mwambunnyara
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 518
- 206
Ni mke wa kaka yangu amekuwa akifundisha shule ya sekondari Mgulasi,iliyopo manispaa ya Morogoro.
Shemeji yangu huyu pamoja na kuwa wako 2 tu wanaofundisha fizikia shuleni kwao,lakini Mkuu wake wa shule amemfanyia zengwe za ajabu kwa sababu tu alihoji mapato na matumizi ya shule kwenye kikao.
Matokeo yake,shemeji yangu huyu aliuguliwa na mtoto,usiku(ilikuwa ghafla) akalazimika kumpeleka mtoto hospital, asubuhi akaandika barua ya kuomba ruhusa akiwa hospital,akampatia madam mwenzake ampelekee kwa Mkuu wake wa shule.
Mkuu wake alipokea barua na kuificha bila kuweka kwenye file,na akaanza kumuandikia "NO ANY INFORMATION" kwenye daftari ya mahudhurio,zilipotimia siku tano,akapeleka taarifa kwa afisa elimu,ilipofika tarehe 01/03/2016 akaletewa barua tatu na Mkuu wa shule,barua hizo zilikuwa...
1.TUHUMA ZA UTORO KAZINI
2.BARUA YA KUJIELEZA KWANINI ASICHUKULIWE HATUA
3.BARUA YA KULIMWA MSHAHARA WAKE,(NUSU MISHAHARA)
Barua zote tatu,zimeandikwa siku moja,01/03/2016.Baada ya kupokea barua hizo alienda kwa afisa elimu wake kutafuta ufafanuzi wa jambo hilo akamtimua,alipoenda kwa mkurugenzi kutafuta haki yake hakupata fursa hiyo,aliambiwa mkurugenzi yupo busy sana.
(kwa zaidi ya mwezi wiki mbili hakupata msaada wowote) Hatimaye mwisho wa mwezi wa tatu mshahara wake ukafyekwa,akakuta kuna nusu mshahara,akaamua KUACHA KAZI.
MPAKA SASA MGULASI SEKONDARI ILIYOPO MOROGORO MANISPAA YENYE WANAFUNZI 1034 INA MWALIMU MMOJA TU WA FIZIKIA,ETI KISA MWALIMU KUHOJI MAPATO NA MATUMIZI YA SHULE, KWA MWENDO HUU TUTAFIKA?
Kwa hiyo situation hapo wakuu,mnamsaidiaje shemeji yangu huyu kisheria imekaaje!?