v/s Wabunge wa kujua Kusoma na kuandika=Mikataba ya Wizi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,771
7,138
Wana JF,

Sakala lililohewani kwa sasa, ni maajabu sana kuona wanasheria nguli A. Chenge na Jaji Welema AKA Mr. Tumbili wakiwaya waya kujiokoa dhidi ya lawama zilizotanda kila kona, wapo nao kwa machozi ya mamba kuungana na watanzania kumsifu JPM kuwa alichofanya sawa lakini huku wakikataa kuwa kiasi kinachosema sio sahihi.Hawa kweli walisomeshwa kuharibu nchi yetu au urafi ndio umewafanya hivyo. Mwl Nyerere alisema " madini/ dhahabu sio nyanya kwamba itaoza, kwanza wape watu Elimu wajue technologia ndio muanze kuchimba", aliwambia kama huna vifaa vya kuyahakiki mzungu atakugeuza zuzu atachukua kitu kizuri na kukuachia mashimo, hawakusikia, sijui hapa BWM aliingiwa mizuka gani kutuingiza mkenge kama huu. Ona sasa Rais wetu analia, watanzania tunalia, kila sehemu kilio. Hawa watu wana mabilioni wameficha nchi za nje, wanayafurahia tu kwakuhesabu trakimu huku hayatusaidii, reli ya kati kwa sasa kila Rais anayekuja kututembelea ni lazima atembezewe bakuli. wakati sisi tulitakiwa kuanza kutoa misaada.

Je, Tuendelee kuwa na wabunge wa kujua kusoma na kuandika? Je, hawa wataweza kupitia mistari moja hadi mwingine wa mikataba ulioandikwa kwa kiingeleza? Tuje kwa hawa wakuu wa Mikoa. Juzi mmoja alikataliwa kuingia migodini, uenda alishidhwa kujieleza kwa kiingeleza yakatokea mabishana, tunavyojua Mkuu wa mkoa ndiye Rais wa mkoa , huyu mwekezaji anawezaje kumzuia wakati yeye alienda na mkuu wa usalama (polisi) wa eneo hilo.
 
Back
Top Bottom