Wakuu habari.....
Nimekuwa ni msomaji tu wa JF kama guest. Lakini baada ya kunikuta nikaona nijiunge nipate msaada maana hapa hakuna kinachoshindikana,
Iko hivi nina mwanangu wa kiume umri miaka 33..! Huyu kijana ndio nilikuwa nikimtegemea haswa aje kusimamia mali zangu siku nikiwa sipo, na nilikuwa namuamini sana.
Sasa mwezi uliopita nilimuagiza akauze kiwanja changu mahali, na kwakuwa namuamini nikamruhusu pesa zilipwe kwa bank acc yake, cha ajabu baada ya kuwekewa pesa akatoweka na kunipa taarifa kwamba anaenda kutafuta maisha yake. Nikamkatalia na kumwambia kistaarabu arudishe pesa ila aligoma katakata na mpaka sasa simu zake zote hazipatikani.
Sasa nahitaji kumfungulia kesi atafutwe arudishe pesa lakini pia afungwe japo miezi 6 iwe fundisho kwa wadogo zake.
Nahitaji kujua nifuate taratibu gani kisheria zitakazonipa uhalali wa kufanya hayo ninayo yataka. Msaada wenu muhimu wakuu.