Wanasheria: Mahakama ya mafisadi itakuwa final?

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,363
2,000
Naomba kujua kama mahakama ya MAFISADI ndiyo itakuwa final katika kesi zitakazofikishwa kwake. Au mtuhumiwa ana nafasi ya kukata rufaa Court of Appeal.
 
MESOYA

Senior Member
Aug 19, 2014
150
250
Hiyo ndio siasa, hasa katika baadhi ya mataifa yasiyo thamini utawala wa kisheria.
Ni ukweli usiopingika kwamba mahakama zetu zipo imara na zimesheheni wasomi wenye weledi. Na kazi zake kuu kwa miaka mingi toka Uhuru ni kutafasiri jinai zote dhidi ya Jamhuri.
Sasa sijui hapa labda neno 'UFISADI' ndio jipya. Lakini kisheria yote hii ni jinai, na mahakama haijawahi shindwa toka kuanza kuhudumu kazi zake.
Wazo la msingi hapa ni kuishauri serikali kuziboresha mahakama zetu na kuwajengea masilahi bora watendaji wake.
Kauli ya Raisi kuokoa fedha za umma ianzie hapa.
 
mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,283
2,000
Mie nilikuwa najiuliza hivi hii Mahakama ya mafisadi itakuwa Na Sheria tofauti Na zilizopo za jinai? Pia nilikuwa najiuliza hivi Mahakama zilizopo zimeshindwa kushughulikia kesi za ufisadi mpaka iundwe Mahakama ya mafisadi?
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,363
2,000
Mie nilikuwa najiuliza hivi hii Mahakama ya mafisadi itakuwa Na Sheria tofauti Na zilizopo za jinai? Pia nilikuwa najiuliza hivi Mahakama zilizopo zimeshindwa kushughulikia kesi za ufisadi mpaka iundwe Mahakama ya mafisadi?
Kutafuta sifa tu! There is no need of having another division of the high court specif for economic crimes the so christened "mahakama ya mafisadi". Kitakachotokea hapa ni kuwapandisha mahakimu wasio na sifa/hawajafikia viwango waweze kuhudumu katika makahama hiyo maana majaji hawatoshi!
 
Wise1

Senior Member
Dec 6, 2012
186
250
Mie nilikuwa najiuliza hivi hii Mahakama ya mafisadi itakuwa Na Sheria tofauti Na zilizopo za jinai? Pia nilikuwa najiuliza hivi Mahakama zilizopo zimeshindwa kushughulikia kesi za ufisadi mpaka iundwe Mahakama ya mafisadi?

Nafikiri issue kubwa iko kwenye sheria zetu tulizonazo Katika mantiki hii,sheria zinatoa adhabu ndogo au zisizolingana na kosa husika (magnitude of the OFFENCE),Unakuta aliyepatikana na hata ya Kuiba Tsh.100,000/= anahukumiwa adhabu inayolingana na Yule Anayekuja patikana na hatia ya Kuiba Tsh.1Billion.
Siwezi kuifahamu hasa nia ya Yule mwanzilishi wa Mahakama hii Ila tumpe Muda Tuone mipango yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom