Wanasheria msaada: Nimedhamiria kumshtaki na kumfunga mwanangu wa kumzaa

Utakuwa ni psychopath na labda ndo maana mtoto katoroka, yaani damu yako unataka ifungwe Jela ?

Mimi Damu yangu hakuna kosa kubwa, hata anifanyie nini, she is always welcome back home maadamu bado naishi!
Huyo ni wewe.....! Mimi sina falsafa hizo
 
Si bora huyo kaondoka na fedha za malipo ya kiwanja.
Huku kuna mwingine Mzazi wake Amestahafu - Fedha Penseni zilivyoingia Benki tu, Mwanae anaijua password ya Kadi ya Benk, Kaiba kadi kisha kaenda kukwangua mzigo wote kisha kasepa
Hawa watoto wa siku hizi sijui wamerogwa na nani
 
Wakuu habari.....

Nimekuwa ni msomaji tu wa JF kama guest. Lakini baada ya kunikuta nikaona nijiunge nipate msaada maana hapa hakuna kinachoshindikana,

Iko hivi nina mwanangu wa kiume umri miaka 33..! Huyu kijana ndio nilikuwa nikimtegemea haswa aje kusimamia mali zangu siku nikiwa sipo, na nilikuwa namuamini sana.

Sasa mwezi uliopita nilimuagiza akauze kiwanja changu mahali, na kwakuwa namuamini nikamruhusu pesa zilipwe kwa bank acc yake, cha ajabu baada ya kuwekewa pesa akatoweka na kunipa taarifa kwamba anaenda kutafuta maisha yake. Nikamkatalia na kumwambia kistaarabu arudishe pesa ila aligoma katakata na mpaka sasa simu zake zote hazipatikani.

Sasa nahitaji kumfungulia kesi atafutwe arudishe pesa lakini pia afungwe japo miezi 6 iwe fundisho kwa wadogo zake.

Nahitaji kujua nifuate taratibu gani kisheria zitakazonipa uhalali wa kufanya hayo ninayo yataka. Msaada wenu muhimu wakuu.
Mzazi anatakiwa kuandaa maisha bora kwa ajili ya uzao wake. Ukishindwa kuwekeza kwa watoto wako;ambao ndio urithi wako, ni hatari sana. Na matokeo yake ndio kama hayo.

Vumilia tu. Utasahau hayo maumivu muda si mrefu. Hakuna kitu chenye thamani duniani kama watoto. Wasiokuwa nao na wangetamani kuwa nao, wanatamani wapate hata kama huyo tapeli.

Japokuwa, malezi uliyomlea yanaweza kuwa chanzo cha hayo yote. Ukipata nafasi soma hatua za makuzi toka kwa mwanasaikolojia erick erickson
 
He! pyschopath tena kwa fedha zake mwenyewe! Kwa kweli alivyofanya ni ukosefu wa adabu na hasa kama anao na ndugu zake.

Haujui the whole story, labda ni Baba katili na irresponsible kwa watoto? Wakati mwingine watoto hawana jinsi wanavumilia mateso na inafikia muda wanasema inatosha wanakinukisha.

Mtoto aliyelelewa vizuri na kupata malezi bora na upendo hawezi kumuibia mzazi wake hata siku moja.

Na Baba mwenye upendo kwa mtoto wake hawezi mfunga jela mtoto wake damu yake mwenyewe eti kumkomoa na hapo ndipo psychopathy inapoingia!
 
Maamuzi ya huyo mwanao yanaonesha dhahiri kuwa bado alikuwa tegemezi kwako.
Miaka 33 si haba!!
Huenda akilini mwako ulimtegemea kuja kumiliki mali zako lakini haukumtengenezea njia yake binafsi ya kujipatia kipato. Hivyo ni rahisi kwake kudhani kuwa amesahaulika.

Ushauri; Mwache akajaribu bahati yake. Akirudi kwa kushindwa kupambana na maisha, mpokee tena. Halafu umpe ABC's.
 
Wakuu huo ushauri mnaonipa sijui nimuache sio kitu nilichokuja kuhitaji humu...! Maana hilo familia na ndugu wamenishauri ila nimewakatilia kata kata siwezi kumuacha aondoke na mali yangu, akatafute zake kama mimi nilivyohangaika kuzipata
Kumbe wewe ni boya kwani ofisi za wanasheria huzijui.....? Au unataka kuyuchosha tu
 
Ukimpeleka mahakamani nae atatoa maelezo yake, akishindwa kujitetea anahukumiwa Kama wezi wengine. Masuala yakusema hoooo afungwe miezi sita hayakuhusu, mahakama inaweza kumpiga mvua 4 au 8 huwezi kuipangia mahakama adhabu.

Kitendo Cha kusema arudishe pesa na afungwe miezi 6 inaonesha bado unahuruma dhidi yake hivyo muache na maisha yake. Kwasababu mpaka Sasa hiyo pesa Hana iliyokamilika, ameshapunguza nauli na kujipanga kimaisha kabla hajaanza biashara zake. Ukimpeleka mahakamani ndugu waliokushauri umsamehe ndio watakao muwekea dhamana, hivyo utaweka ufa kwenye familia.

Huyo mtoto hatujapata maelezo yake huenda akisimulia alivyopambana hapo nyumbani tunaweza kuona hata alichochukua ni kidogo.

Hata ukifungua kesi mahakamani watawaomba mkakae kifamilia Kwanza muyamalize na mzee ukizingua kwenye vikao vya kifamilia, adhabu anapunguziwa yaani atahukumiwa kwenda jera miezi minne bila ghalama au alipe faini ya elfu 50. Yaani hata mia hupati na dogo analipa faini na kesi inakua imeisha.

Nawachukia watoto wasio na adabu lakini siwapendi wazee mabahili Kama wewe.
 
Shukrani...! Angalau we umenipa mwanga, sasa kumpata ndio mtihani maana namba zake zote hazipatikani
 
Wakuu huo ushauri mnaonipa sijui nimuache sio kitu nilichokuja kuhitaji humu...! Maana hilo familia na ndugu wamenishauri ila nimewakatilia kata kata siwezi kumuacha aondoke na mali yangu, akatafute zake kama mimi nilivyohangaika kuzipata
Baba najua una hela ndio, ila kijana nina miaka 33 hujaniwekea msingi wa maisha yangu hadi nadiriki kutoroka na hela zako huoni tatizo lipo kwako? Tusilaumiane baba tena kuwa makini na mimi!

Wazee kama nyinyi dawa yenu ninayo mimi.
Kwa taarifa yako unayemtafuta ndio mimi na huwezi kunifanya kitu! Sanasana ukinifuatilia nakugeuza msukule maana nakujua nje ndani
 
Kijana wake yupo Facebook kule haijui jf labda Kama unamjibia.
 
Wakuu huo ushauri mnaonipa sijui nimuache sio kitu nilichokuja kuhitaji humu...! Maana hilo familia na ndugu wamenishauri ila nimewakatilia kata kata siwezi kumuacha aondoke na mali yangu, akatafute zake kama mimi nilivyohangaika kuzipata
Umgemuacha toka ana miaka 23 akaenda kutafuta mpaka sasa angekuwa na chake. Asingekuja kuiba hela ya kiwanja. Pengine mpaka sasa angekuwa na familia. Lakini umemfuja, labda hata laki hujawahi kumpa, leo ameuza kiwanja amejilipa kiinua mgongo ametambaa.

Muache aende, alichochukua ndio mshahara wake
 
Hawa wazee sometimes miyayusho kijana kaona ajilipe mafao yake mapema
 
Ningekuwa Mimi ningemuacha Ila ktk Mali nilizonazo Sasa ningetafuta mwanasheria na kuandika wosia wa kwamba ikitokea Mimi na mke wangu wote tukafa Mali furani apewe mtoto Fulani Mali ile apewe yule kila mtoto na Mali yake nagawa kabisa mwisho naandika mtoto Fulani ambaye ndio amekimbia na hela asipate chochote kwny mgao wa Mali zangu yeye alishachukua chake wakati wa kuuza kiwanja Cha sehemu Fulani bila idhini yangu.Hapo bila wosia hata ikitokea ukafa atakuja kuwasumbua wenzake
Naona unamshauri mzee mwenzako ujinga....unajua Mali aliyonayo mtoa mada? Je unafahamu kauza kiwanja cha tsh ngapi?
Unataka kuniambia kwamba wewe hujawahi kukosea katika makuzi yako....na je hatua Kali zingechukuliwa kama unavyoshauri hapa ungekuwa hapa jf?
Msiharibu familia za watu kimasihara....kumkuza mtoto hadi 33yrs sio jambo dogo.
 
Msiharibu familia za watu kimasihara....kumkuza mtoto hadi 33yrs sio jambo do
Unataka kuniambia kwamba wewe hujawahi kukosea katika makuzi yako....na je hatua Kali zingechukuliwa kama unavyoshauri hapa ungekuwa hapa jf?
Msiharibu familia za watu kimasihara....kumkuza mtoto hadi 33yrs sio jambo ddo

Naona unamshauri mzee mwenzako ujinga....unajua Mali aliyonayo mtoa mada? Je unafahamu kauza kiwanja cha tsh ngapi?
Unataka kuniambia kwamba wewe hujawahi kukosea katika makuzi yako....na je hatua Kali zingechukuliwa kama unavyoshauri hapa ungekuwa hapa jf?
Msiharibu familia za watu kimasihara....kumkuza mtoto hadi 33yrs sio jambo dogo.
Usijibu kwa mihemko toa ushauri wako ww Kama hujaelewa comment yangu pita sio lazima ukaandika Kama huna Cha kuandika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom