Wanasheria msaada: Nimedhamiria kumshtaki na kumfunga mwanangu wa kumzaa

Mbane

Member
Jun 6, 2022
33
64
Wakuu habari.....

Nimekuwa ni msomaji tu wa JF kama guest. Lakini baada ya kunikuta nikaona nijiunge nipate msaada maana hapa hakuna kinachoshindikana,

Iko hivi nina mwanangu wa kiume umri miaka 33..! Huyu kijana ndio nilikuwa nikimtegemea haswa aje kusimamia mali zangu siku nikiwa sipo, na nilikuwa namuamini sana.

Sasa mwezi uliopita nilimuagiza akauze kiwanja changu mahali, na kwakuwa namuamini nikamruhusu pesa zilipwe kwa bank acc yake, cha ajabu baada ya kuwekewa pesa akatoweka na kunipa taarifa kwamba anaenda kutafuta maisha yake. Nikamkatalia na kumwambia kistaarabu arudishe pesa ila aligoma katakata na mpaka sasa simu zake zote hazipatikani.

Sasa nahitaji kumfungulia kesi atafutwe arudishe pesa lakini pia afungwe japo miezi 6 iwe fundisho kwa wadogo zake.

Nahitaji kujua nifuate taratibu gani kisheria zitakazonipa uhalali wa kufanya hayo ninayo yataka. Msaada wenu muhimu wakuu.
 

0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
3,448
8,281
Kuna wazee unaweza kuwa unafanya nao kazi lakini malipo yako yanakuwa ni chakula tu ukitaka kuondoka anakuzuia lazima kuna siku utafanya tukio tu.

Iko hivi, ukiwa na vijana wako mna biashara fulani mfano kwa mwezi mnaingiza million kijana unaweza kuwa unamtoa hata laki 3, lakini kuna wazee wanabana sana.

Ila sipo kumtetea kijana wako maana alilolifanya siyo sahihi, kama hiyo hela ya kiwanja haijakuathiri sana kiuchumi achana nae na fanya ni kama mmemalizana hana chake tena kwako.
 

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
1,967
4,886
Tatizo wazee mmezidi ukoloni sana. Kama kijana kaamua kwenda kupambana muache tu. Mpe baraka zote maana matunda ya hayo mapambano bado atakuka na wadogo zake.

Ila sijui kumfunga, kumpa laana nk hayo unaongeza tatizo juu ya tatizo halafu ni kijana ambaye bado unampenda ....Mpe baraka za mafanikio kunjua moyo kwani hayo mafaniko atakula na wajukuu zako ambao bado ni muendelezo wa kizazi chako.

Stay positive mzee. Mali bado zipo mikononi mwako.
 

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,538
3,153
We mzee una roho mbaya kwa damu yako!!! Yaani unataka kijana wako aanze kupambania kombe wakati wewe ushakufa...bila ya shaka utakuwa ni mzee wa kichaga.

Mpe baraka mwanao ,mwache akajitafutie maisha na usiache kumuombea kwa Mungu afanikiwe huko aendako. Inaonekana wewe ni wale wazee wa kikoloni ,wakali kupindukia ,mna kausemi chenu cha kueni myaone!!!

Kijana ana miaka 33 na unajinasibu kuwa una mali ila hata milioni moja hujawahi kumpatia mwanao wa kiume wa kwanza ???
 

Ngishi

JF-Expert Member
Sep 17, 2018
216
358
Maoni yangu hayajakaa kisheria.

Ni hivi mkuu, kama ni mwanao wa kumzaa na background yake kiakili yuko vizuri, yaani hana tatizo lolote la kiakili basi fanya kama umetoa SADAKA, mwache akapambanie kombe lak
Ningekuwa Mimi ningemuacha Ila ktk Mali nilizonazo Sasa ningetafuta mwanasheria na kuandika wosia wa kwamba ikitokea Mimi na mke wangu wote tukafa Mali furani apewe mtoto Fulani Mali ile apewe yule kila mtoto na Mali yake nagawa kabisa mwisho naandika mtoto Fulani ambaye ndio amekimbia na hela asipate chochote kwny mgao wa Mali zangu yeye alishachukua chake wakati wa kuuza kiwanja Cha sehemu Fulani bila idhini yangu.Hapo bila wosia hata ikitokea ukafa atakuja kuwasumbua wenzake
 

Abuu Said

JF-Expert Member
Jul 5, 2015
4,017
4,616
Kuna shida hapa, ulimpa kipaumbele kusimamia mali zako...wewe ukataka kuuza hizo mali na hukumpa mpango mkakati baada ya kuuza hicho kiwanja hiyo pesa mnaitumia kwenye nini 😒 ungemueleza kwamba pesa inayopatikana tunafungua biashara na wewe ndio utaisimamia asingefanya hivyo kwahiyo yeye kaamua kujiongeza huwenda katafuta mtaji wa biashara aizungushe hiyo pesa then akurudishie pesa yako na yeye abaki na biashara yake. Usimfunge mpaka ukae nae chini pale atakapo patikana uone alikuwa na lengo gani
 

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
4,040
6,014
Tujue kwanza ni kiasi gani kaondoka nacho usijekuta tuna hangaika kukushauri humu kumbe hela yenyewe 5m au 10m ndo unayotaka kwenda kumfunga mwanao.

Ambaye umemnyima fursa na kumfuja mpaka amefikia miaka 33 hana mbele wala nyuma kwa kumtumia tu kwa matakwa yako.
 

Mbane

Member
Jun 6, 2022
33
64
Inaonekana unamwamini lkn ujamtengenezea naye mfumo wakupataa mali zakee, penginepo amechokaa kila cku kukuomba omba elfu kumi na laki ..
Mkuu tuachane na hayo mimi nataka kujua nianzie wapi kumkamata hayo mengine yatajulikana baadae....! Ila lengo langu arudishe pesa na kumfunga
 

Mbane

Member
Jun 6, 2022
33
64
Wakuu huo ushauri mnaonipa sijui nimuache sio kitu nilichokuja kuhitaji humu...! Maana hilo familia na ndugu wamenishauri ila nimewakatilia kata kata siwezi kumuacha aondoke na mali yangu, akatafute zake kama mimi nilivyohangaika kuzipata
 

Mbane

Member
Jun 6, 2022
33
64
Ina onesha bado alikua anaishi home na wewe una mfanya kama toy lako kwa kumuendesha kama mtoto
Ndio nilikua naishi nae, na alikua ananisimamia moja ya biashara yangu. Sikutaka aondoke nyumbani kwanza mpaka aoe maana vijana wakienda kujitegemea bila kuoa ni tatizo mkuu
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,868
3,606
Si bora huyo kaondoka na fedha za malipo ya kiwanja.
Huku kuna mwingine Mzazi wake Amestahafu - Fedha Penseni zilivyoingia Benki tu, Mwanae anaijua password ya Kadi ya Benk, Kaiba kadi kisha kaenda kukwangua mzigo wote kisha kasepa
 

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
5,134
4,773
Utakuwa ni psychopath na labda ndo maana mtoto katoroka, yaani damu yako unataka ifungwe Jela ?

Mimi Damu yangu hakuna kosa kubwa, hata anifanyie nini, she is always welcome back home maadamu bado naishi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Top Bottom