Wanasayansi watangaza kukaribia kupata tiba ya HIV

Wanasayansi watangaza kukaribia kupata tiba ya HIV

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,997
Reaction score
61,231
WANASAYANSI nchini hapa israel wanaamini wanakaribia kupata tiba ya kutokomeza virusi vya Ukimwi (VVU).

Imani hiyo imekuja baada ya timu ya watafiti kumaliza jaribio la kimaabara mwilini mwa binadamu, ambalo wanasema limetoa matokeo mazuri ya kushangaza.

Watafiti hao walitangaza jana kuwa katika hatua ya kwanza ya jaribio, dawa ijulikanayo kama Gammora ilitokomeza asilimia 99 ya virusi ndani ya wiki nne za matibabu.

Kampuni ya tiba ya Zion ya Israel imeshirikiana na Chuo Kikuu cha Hebrew cha Yerusalem na kampuni ya Sirion Biotech ya Ujerumani katika majaribio hayo.

Matokeo hayo ya kufurahisha yalionesha kuwa dawa iliua seli zilizoambukizwa VVU katika mwili wa mwanadamu bila kuathiri seli zenye afya.

Awamu hii ni ya kwanza ya majaribio, iliyotumia kiwango kidogo cha washiriki kwa kuanzia, ilitoa matumaini makubwa ya uwezekano wa tiba ya VVU, ambavyo viliibuka mara ya kwanza miaka 35 iliyopita.

“Matokeo ya kwanza ya kimaabara yalikuwa kinyume na matarajio yetu na yanatoa matumaini ya kupata tiba ya maradhi haya,” alisema Dk. Esmira Naftali, mkuu wa maendeleo wa Kampuni ya Zion.

Virusi hivyo hatari ambavyo kwa kiasi kikubwa husambazwa kwa njia ya kukutana kimwili, huambukiza seli za mfumo wa kinga ziitwazo ‘seli T’.

Julai na Agosti mwaka huu, wagonjwa tisa katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Ronald Bata nchini Uganda walipewa dozi za Gammora kwa wiki kati ya nne hadi tano.

“Sehemu kubwa ya wagonjwa walionesha kupunguza kwa mzigo wa virusi hadi kwa asilimia 90 wakati wa kipindi cha wiki nne za kwanza,” alisema Dk. Naftali.

Katika sehemu ya pili ya majaribio iliyofanyika wiki mbili baadaye, wagonjwa walipatiwa tiba ya ziada ya ARV kwa wiki nyingine nne hadi tano.

Matokeo yalionesha kwamba muunganiko wa tiba ulitokomeza hadi asilima 99 ya virusi katika wagonjwa hao katika wiki nne.

Wagonjwa walioshiriki katika majaribio hawakukumbwa na dalili za athari zozote zinazotokana na utumiaji huo wa dawa.

Wakati wa jumla ya wiki 10 za utafiti, wagonjwa wa makundi yote mawili walionesha ongezeko la idadi ya seli T, ambazo ni muhimu katika utendaji wa mfumo wa kinga.

“Kutokana na ukomo wa utafiti huu, tunafurahi kuwa tuko tayari kuthibitisha ufanisi wa dawa yetu katika awamu ya pili itakayoshirikisha idadi kubwa ya washiriki na kudumu kwa kipindi kirefu,” alisema Dk. Naftali.

Hata hivyo, wakati matokeo ya Gammora yakitia moyo, inaweza kuchukua miaka mingi kabla ya dawa hiyo kuwa tayari sokoni.

Majaribio na mapitio zaidi yanahitajika kabla ya tiba mpya kuthibitishwa rasmi kwa matumizi.
 
Naamini kuna watu watatuliza Akili zao na macho yao na kusoma uzi huu kwa umakini zaidi japo mm nimrshindwa nimesoma haya 3 tu nimechoka atakayesoma mpaka mwisho naomba anipe alichokipata kwa ufupisho
 
Sasa kimbembe uyo Doctor anayeaminika zaidi apo akifariki itakuaje Aiseee
 
Hizi story mbona zimezoeleka na haipatikani bado tunapeana matumaini tu na magonjwa mengine yanaibuka mf.Ebola ambayo inauwa kwa muda mfupi kuliko HIV
 
Hawa wanazo dawa ambazo ukimeza uwezi ambukizwa Ukimwi, pia wapo karibu kupata tiba kabisa ya ukimwi
http://www.gilead.com/
pia wenye nayo hii kampuni ni Wa israel
 
Hua tunawatenga Israel, Je tutakuwa na ubavu wa kuhoji dawa kama imetoka Uyahudi ??!! [emoji23] [emoji12]
 
Back
Top Bottom