Wanasayansi: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka

Wanasayansi: Ziwa Victoria lipo hatarini kukauka

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
_98945359_e9f9e58a-8365-43a7-b8c5-345051de1c46.jpg


Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa.

Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.

Mwandishi wa BBC anasema jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.


Chanzo: BBC Swahili
 
Umeleta taarifa ya maana sana, naamini bila kuchukuwa tahadhari hili janga lazima lije, na ndio maana Misri wanahaha huku na kule, kuanzia kwenye vyanzo vya Mto Nile mpaka mwisho wa maji yanapowafikia...Hata kuhakikisha ile mikataba ya Kikoloni itumike kulinda maji haya na vyanzo vyake..
Wanasayansi tena wanadai, vita vya baadaye vitakuwa ni sababu ya maji, kama mafuta na gesi sasa, tuchukuwe tahadhari raia wa dunia hii..
 
Historia inadai ziwa chad lilikuwa kubwa kuliko victoria, leo linaelekea kuwa bwawa. Hata mradi wa kuvuta maji vitoria kwenda mikoani, ni wenye akili kubwa wanaoweza kuona uzuri wa wazo hilo. Ukiitaka Misri itujengee mabwawa makubwa kila wilaya yenye uhitaji wa maji, ingependeza.
 
Haya mambo itakuwa tu ni nature inafanya yake.
Nilisoma sehemu kuwa mwaka 1940, hali ya ehewa ilikuwa chafu zaidi ya leo.
Kuna mtu anadai kuwa ziwa chad lilikuwa kubwa kuliko Victoria ila linakauka na kugeuka kuwa bwawa.
Kama ni kweli basi lilikuwa kubwa over 500 years ago na kipindi hicho uchafuzi wa mazingira ulikuwa mdogo kwakuwa waafrika tulikuwa tunaishi kwa kuadapt nature siyo kuituje nature iendane na sisi. Lakini kama bado lilikauka basi utaona kuwa ni nature.
Kuna wanasayansi wana argue kuwa global warming siyo sababu ya shughuli z kibinadamu, wao wanadai ni mfumo tu wa dunia ilivyoumbwa na siyo mara ya kwanza kutokea uwa inaenda joto linaongezeka viumbe wanakufa species zinapotea then process inaanza upya...
 
Kwahiyo sisi tutumie pesa na rasilimali watu kulitunza ziwa lisikauke halafu Egypt anatuzuia tusilitumie kwa matumizi ya kusambaza maji mikoa mbali mbali? ; sasa acha likauke halafu tuone huo mkataba wao unasemaje juu ya hilo
 
Hata kama mvua itaachwa kunyesha basi itapita miaka 50 ndipo likauke, wangesema kina cha maji kupungua sio kukauka Kiswahili itakuwa awakijui BBC
 
Uwezekano wa kukauka ni mkubwa. Kwanza ni basin lake kwa maana kina chake ni kifupi na upana ni mkubwa hivyo kuwa na surface area kubwa inayosababisha high evaporation
Pili ziwa Victoria lina mito michache inayoingiza maji. Mito mingi inapita, mfano mto Karega haumwagi maji bali unapita katikakati, Mto mkubwa ni Mto Mara tu nao umeanza kukauka. Mto Simiyu umeharibiwa sana kiasi kwamba badala ya kumwaga maji safi unamwaga maji machafu.
 
Isingekuwa chuki ya Nyerere dhidi ya wahayudi walitaka kuchimba kama ile misri suez canal kutokea ziwa victoria ingepitia Shinyanga Tabora Singida mpaka dodoma ili kuoandoa ukame kwenye mikoa hiyo akajifanya yeye ana huruma sana na Wamisri na Wapalestina akawa amegoma ila leo hii tungekuwa tunatoka mwanza mpaka dodoma na mitumbwi yetu
 
Uvuvi haramu unakaushaje maji ziwani? Ukisikia matango pori ndo hayo sasa ongezea na point hz
Forced labour
Land alienation
Low wages
Poor infrastructure
Oppression
etc
Ahaaaaa umenikumbusha history loh
 
View attachment 638737

Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa.

Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.

Mwandishi wa BBC anasema jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.


Chanzo: BBC Swahili
kuna kitu kinanitatiza, kumbe uvuvi haramu na uchafu hukausha maji!
itabidi nifanye hii kitu kwenye bahari nahisa nayo itakauka!
 
ile idadi alio isema mkulu ya samaki vipi -imepungua au imezidi kulingana na tafti-mshazoe sasa ila kizazi hiki ni kizazi cha kuhoji ,atuwezi kwenda na dira za watu baadh tuu kwa kuburuzwa kiakili-hilo ziwa litakuwepo na litaendelea kuwepo -
 
Back
Top Bottom