Wanasheria/Mawakili nanyi "Mkisurrender" basi tumekwisha!

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,138
13,826
Wakuu,

Hakuna kitu kibaya kama kutawala nchi ukiwa haujiamini, unakuwa kiongozi uliejawa na woga na ku 'react' vibaya kwa kila kitu kinachoonekana kuwa ni Pinzani kwako.

Unakuwa Sensitive kupita kiasi kwa kila aina ya critism inayokuja upande wako.

Na ndicho kinachoendelea kwenye Utawala huu. Wamefanikiwa kuwafunga midomo (kwa kuwatisha) Makundi karibia yote ya kijamii ambayo ndio yanayotegewa kama "Kisemeo cha Wasio na Sauti"(The voice of the voiceless). Na wao wakakubali Yaishe hivyo kuamua 'Ku-Surrender' na kukaa kimya huku wakiacha ikiwa 'paralysed'.

Walianza Ku-Surrender Wasomi wa kada mbalimbali, Wakaja Wanaharakati, Wakaja Waandishi wa Habari, Wakaja Viongozi wa dini na Sasa Wabunge.

Kundi Pekee lililobakia ni WANASHERIA/MAWAKILI, Kundi hili nalo likiamua ku-Surrender basi ndio Mwanzo wa Taifa kuwa Kimya. Na duniani kote hakuna ukimya ulioleta maendeleo. Ni kweli kwa Mabavu tunakubali kukaa kimya, Ila rohoni tunaongea sana kwa rohoni hakuna wa kutunyamazisha.

Watafanikiwa kwa kutumia nguvu za dola lakini hawatafanikiwa kwa kutafuta suluhu za matatizo yanayotukabili.

Na kwasasa hakuna Utawala wa Sheria bali wenye nguvu ndio wenye Sheria.

Kuna Wakati Kuipenda Serikali iliyopo Madarakani Sio Uzalendo na Kuna Wakati Kuichukia Serikali Iliyopo Madarakani Ndio Uzalendo. Kuichukia au Kuipenda Nchi Ni Tofauti Kabisa na Kuichukia au Kuipenda Serikali.
 
Tupambane na ukweli.

Ukweli ni kwamba wabunge yale ndiyo maisha yao mshahara wao na marupu rupu mengine yanayosababisha tuone wanavyong'ara vinatokea pale (siyo wote).

Leo hii wamesikia bunge kuvunjwa hakuna ambaye yupo tayari kuona bunge likivunjwa mostly ni kwa sababu wengi wao hawana uhakika kama kesho uchaguzi ukiitishwa upya watarudi bungeni, hivyo wanakubali kulinda ajira yao kwa hii miaka iliyobaki.

Cha darasani kinasema raisi anaweza kuvunja baraza la mawaziri siyo bunge, akivunja bunge kutaenda sambamba na kususpend katiba hapo maana yake tumekua dictatorial regime kamili.

Kama anataka tuingie hadi huku kisa kudai uhalali wa utambulisho wa mtu basi naungana na Mdee anayeshangaa kwani Mkulu anapewa nini na Makonda.
 
Watu wa kila idara wananyamazishwa kwa vitisho vikubwa sana.Mawakili maisha ya watanzania yapo mikononi mwenu.
 
Ninawaambia mpaka kesho wakoloni weusi wakiona hakuna namna wanawezatumia propaganda chafu kumuweka mtu wao basi kwenye uchaguzi wategemee polis watakuja kuharibu mambo ukumbini.....tena wapo uchaguzi unafanyikia kwenye mkoa wa kale ka bwana mdogo kaliko hifadhi akili lumumba.
 
Wakuu,

Hakuna kitu kibaya kama kutawala nchi ukiwa haujiamini, unakuwa kiongozi uliejawa na woga na ku 'react' vibaya kwa kila kitu kinachoonekana kuwa ni Pinzani kwako.

Unakuwa Sensitive kupita kiasi kwa kila aina ya critism inayokuja upande wako.

Na ndicho kinachoendelea kwenye Utawala huu. Wamefanikiwa kuwafunga midomo (kwa kuwatisha) Makundi karibia yote ya kijamii ambayo ndio yanayotegewa kama "Kisemeo cha Wasio na Sauti"(The voice of the voiceless). Na wao wakakubali Yaishe hivyo kuamua 'Ku-Surrender' na kukaa kimya huku wakiacha ikiwa 'paralysed'.

Walianza Ku-Surrender Wasomi wa kada mbalimbali, Wakaja Wanaharakati, Wakaja Waandishi wa Habari, Wakaja Viongozi wa dini na Sasa Wabunge.

Kundi Pekee lililobakia ni WANASHERIA/MAWAKILI, Kundi hili nalo likiamua ku-Surrender basi ndio Mwanzo wa Taifa kuwa Kimya. Na duniani kote hakuna ukimya ulioleta maendeleo. Ni kweli kwa Mabavu tunakubali kukaa kimya, Ila rohoni tunaongea sana kwa rohoni hakuna wa kutunyamazisha.

Watafanikiwa kwa kutumia nguvu za dola lakini hawatafanikiwa kwa kutafuta suluhu za matatizo yanayotukabili.

Na kwasasa hakuna Utawala wa Sheria bali wenye nguvu ndio wenye Sheria.

Kuna Wakati Kuipenda Serikali iliyopo Madarakani Sio Uzalendo na Kuna Wakati Kuichukia Serikali Iliyopo Madarakani Ndio Uzalendo. Kuichukia au Kuipenda Nchi Ni Tofauti Kabisa na Kuichukia au Kuipenda Serikali.
Hizi kampeni uchwara za kuingiza siasa uchwara kwenye taaluma kupitia TLS, hazina tija kwa Taifa na nchi yetu. Hatuzitakiii!!!!
 
Back
Top Bottom