Wanasema vijana ajira ni kilimo. Hebu jiulize kama Serikali iko serious

hewamkaa

Member
Mar 30, 2023
46
83
Nyakati tulizo nazo sasa ni za kilimo cha kisasa. Kilimo cha technology. Nyakati hizi ni za kutumia viuatilifu na teknolojia zingine.

Hebu jiulize, ni vijana wangapi wanaweza gharama hii? Yaani 500,000/= kwa mafunzo ya siku 3 ya viuatilifu? Na hapo ujitegemee chakula na malazi! Mafunzo haya yanafanywa na taasisi ya Serikali. Hawa wanalipwa mishahara na kodi zetu.

Hivi wameshindwa namna ya kuwafikia waTanzania kwa gharama nafuu? Mbona kuna semina na training kubwa zinafanyika, tena mpaka walengwa wanalipwa posho. Kwa hili Bashe kakwama wapi? Serikali inashindwa wapi?

Ukiangalia gharama ya mafunzo ni mtaji tosha. Kwa anayeweza kulima mahindi ekari moja, ni gharama tosha mpaka kuvuna. Kwa anaelima nyanya, gharama hiyo ni sawa na robo eka. Kweli tutafika?

Hivi Serikali imeshindwa kuyawekea ruzuku mafunzo haya ili Watanzania wafaidike wengi?
Screenshot_20231010_033203_Facebook.jpg
 
Huo ni utapeli wa wazi.
Kuna changamoto ya kuunza bidhaa nnje ya nchi hasa kama SI Asili/Halisi/hai/organic .
Ukiangalia ni swala la kibiashara zaidi na Lengo SI kimwezesha mkulima Bali kumfilisi.
Njia mbadala ni nyingi sema labda serikali inafanya Siri na kumbuka hata vyuo vikuu wadhamini wa baadhi ya program ni watengeneza viuatilifu.
Tafiti ziko mitandaoni za kutosha jinsi ya kulima bila dawa Wala mbolea za viwandani.
 
Back
Top Bottom