Wanasheria mnahitajika hapa

Wanasheria mnahitajika hapa

Asante kwa ushauri mkubwa,
Thamani ya mali zake zote anafahamu, kuhusu risiti jamaa anasema zilikuwepo katika draw ya dressing table ila hiyo dressing table mwenye nyumba pia aliuza..!!
Msaada wako kisheria kuhusu hilo Jambo la risiti unahitajika sana ndugu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Anaweza kurudi kwenye maduka aliyonunua hizo mali zake.....najua ni ngumu inaweza kuwa alinunua zamani sana na hayo maduka pengine hayapo...but penye nia pana njia .....hizo risiti atafute atapata
 
Mambo muhimu ya kuzingatia.
Baada ya kujua vitu vyake havimo ndani ya nyumba na kupata ushahidi kwa majirani na serikali ya mtaa. Kwanini hakwenda kutoa taarifa kwa polisi?
Mkataba wake wa kodi unaisha lini na baada ya yeye kuhama huyo mwengine kahamia baada ya muda gani?
Anao ushahidi wa vyeti vya mkewe kama alikuwa akiumwa?
Kwanini ifike mwaka ndio aende kudai vitu vyake?
Alicho kifanya landlord ni ujambazi kwasababu alikataa kuchukuwa vitu mwanzo baadae kakubali, huo ni ujambazi hapo angeweka ripoti polisi landlord agewekwa ndani kwa ujambazi.
Rafiki yako kwa sasa anatakiwa akusanye ushahidi wote kutoka kwa majirani,serikali ya mtaa na kwenda polisi kufungua kesi ya madai pamoja na wizi kwa landlord wake.


Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Asante kwa ushauri mkubwa,
Kwa mujibu wa Jamaa anasema ushahidi wa majirani upo, pia mkataba haukuwa umeisha ndio ilibakia deni la laki moja katika mwezi huo wa mwisho uliobakia.
Jamaa hakwenda polisi mara ya kwanza sababu anasema hakujua ili Jambo lingefikia katika hii Hali.
Pia kuhusu kukaa mda mrefu kuchukua vyombo ukisoma vizuri mada utaona maelezo na sababu ya kuchelewa kuja kuchukua vyombo.
Ila bado msaada wako kisheria unahitajika ili huyu ndugu yetu aweze kupata haki yake kisheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaweza kurudi kwenye maduka aliyonunua hizo mali zake.....najua ni ngumu inaweza kuwa alinunua zamani sana na hayo maduka pengine hayapo...but penye nia pana njia .....hizo risiti atafute atapata
Asante kwa ushauri,
Ila nafikiri hilo ni jambo lingine, ila Jambo la kwanza ni kumshauri aende kuwasilisha kesi yake ya madai.
Pia ushauri wako bado unahitajika sana ndugu katika hili Jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri,
Ila nafikiri hilo ni jambo lingine, ila Jambo la kwanza ni kumshauri aende kuwasilisha kesi yake ya madai.
Pia ushauri wako bado unahitajika sana ndugu katika hili Jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
Nisikilize vizuri.... huwezi kufungua shauri la madai wakati huna vielelezo/ risiti nilizokutajia hapo juu....
Otherwise...mtashindwa kuthibitisha kesi yenu ....kwa maana ya gharama ya vitu vilivyoharibika ...mahakama inatoa fidia kulingana na gharama halisi/specific damages ambazo zitathibitishwa na risiti za manunuzi ya hizo mali zilizoharibika
 
Nisikilize vizuri.... huwezi kufungua shauri la madai wakati huna vielelezo/ risiti nilizokutajia hapo juu....
Otherwise...mtashindwa kuthibitisha kesi yenu ....kwa maana ya gharama ya vitu vilivyoharibika ...mahakama inatoa fidia kulingana na gharama halisi/specific damages ambazo zitathibitishwa na risiti za manunuzi ya hizo mali zilizoharibika
Asante kwa ushauri ndugu,
Umeeleweka vizuri, nitafikisha ujumbe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hta wanaume wa mikoani wakishakaa Dar mwaka mmoja2 na wao wanakua wa uko uko! yani mimi kama hii story ni kweli nadhani saiv mngekua mnasoma uzi wenye kichwa cha hbri tofauti na hii kuhusu uyo mwenye slop yake iyo,

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi ndugu,
Ili Jambo linasikitisha Sana ndio maana nimelileta kwa ushauri hapa JF kabla jamaa hajachukua hatua yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ILI KUBALANCE STORY MLETA MADA FANYA MPANGO TUPATE NAMBA YA MWENYE NYUMBA HAPA HAPA ISIWE SIRI...
 
Mnakuja kuomba ushauri mlishaharibu? Nataka kujua jamaa yako he alifunga Nyumba akaondoka na ufunguo ama? Au ufunguo alimwachia mwenyewe Nyumba?

Kama alienda na ufunguo mwenye Nyumba akabomoa hiyo ni case, house break.

Elezea vizuri tupate pa kuanzia
 
Mnakuja kuomba ushauri mlishaharibu? Nataka kujua jamaa yako he alifunga Nyumba akaondoka na ufunguo ama? Au ufunguo alimwachia mwenyewe Nyumba?

Kama alienda na ufunguo mwenye Nyumba akabomoa hiyo ni case, house break.

Elezea vizuri tupate pa kuanzia
Jamaa anasema funguo aliondoka nayo, kwa hiyo mwenye nyumba alivunja mlango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂 😂 😂 😂
SIYO STORY NI JAMBO...
Hi sio story ndugu ni jambo limetokea kweli, na nilitaka kujua lengo la kuomba namba ya mwenye nyumba nini hasa?
Watu wa chumba cha habari wanaita story kaka, kama wewe unaita ni jambo.

Alafu kubalance ni kusikia na upande wa pili unasemaje badala ya malalamiko ya ndugu yako tu, hii ndiyo italeta UHAMUZI nitakao toa uwe wa haki bin amani kwa wote.
 
Dah! kuna watu wanaendekeza sana njaa

Huo ni wizi, karipoti polisi mzee akamatwe afunguliwe mashtaka taratibu nyingine ziendelee, kwakuwa umesema mashahidi wapo, ni vyema ukaandaa vielelezo muhimu kama mkataba wa kupangishina nyumba na risiti za vifaa.

Inawezekana hivyo vifaa vingine hajaviuza amevificha mahali anasoma upepo mkilemaa ndio aviuze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za jumapili wadau?
Nimeandika kwa kifupi ili iweze kueleweka, pia naomba usome hadi mwisho ili uweze kuelewa vizuri.
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Iko hivi kuna rafiki yangu alipanga nyumba eneo la Tabata jijini dar es salaam, wakati anaendelea kukaa katika hiyo nyumba akaonana na dalali na kumwambia Kama akipata nyumba ambayo ina vyumba viwili vya kulala amjulishe sababu anategemea kuhamisha familia kutoka Moshi na kuja dar hivyo atahitaji nyumba ya kutosha zaidi kwa familia,
Baada ya wiki mbili dalali akarudi na kumwambia rafiki yangu nyumba imepatikana ila rafiki yangu akamwambia dalali Bado hajafanikiwa kupata pesa na pia sehemu anayokaa bado pango la miezi miwili halijaisha hivyo dalali asubirie,
Dalala akarudi kwa mara ya pili kwa rafiki yangu akiwa na huyo mwenye nyumba kubwa mpya, mwenye nyumba akamwambia rafiki yangu naomba amia kwenye nyumba na utakuwa unanilipa laki mbili kila mwisho wa mwezi lakini rafiki aligoma na akasema kwa wakati huo hakuwa na pesa na pia sehemu anayokaa bado Kodi ya miezi miwili haijaisha, ila mwenye nyumba alimbembeleza rafiki yangu aamie hivyo hivyo na pesa atakuwa analipa taratibu, rafiki yangu ikabidi akubali kwa sababu yule mwenye nyumba alikuwa anaumwa hivyo pia alikuwa anahitaji pesa kidogo kwa ajili ya matibabu.

Sasa tatizo lilianzia hapa rafiki yangu alifanikiwa kulipa kwa miezi miwili ila kwa mwezi wa tatu alilipa laki moja na ikabaki laki moja, hapa mwenye nyumba akaanza utata anakuja kwa rafiki yangu anaongea lugha za kejeli na mda mwingine anaenda na wajumbe ila mjumbe akisikiliza maelezo anaona yule mwenye nyumba ni mkorofi.

Rafiki yangu akapata dharula mke wake akajifungua kwa operation na matatizo kibao hivyo ikambidi arudi Moshi kuangalia familia hivyo ikambidi hata biashara afunge ili amuuguze mke wake kwa ukaribu zaidi. Ikumbukwe huku nyuma aliacha deni la laki moja.
Baada ya wiki mbili akataka kumpa funguo mdogo wake ili akaangalie nyumba na pia akalipe deni Dar es salaam, ila kabla hajafanya hivyo akampigia sim jirani yake kujua maendeleo ila jirani yake akamwambia mwenye nyumba kaja kuchukua vyombo vyake na nyumba ni tupu, baada ya miezi miwili jamaa alivyoona mke wake amepata nafuu ikabidi aende Dar kujua hatma ya vyombo vyake,

Alivyofika, mwenye nyumba akamwambia jamaa hajui vyombo vyake Nani alichukua jamaa akauliza majirani na pia mjumbe ila wote wakamwambia vyombo alichukua mwenye nyumba jamaa akarudi tena kwa mwenye nyumba ila mwenye nyumba anagoma kusema ukweli vyombo vilipo ili siku ziendelee kuongezeka kwa kuwa jamaa hakuwa na makazi mengine dar es salaam ikabidi arudi Moshi na biashara ya dar es salaam akaifunga rasmi baada ya kurudi Moshi jamaa alitafuta kazi nyingine ambapo alipata biashara ya kupeleka mzigo Kenya hivyo mda mrefu alikuwa Nairobi mda mwingine Moshi kwenye familia sababu mke wake bado Hali haikuwa nzuri.

Akipata mda wa siku chache kuja dar bado mwenye nyumba anagoma kusema kwamba alitoa vyombo na wakati majirani wote wanajua alichukua vyombo ni yeye kwa kuwa alikuwa anafikia nyumba ya wageni akawa anashindwa kufatilia hilo Jambo kwa ukaribu, hivyo ikabidi aende kwenye ofisi ya mtendaji kule nako taarifa zilipofika akaambiwa vyombo alichukua mwenye nyumba, mwenye nyumba ndio akakubari kwamba kweli alichukua hivyo vyombo na akataka fidia ya miezi karibia kumi na moja ambayo alikaa na vyombo na wakati baada ya kutoa vyombo katika hiyo nyumba alipangisha, rafiki yangu akasema yeye hawezi kulipa ela yeyote sababu vyombo havikuweko ndani ya nyumba aliyopanga. Hivyo rafiki yangu akatoa laki moja aliyokuwa anadaiwa na laki moja nyingine ni Kama usumbufu kwa kuhamisha vyombo, ila mwenye nyumba akagoma akasema anataka laki tano, hivyo mwenye nyumba akasema anapokea hiyo laki mbili ila atatoa baadhi ya vyombo na vyombo vingine atavitoa baada ya hiyo laki tatu kumalizika rafiki yangu kuona hivyo akaona ni bora akubali sababu vyombo vyake ni vya thamani kubwa ukilinganisha na hiyo ela kumbuka hayo makubaliano yanafanyika ofisi ya mtendaji kabla rafiki yangu ajaona vyombo vyake.
Sasa rafiki yangu alivyofika kuona vyombo balaa likaanzia hapo kumbe mwenye nyumba vyombo aliviweka kwenye store ya nje ambayo haijasakafiwa kakuta vyombo vimeharibika karibia vyote kuanzia jagi la umeme, feni ipo vipande vipande, neti ya vyuma nayo imekatika nguo zimeoza, mashuka yameoza kwa unyevu, ndoo zilikuwa zinatumiwa kuchanganyikiwa rangi, vyombo vya chakula vina marangi, kitanda kilianza kuoza sababu ya unyevu kwenye hiyo store. vitu alivyovikuta salama ni vile ambavyo mwenye nyumba alikuwa anatumia Kama godoro. Ila vitu vingine Kama Samsung flat screen inch 32, HP printer, Friji kubwa milango miwili, oven, sofa seti, full HP computer desktop n.k mwenye nyumba alishauza. Jiko la gesi kakuta linatumika mwenye nyumba kagoma kutoa sababu eti mtungi una gesi hivyo hadi uishe.
Madai ya mwenye nyumba ni kwamba amefanya hivyo ili kufidia mda aliokaa navyo hivyo vyombo na ni Kama mwaka na wakati vyombo alivitoa kwenye nyumba ila alivichukua kuvitumia na vingine havikuwa sehemu salama na vingine aliviuza na nyumba alipangisha mda mfupia baada ya kutoa vyombo.
Rafiki yangu kaona hawezi kulipa hata hiyo laki tatu iliyobakia sababu vitu vyake vingi vimeharibika na vingine havipo.

Sasa wanasheria na pia wadau wengine wenye uzoefu na haya mambo tunaomba msaada juu ya hili Jambo ili huyu rafiki aweze kupata vyombo vyake na pia kuelimishwa uhalali wa hili Jambo.
Pia ni hatua gani ziweze kufatwa ila haki ipatikane.
Natanguliza shukrani za dhati, hili jambo ni serious jamani naomba masihara yasiwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
MKOME

WAKATI.WACHAGA WANANUNUA 20*30 KMR.MKAONA WAJINGA EEH..MNASHINDA BAR.BADALA YA KUJENGA KAZI MNAYOOO..STAREHEYADENI KULIPA.MWANASHERIA ANAJUA

AMEKOSA LAKI YAMWENYENYUMBA MWANASHERIA ATAMLIPA NA MAWE...???ACHUKUE.NKE.WARUDI.KIJIIJIM KUJIPANGA
 
Angelipa yasingemkuta hayayootee ndioomaana WENGINE KWENYE mkataba tunaandika mpangaji akishindwa kulipà mmilki ana HAki ya kukamata Mali .kufidia denilake na malipo yoyote ya ziada yatakayotokea

Hapooo namaanishà usafiri wakubeba utàlipà
Na serkl zamtaa wakisema per day vitu vyako kulinda ßh kadhaa utàlipa tu
 
Back
Top Bottom