Wanaotamani Kiongozi "perfect", wasubiri tuende mbinguni

Wanaotamani Kiongozi "perfect", wasubiri tuende mbinguni

Mtemi Mojo

Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
39
Reaction score
44
Uzuri wa JF, tunapata fursa ya kuandika unavyojiskia. Wapo waandishi wazuri kama akina Mayalla, na tupo the majority other. Ila wote tupo huru kupost.

Hii kitu "uhuru" umesemwa sana kuwa ni moja ya mambo yanayokosekana ktk utawala wa JPM. Jambo hili na mengine kadhaa limefanya nifikirie kwa upeo wangu wa kawaida, ni Rais gani katika dunia hii aliye perfect.

Je? Ndugu msomaji, ungetamani Rais wako awe kama JK? Yule aliyesemwa bungeni na mnyika kuwa ni dhaifu? Aliyelaumiwa kwa DOWANS na ESCROW? Hata hivyo siwalaumu wanaotamani kiongozi kama yeye, maana JKnaye ni binadamu, na hakuna aliye perfect, wanamtamani kwa yale mazuri yake.

Huenda unatamani kiongozi kama Nyerere, sivyo?, yule aliyeweka watu kizuizini (bila kupelekwa mahakamani for yrs), yule aliyehamisha watu kwa nguvu, yule ambaye hakutaka upingane naye (muulize mzee Mtei na soma historia ya Kambona). Siwalaumu pia wanaotamani mtawala wa aina hii, Nyerere naye alikua binadam, hakua perfect.

Labda twende nje, je, tuwe na kiongozi kama Macron? Huyu wa 'yellow vest demonstrations'!!!? Au Trump (no need to narrate his imperfections), au labda Putin (anayefunga wapinzani), au Kagame (kamuulize yule maza aliyempinga kwenye uchaguzi), au Kenyatta (unawajua Mungiki na madhambi yao? Au wachina wanavyochukua Mombasa Port?), nani mwingine.....?

Ninachojaribu kusema, hata tukimchagua Fatma Karume awe Rais, bado hawezi kuwa perfect. kama binadamu wengine JPM hawezi kuwa perfect, kuna mambo hata mm natamani sana yangekuwa tofauti, ila tukiweka mzani wa kupima, nauhakika kama tutapima kwa Hakika, JPM will go in history as one of the best presidents ever to rule this Motherland of mine.

Mliotarajia niwe na mtiririko ulio "perfect" I would apologize, but then I thought, its not my fault to be human. So hata ukitoa povu sitamind maana nawewe sio perfect.
 
Ni suala la kupima. Kuna imperfection zingine ni very deadly kwa nchi. Ujinga usitetewe
 
Na ndio maana tunataka katiba ya wananchi na sio ya watawala kama sasa, mpaka wajiona mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sure. Katiba inasaidia. Ila haiondoi maovu ya wanadam. Slobodan Milosevic, Hitler, nk, wote walichaguliwa mi Katiba. Clinton aliongoza marekani yenye Katiba "nzuri" lakini akala demu ofisini.
 
Sio risasi upone, anahakikisha Unakufa. Refer aliowatuhumu kupanga mapinduzi mwaka juzi.
Mambo wawili tofauti kabisa, anaye piga risasi mpinzani wake halali, kumla nyama aliyejarubu kumpindua ataona ni adhabu isiyo tosha!!. Acheni ku justify matukio haya Magufuli anaweza kuleta maendeleo pasipo kupiga watanzania wenzake risasi wala kuteka na kupoteza raia yeyote
 
Maelezo ya ujanja ujanja unataka kuhalalisha anayeteka, anayeua ,anayefunga watu kwenye viroba, anayefunga wapinzani wake na kuwapa watu kesi bandia aue polisi ashtakiwe mbowe, unatetea mtu asiyeajili, asieongeza mshahara ,unatetea mtu aliekula hela za wahanga wa tetemeko kagera na 1.5 trillion I.
 
Back
Top Bottom