Wanasayansi watamba kuhusu tiba ya Ukimwi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Leon Bahati
WATAALAMU wa afya wa kimataifa wamesema yapo matumaini ya kupata tiba na chanjo ya Ukimwi ya uhakika miaka michache ijayo.Walisema hayo kwenye mkutano wa 18 wa Kimataifa wa Kujadili Ukimwi na Jamii (IAS) uliofanyika mjini Rome, Italia, hivi karibuni na kuhudhuriwa na watafiti wa ugonjwa huo zaidi ya 5,000.

Taarifa ya IAS kwa gazeti hili, iliwanukuu watafiti hao wakisema, ni jambo la kujivunia kwamba hivi sasa wanaweza kutamka kwa kujiamini kuhusu matarajio chanya ya dawa ya Ukimwi, suala ambalo walikuwa hawathubutu kulinena hadharani miaka 15 iliyopita.

“Miaka 15 iliyopita, hata watafiti waandamizi walikuwa hawathubutu kutamka juu ya matarajio ya tiba au chanjo ya Ukimwi,” alisema Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Rais wa IAS, Profesa Elly Katabira.
Alisema hivi sasa wanasayansi wanathubutu kunena hadharani kuhusu tiba kutokana na maendeleo mazuri yaliyofikiwa kwenye tafiti mbalimbali zilizopo kwenye majaribio.

Profesa Katabira alisema mafanikio ya tafiti za tiba ya Ukimwi, yalianza kujitokeza mwaka jana na IAS imeendelea kutoa ushirikiano kwa watafiti hao sehemu mbalimbali duniani na yamekuwa ya kutia matumaini.

Kwa kuwa bado tafiti mbalimbali zinaendelea duniani, alisema anaamini wataushangaza ulimwengu kwa kuweka wazi mambo yote kwenye mkutano wa 19 wa IAS, utakaofanyika mwakani Washington, Marekani.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wataalamu waandamizi waliohudhuria mkutano huo walisema nguvu kubwa wamezielekeza kupata tiba na chanjo ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaid), Profesa Anthony Fauci, aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akisema dunia imeingia mapinduzi makubwa ya kuelekea kwenye teknolojia ya kuzuia na kutibu Ukimwi.
Alisema mafanikio hayo yalianzia miaka michache iliyopita wakati walipogundua dawa za Kurefusha Maisha kwa Wagonjwa wa Ukimwi (ARV), lakini sasa wanapiga hatua mbele zaidi kulikabili gonjwa hilo ambalo katika nchi nyingi zinazoendelea limegeuka janga la uchumi kwa sababu wataalamu wanapoteza maisha.

Profesa Fauci anasema: “Dawa hii iliyogunduliwa na wanasayansi nchini Cambodia inaokoa maisha ya mwathirika mwenye hali mbaya.Hii inatokana na dawa hiyo kuweza kutumika wiki mbili baada ya mgonjwa kuanza kutumia dawa za kifua kikuu badala ya kusubiri mpaka zipite wiki nane.”

CHANZO:Gazeti la Mwananchi

Dawa kubwa ya kujıkınga na ukımwı nı kuacha mambo ya zınaa
 
Itakuwa ni jambo la kheri kupatikana japo chanjo ya gunjwa hili jamani. Ee Mungu tusaidie!
Gonjwa hili linachangia pakubwa kurudisha nyuma maendeleo hasa ya bara letu pendwa la Afrika na ulimwengu kwa ujumla.
Mungu awatangulie wote wanaojishughulisha na kutafuta kinga ya gonjwa hili na awape moyo wa kutokata tamaa kama apendavyo yeye. AMEN.
 
Hapo kwenye blue ndio pakufata
<br />
<br />
na yule aliyenao atafanyaje? ndo maana cku hizi hata kanisani wamebadili staili yao ya kuhubiri kuhusu huu ugonjwa.kuna wengine wameupata bahati mbaya,kutoka kwa wenzi wasio waaminif,kutoka kwa mama nk. Tujaribuni kuwafanya hawa wenzetu wacjickie guilty na kuanza kuusambaza makusudi ili tufe wengi. Ni wazo langu tu wakuu!
 
Back
Top Bottom