Wanaposema ni CCM Mpya, kwani ilichakaa lini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,176
Reaction score
48,460
Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole na kundi lake, wako bize kuzunguka nchi nzima kusema kwamba CCM mpya inakuja. Na pahala kwingine wamesikika wakisema kwamba sasa CCM imekuwa mpya.

Lakini kwenye Kampeni za Mwaka 2015 CCM walikuwa wanasema kuwa "CCM ni ile ile". Sasa CCM "ile ile" ni ipi? Ni ya kuanzia kwa Mwalimu Nyerere ama ni ya kuanzia kwa nani mpaka kwa nani? Na hawa wa "CCM Mpya" CCM wanayoiona kwamba ilikuwa "imechakaa" mpaka watake mpya ni ipi?

Na wakati CCM ilipokuwa "imechakaa" CCM yenyewe ilijijua kama imechakaa? Na kuchakaa huko siyo kule alikokusema Mzee Kingunge Ngombare Mwiru kwamba "CCM imekata pumzi"?

Madhara ya nchi kuendeshwa na CCM iliyochakaa ni yepi na taathira zake zimeondoka ama bado zipo? Jee ndani ya hiyo "CCM Mpya" ya kina Polepole ule uchakavu wa CCM iliyochakaa haujaingia?

Mawazo chakavu ya CCM chakavu ndiyo yamezaa viongozi chakavu waliyoichakaza nchi yetu mpaka kuwa hivi ilivyo. Ni kweli kuwa hata hii ya sasa ni CCM mpya ama ni ile ile chakavu ila inatoa kauli ikiwa kwenye nyumba mpya?
 
377b168668975a246e0d39a8e6b90c53.jpg
 
Ilichakazwa na Sumaye na Lowasa
 
CCM inayotegemea polisi na mtutu wa bunduki.
Ilichakaa ilipoishiwa hoja na maarifa ya kuendeleza nchi.
 
Kuna kikundi tu cha Anko Bashite na Polepole ndo wanaamini sasa ccm ni mali yao wataibadirisha ipendwe na wananchi wakisahau kuwa matendo yao yananuka
 
Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole na kundi lake, wako bize kuzunguka nchi nzima kusema kwamba CCM mpya inakuja. Na pahala kwingine wamesikika wakisema kwamba sasa CCM imekuwa mpya.

Lakini kwenye Kampeni za Mwaka 2015 CCM walikuwa wanasema kuwa "CCM ni ile ile". Sasa CCM "ile ile" ni ipi? Ni ya kuanzia kwa Mwalimu Nyerere ama ni ya kuanzia kwa nani mpaka kwa nani? Na hawa wa "CCM Mpya" CCM wanayoiona kwamba ilikuwa "imechakaa" mpaka watake mpya ni ipi?

Na wakati CCM ilipokuwa "imechakaa" CCM yenyewe ilijijua kama imechakaa? Na kuchakaa huko siyo kule alikokusema Mzee Kingunge Ngombare Mwiru kwamba "CCM imekata pumzi"?

Madhara ya nchi kuendeshwa na CCM iliyochakaa ni yepi na taathira zake zimeondoka ama bado zipo? Jee ndani ya hiyo "CCM Mpya" ya kina Polepole ule uchakavu wa CCM iliyochakaa haujaingia?

Mawazo chakavu ya CCM chakavu ndiyo yamezaa viongozi chakavu waliyoichakaza nchi yetu mpaka kuwa hivi ilivyo. Ni kweli kuwa hata hii ya sasa ni CCM mpya ama ni ile ile chakavu ila inatoa kauli ikiwa kwenye nyumba mpya?
New wine into an old bottle
 
CCM mpya maana yake umekuja kwa kazi ya Mauaji ya RAIA wake,ndivyo ninavuoelewa kwa sasa labda wanipe sababu ya kufikiria vinginevyo.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM Mwenyekiti wa Taifa ndiyo mwenye chama chake. Tofautisha kati ya CCM na wanaCCM.
Wewe unawashwa nini ccm ikiwa mpya au ya zamani !?.....chama chenu cha babamkwe, mwenyekiti ni wa maisha
 
Back
Top Bottom