Ili kutatua tatizo la ukosefu wa ajira ni muhimu sana tuwe na viwanda vya nguo. Kiwanda chochote cha nguo lazima kiwe na wafanyakazi wengi.
Have we lost all sense of self worth? Haiingi kabisa akilini kwetu kwamba tunaweza kuwa na viwanda vitakavyotengeneza nguo nzuri? Na hatuongelei mitindo (design) za ndani bali nguo za kutengeneza vitambaa hapa kwetu na kushona mashati, suruali na nguo za wanawake nchini kwetu.
Ningependa sana nivae nguo za vitambaa vilivyotengenezwa Tanzania na kushonwa na mafundi nguo wa Tanzania. Nashindwa tu kuzipata.
Tubadilike. Tujue kwamba ni sahihi waziri apange mikakati ya kuwepo viwanda vya nguo na kulinda soko lake.