WANASHERIA: Hivi ni sahihi Rais kudukua mawasiliano ya wateuliwa wake?

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Mh rais amekiri kuwa ameagiza watu wake kurekodi (kwa lugha ya kitaalamu kudukua) maongezi ya mawaziri na makatibu wakuu ili apate ushaidi wa kuwafukuza.

Nimesoma katiba nzima sikuona sehemu iliyoandikwa eti kulalamika ni kosa la jinai au la kawaida. Sasa huu udukuzi anaoufanya Mh. rais hauvunji haki za binadamu??

Wanasheria nisaidieni,
 
Pesa hazitoshi kutekeleza majukumu yako Wizarani si uache kazi?

Wahuni wenyewe wa Bungeni wamerudisha pesa za Vitafunio na Safari za nje unafanya Mchezo!

Nyumbaa ya Shetani imevamiwa na Chizi ishi kwa tahadhari!
 
hakuna cha ajabu hapo huo ndio utaratibu dunia nzima, sisi wengine tu na ukapuku wetu bado vi-email vyetu vinasomwa ndio isiwe mawaziri ambao ni watendaji wa juu kabiasa hapa nchini. unafikiri ataendeshaje nchi. kwa kupiga ramli au kuota?
 
Ukawa kila mkimchokonoa magufuli hamumpati
Alichosema yeye so kudukua,kaagiza watakapo to a kauli hizo warekodiwe

Ukawa mnapaswa kuja kivingine baada ya kutupa Sera ya kupinga ufisadi
 
Mh raisi amekili kuwa ameagiza watu wake kurekodi (KWA LUGHA YA KITAALAMU KUDUKUA) maongezi ya mawaziri na makatibu wakuu ili apate ushaidi wa kuwafukuza.
Nimesoma katiba nzima sikuona sehemu iliyoandikwa eti KULALAMIKA ni kosa la jinai au la kawaida. Sasa huu udukuzi anaoufanya Mh raisi hauvunji haki za binadamu??

WANASHERIA NISAIDIENI,
UDIKTETA. KWENDA. MBELE
 
kwa utawala huu uwe makini kuropoka ropoka ovyo inaweza kugharimu hata kile kidogo ulichobaki nacho.
 
Kuna wakati inabid iwe hivyo kwa usalama wa nchi mana bila kufanya hivyo utajuaje kama flan ni mwizi au jambazi na napopanga Milan to yake utajuaje, unapomtilia shaka lazma umdukue tu haina namna
 
Pesa hazitoshi kutekeleza majukumu yako Wizarani si uache kazi?

Wahuni wenyewe wa Bungeni wamerudisha pesa za Vitafunio na Safari za nje unafanya Mchezo!

Nyumbaa ya Shetani imevamiwa na Chizi ishi kwa tahadhari!
we jamaa nooma
 
Mh raisi amekili kuwa ameagiza watu wake kurekodi (KWA LUGHA YA KITAALAMU KUDUKUA) maongezi ya mawaziri na makatibu wakuu ili apate ushaidi wa kuwafukuza.
Nimesoma katiba nzima sikuona sehemu iliyoandikwa eti KULALAMIKA ni kosa la jinai au la kawaida. Sasa huu udukuzi anaoufanya Mh raisi hauvunji haki za binadamu??

WANASHERIA NISAIDIENI,

Hata kama ame kili bado yetu hizo ni kazi ambazo hufanyika na usalama wa taifa nchi yoyote ile inafanya hata kama usipo ambiwa jua hilo, tusishangae nyie hilo ni jambo la kawaida ila kwa wale wapiga madeal ndio watakao pata shida.

Wanasheria hao hao wengi wao ndio wataalamu wa kupindisha vipengere vya sheria sasa na wao lao laja

Alisha semaga ndani ya chama chao CCM kuna wanafiki sasa wacha wachunguzane maana kuna wengine hawataki jinsi anavyo ongoza Taifa hili.

My Take,

Tumejisahau saaana katika nidhamu na utendaji jamani watu tulisha bweteka mmnooo kupita maelezo kila kitu nunua toka nje acha CCM waisome namba
 
kiongozi wa serikali ,bunge,au mahakama kama anapewa simu au anapewa posho kwa ajili ya simu au mawasiliano ruksa kudukua simu zake zote sababu zinagharimiwa na pesa za walipa kodi
 
Ukawa kila mkimchokonoa magufuli hamumpati
Alichosema yeye so kudukua,kaagiza watakapo to a kauli hizo warekodiwe

Ukawa mnapaswa kuja kivingine baada ya kutupa Sera ya kupinga ufisadi
Ukawa wametoka wapi? Wao UKAWA ndio sera zao zinatekelezwa halafu waje na vimeo tena hapa? Wako kimya kwa sasa, ukiona kitu anachofanya Magufili kinamkera mtu basi ujue ajue yu karibu kutumbuliwa au kajipu kanakaribia kuiva,.

Ndugu zangu watanzania hii vita ya ufisadi haina chama, mbona wengi wanaotumbuliwa ni wa upande wa CCM? Lazima tumsupport Mtume Magufuli
 
Umemuelewa vibaya sicho alichomaanisha,unajua kuna ile kulalamika na kunung'unika chini kwa chini sasa unaweza kuongea na mtu mkiwa pamoja halafu unasikia yashamfikia mwenyewe kumbe uliyekuwa unaengea naye ni mmbea au kwa jina lingine ni kipemba,kwahiyo mawaziri wasoropokeropoke hovyo wakidhani waliokuwa nao ni wema kwao,na watu wenyewe wanaweza kuwa madereva au wale wasaidizi wao
Kiongozi hatakiwi kulialia, na kama analialia wananchi watafanyeje?Itamsaidia kujua wateule wake wanaomsaidia na wanaomsaliti.
 
Back
Top Bottom