Wanaotembea nusu uchi wana lao jambo……….!

Kuna wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.

Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao.

Wanaume wanaovaa saggin' pants/mlegezo ama kata K huku mfereji na makalio yakiwa njeeee nao ni vipi?
Wanaume wanaovaa pants/jeans zimebana tii hadi vyombo vyote vinaonekana waziiii nayo imekaaje?
Tusiwashambulie wanawake tu, inabidi tutoe boriti kwenye macho yetu ndio tutaona vibanzi kwa wanawake
Just a thought
 
kuna kila dalili za uanaharakati humu. Ngoja tuangalie maana hizi issue za ki social wengine ni maluweluwe tu!
 
mambo ya kukaa kwenye kioo saa moja kwa kisingizio cha kujipenda, mhhhhhhhh bado siamini sana. Nadhani kuna kutanuliana tu kwenye issue ya mavazi kwa wadada. Na kama sio hiyo kitu basi ni attraction to the other opposite sex!
 
Back
Top Bottom