Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,796
- 1,849
Wakulima wa tumbaku wajipatia mabilioni
Na Lucas Macha
1st October 2009
Shamba la tumbaku.
Wakulima mkoani hapa wamejipatia Sh bilioni 149 kwa kuuza tumbaku katika msimu wa mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi wa Bodi ya Tumbaku nchini, Vitta Kawawa wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Msimba na Ibili kilichopo Wilaya ya Uyui.
Kawawa, alisema kiwango hicho kimeongezeka maradufu kutoka Sh bilioni 60 ambazo wakulima hao walijipatia mwaka jana baada ya kuuza tumbaku.
Kawawa ambaye pia ni Mbunge wa Namtumbo mkoani Ruvuma, alisema wastani wa bei ya kilo moja ya tumbaku kwa sasa ni mzuri kwa kuwa inauzwa kwa Sh 2,500 kwa kilo.
Alisema wakulima wa tumbaku nchini wanaufaika na zao hilo kwani z ni imara na halijateteleka hasa katika kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi unaozikumba nchi mbalimbali duniani.
Mwenyekiti huyo yuko mkoani hapa kwa ziara ya kukagua maendeleo ya zao hilo na kuwahamasisha wakulima kuboresha kilimo hicho ili kuongeza kipato.
Korosho za Tanzania zatesa soko la dunia
Na Said Hamdani
3rd October 2009
Korosho.
Korosho za Tanzania zimeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika soko la Dunia katika kipindi cha mwaka jana, imefahamika.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini, Athumani Muhagama katika kikao cha kupanda dira ya bei ya zao hilo kwa msimu ujao.
Akizungumza katika kikao hicho kilichoandaliwa na bodi hiyo, Muhagama, alisema korosho hizo zilizozalishwa katika baadhi ya mikoa nchini ni ya Tanga, Mtwara, Lindi na Pwani zilishika nafasi hiyo ya kwanza mwaka jana kutokana na wakulima kuzingatia ushauri wa wataalam wa kilimo hicho na masoko.
Mkurugenzi huyo, alisema kwa sasa wakulima hao wana changamoto ya kuendelea kuboresha kilimo hicho na kuzingatia ushauri wa wataalamu ili zao hilo lizidi kuongoza mwaka hadi mwaka kwa ubora katika soko hilo.
Akizungumzia kuhusu mwaka juzi, alisema zao hilo halikufanya vizuri katika soko hilo kutokana na wakulima kuchanganya na takataka kwa lengo la kuongeza uzito.
Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Magalula Said Magalula, alisema uwezo mdogo wa baadhi ya viwanda nchini wa kubangulia korosho nchini ni chanzo cha wakulima kulazimika kuuza korosho ghafi nje ya nchi, imeelezwa.
Alisema endapo wadau wa kilimo hicho watajipanga upya kinaweza kuwa na faida kwa wote na kuongeza pato la Serikali. Katika kikao hicho wadau wamekubaliana dira ya bei iwe Sh 675 kwa korosho ya daraja la kwanza kwa kilo na Sh 580 kwa daraja la pili.
CHANZO: NIPASHE
MNAOSEMA HAJAFANYA KITU KWENYE KILIMO, NIPENI DATA ZETU. Najua hamtaleta data zozote zile zaid ya kusema kafanyaaa vibaya.
Basi hali kama hiyo iko katika mazao karibu yote, kama Mahindi, Mpunga, na Chai.
Kikwete anaweza!