Wanaotoa mimba washtakiwe kwa kosa la kuua!

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Najiuliza mtoto mchanga aliye tumboni ametukosea nini hata uhai wake usitishwe? Kwanini asizaliwe aje afe kadiri ya mipango ya Mungu?

Leo hii idadi ya mimba zinazotolewa ni nyingi na ninashangaa kuona serikali na jamii ya Kitaifa na Kimataifa kufumbia macho suala hili.

Hawa ni viumbe wasio na hatia na wasioweza kujitetetea. Mimi na wewe tungeuawa kama hawa watoto tungekuwa hatupo leo.

Naomba tutambue kuwa kutoa mimba (abortion) ni kosa kubwa sana kimaadili mbele ya macho ya Mungu Mwenyezi.

Mimba inatungwa mara tu baada ya mbegu za kiume kukutana na yai la kike hatua iitwayo 'conception'.

Natoa rai kwa akina mama na wadada, madaktari na wauguzi na jamii kwa ujumla kutoshiriki kutoa mimba kwa namna yoyote. Uhai wa mtoto ni wa thamani ktk hatua yoyote ya ukuaji.

Abortion ambayo inakubalika kimaadili ni ile ambayo inafanyika wakati kuna tishio la kifo cha mama au mama na mtoto ikiwa mimba itaendelea. Hii inaitwa therapeutic abortion.

Nawaomba tuungane pamoja KUTETEA UHAI WA WATOTO HAWA WASIO NA HATIA.
 
Ni kweli.
Tena mama na baba watarajiwa (wa mimba iliyotolewa) wafungwe....

Maana aliyetia na aliyebeba mimba wote wakosaji......
 
utashangaa kuna taasisi zinajiita za kutetea haki za binadamu wanatetea huo upuuzi kisa baadhi ya nchi za ulaya zinaruhusu au wanapokea msaada wa ngo
 
Ni kweli.
Tena mama na baba watarajiwa (wa mimba iliyotolewa) wafungwe....

Maana aliyetia na aliyebeba mimba wote wakosaji......
mama ni mshtakiwa namba moja. baba anaweza asijue au asishiriki ila akishiriki nae ashtakiwe!
 
mama ni mshtakiwa namba moja. baba anaweza asijue au asishiriki ila akishiriki nae ashtakiwe!
Wakishashtakiwa ndio itajulikana alishiriki au aliikataa mimba au vipi... ( tena wanaokataa mimba na kupelekea mwanamke kutoa mimba hao wanyongwe kabisa)
 
Wakishashtakiwa ndio itajulikana alishiriki au aliikataa mimba au vipi... ( tena wanaokataa mimba na kupelekea mwanamke kutoa mimba hao wanyongwe kabisa)
naunga mkono hoja ya kuwashtaki wanaoikataa mimba kwakuwa ni kichocheo cha mimba kutolewa. lakini umenishangaza kwa kutetea uhai mmoja huku unaupoteza mwingine. adhabu za kunyonga hadi kufa hazifai ndugu.
 
utashangaa kuna taasisi zinajiita za kutetea haki za binadamu wanatetea huo upuuzi kisa baadhi ya nchi za ulaya zinaruhusu au wanapokea msaada wa ngo
kweli mkuu umenikumbusha. mfano hawa LHRC kile kituo cha.akina mama Hellen Bijo Kisimba cjawahi kuwasikia wakitetea kwa nguvu watoto wanaouawa kwa kutolewa mimba.
 
..kuna mwanamume alikua na girlfriend wake,,bahati mbaya kuna siku alibakwa na akapata mimba,,,hvi ww kama mwanaume ungemshaurije girlfriend wako,aitoe au abaki nayo,,baba mwnye mtoto anaendelea kudunda mtaani maana kesi imefika mahakamani,mshua wake na girlfriend wako kasema yeye anataka hela kesi iishe ,akapew.unaeza kulea mtoto wa mwanamme mwenzako,...sio kila mimba ilikua ni voluntary conception wengine ni bahati mbaya,I sincerely believe one should have a choice on the matter on her own body
 
mkuu ktk hali yoyote uhai haupaswi kutolewa! hakuna mwenye mamlaka juu ya uhai wake au wa mwenzie zaidi ya Mungu. tumepewa uhai na miili yetu kama mawakili(stewards) na hivyo tunapaswa kulinda na kutunza na siyo kuharibu. tafadhali sana mkuu, hebu mfikirie na mtoto: yeye kakukosea nini hata umuue? kulea mtoto asiye wako ktk mazingira kama haya ni kujitoa sadaka na kuna thawabu toka kwa Mungu Mwenyezi. uhai ulindwe kwa gharama yoyote inayowezekana kwa mapenzi ya Mungu.
 
Back
Top Bottom