Wanaotaka muungano uvunjike watoke bungeni – Response | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaotaka muungano uvunjike watoke bungeni – Response

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, Jul 21, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Muungano wa Tanzania kimsingi,ulivunjwa rasmi April 1964, na yule yule muasisi wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Na Laila Abdulla

  Naelewa utashangaa kusikia hivyo. Mara tu baada ya kuapishwa Mwalimu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na baadae kujulikana kama Tanzania kwa mujibu wa kitabu cha Rais Mstaafu Aboud Jumbe wa Zanzibar, "THE PARTNER-SHIP", ni kuifuta Tanganyika katika ramani ya dunia. Hii ilimshangaza Jumbe.

  Kwa kuifuta Tanganyika, Zanzibar, kimsingi, haikuwa na mshirika tena katika Muungano. Kwani, katika ndoa akifariki mmoja kati ya mume na mke, ndoa huwa imekwisha na yeyote kati yao aweza kubaki pekee au kufunga ndoa mpya.

  Kilichosalia Bw.Lula ni kuutambua tu urithi aliotuachia Marehemu Mwalimu Julius Nyerere siku ile alipotawazwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kilichofuatia baada ya hapo ni mazingaombwe au niyaite "Abrakadabra." Kwani utaunganishaje nchi mbili ikiwa moja haipo?
  Sasa swali linakuja Zanzibar imeungana na nani tangu April 26,1964?. Haikuungana na Tanzania, kwani, kabla ya tarehe hiyo, haikuwapo nchi au dola iliyoitwa hivyo. Kwa hivyo bila ya Tanganyika, hakuna MUUNGANO. Na kwa kuwa hakuna kitu kinachoitwa Muungano, basi hakuna tena KERO za Muungano.

  Kilichobaki ni tatizo la Zanzibar na wazanzibari wenyewe. Kutojitangaza ilivyo na walivyokuwa, tangu sheria ya April 26 1964 ya kuizika Tanganyika, wao wamebaki vile vile walivyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Peoples Republic of Zanzibar , kisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na sasa Serikali ya umoja wa kitaifa.

  Lakini nani atathubutu kwenda Baraza la wawakilishi Chukwani au Redio Zanzibar, Rahaleo na kunadi kuwa, "Kuanzia leo bila ya kuwapo Tanganyika, Zanzibar ni nchi huru na si sehemu ya Tanzania?."

  Kiongozi wa Zanzibar shupavu wa kunadi hivyo angelikuwa mtu kama Marehemu muasisi wa pili wa Muungano huo – Mzee Abeid Amani Karume ambae aliwahi kunukuliwa akisema: ‘Muungano ni kama koti tu likikubana unalivua'.

  Wengine wenye ujasiri wa aina hiyo upande wa Tanganyika ni mtu kama Kasisi Christopher Mtikila na upande wa Zanzibar, Imam Farid aliyeuchana ule mswada wa mageuzi ya Katiba hadharani. Lakini wote hao wawili, ni Viongozi wa dini ambao wanajaribu kucheza dimba la siasa pia.
  Kwa hivyo Bw Lula nihitimishie kwa kusema, Zanzibar ni ya Wazanzibari na wanamuhitaji kiongozi shupavu na jasiri atakaeweza kumfunga PAKA kengele kuhusu ukweli huo wa Muungano wetu. Wananchi tayari wamekwisha amka.
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ni MZANZIBARI basi utakuwa unajua kwenu kuna baraza la wawakilishi. Basi litumieni ili mpate "haki" mnayoipigania. Mimi ni Mtanganyika, na sioni faida ninayoipata kuwa Mtanzania
   
 3. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  sio faida tu,hiyo bajeti ya tanzania/tanganyika basi haijakugusa wewe na familia yako,na watanganyika wote,sasa jiulize vipi wewe kama mwananchi utaona faida,faida kama wataka kuziona,ni barabara,rail,huduma za afya,mashangingi ya wabunge,mikopo na mikataba mibovu

  Jengine balozi zote zimeandikwa tanzania,mtu hata kama anakuja zanzibar lazima aombe visa kwa kupitia balozi ya tanzania,100dola kwa kila kichwa sio faida ya muungano hio ? Jengine misaada munaomba au mikopo kwa jina la tanzania,ikifika tanzania misaada hio huangukia tanganyika zanzibar kuangukia patupu,viongozi wa zanzibar wakitaka kuomba misaada lazima waombekibali kwa bwana tanzania huoni hio ni kero kubwa ya muungano na hasara kwetu,wewe huwezi kujua faida ya muungano wala hasara kwa sababu hujui hata kile unacho kisubiri au unachodai kwa kupitia mfuko wa tanznaia au tanganyika,jiulize bajeti imekugusa wewe ?
   
 4. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Rudini kwenu, go home!!
  Tumewachoka, gubu kama la mke mwenye wivu!!
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Unachosahau ni kuwa hata nje ya muungano visa na misaada itapatikana. Nje ya muungano Zanzibar italipa umeme kwa gharama halisi sio at a subsidized rate kama leo, watalipa mishahara ya watumishi wake n.k. Ni lini Zanzibar ilishatoa mchango wake kuendesha muungano?Si mjitoe tu, nani anawazuia?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  viongozi wenu wanachukua hii pesa na kila ubalozi kuna mnzanzibari..kama hii pesa huifaidi wenzako wanaipata thts y wamenyamaza
   
 7. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  kama znz ingelinganishwa na mwanamke basi ni yule mwanamke mlalamishi ktk ndoa yaan kila siku na lalamiko lake.Wazanzibar bahati serikali yenu ipo.Kwa nn msitumia baraza la wawakilishi kujitoa kwenye muungano ambao kila siku mnaulalamikia wananchi.Msiwe kama mwanamke niliyetoa habari yako hapo juu.Jiulezeni kwa nin baraza la wawakilishi haliongeleei kuhusu kuvunja muungano? kuna mambo mengi mnayofaidika lakn hamuishi kulalamika
   
 8. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Kabla ya mapinduzi mwaka 1964 zanzibar ilikuwa ina uchumi mzuri tu ukitofautisha na nchi zote za africa mashariki,kama utaamini wewe kuna barua waliwahi kuandika waengereza Uk kuomba mkopo zanzibar,na kwa wakati huo zanzibar ilikuwa na population ya watu kama laki 2 mpaka 2.5 ,jiulize kwa miaka hio tulikuwa na kitega uchumi gani cha kufanya uchumi kuwa juu,hata kufikia muengereza kuja kuomba mkopo zanzibar ?

  Zanzibar ki jografia ukiangalia imezungukwa na bahari,ina uwezo mkubwa wa kuwa vitega uchumi kuliko hata tanzania bara,musijidanganye na wingi wenu huo watu na ardhi,lakini mukashindwa hata kupewa panadol na serikali bure,lakini ukiangalia zanzibar ina iwezo wa kufanya free port,na tukavutiwa na wawekezaji wengi tu,kwa mfano nchi kama kenya,uganda,burungi,mafia,comorro,na sehemu nyengine za africa mashariki,wanaweza kutumia bandari ya zanzibar kwa kupitishia mizigo yao.

  Jengine wawekezaji kama wachina,japan,dubai,tailand,na wengine wanaweza kuja kuweka biashara zao zanzibar ili kuweza kuwauzia wateja wao katika mwambao wa africa mashariki,kama unavyoona dubai,sio lazima sisi zanzibar tuwe na viwanda,kutokana na population yetu,kwa haya yote basi tutajitosheleza kwa ajira.

  Jengine kama unakumbuka,zantel ilianzishwa zanzibar ,wakati walipotaka kuleta biashara yao bara waliiipigia vikali isije huko,lakini angalia sasa hivi eti mapato yake ambayo yanakusanywa yapo katika muungano zanzibar kuangukia patupu. Yote hayo ni choyo.

  Huyo baharesa unae muona wewe akiondoka leo bara nani atapata hasara ? Na nyinyi wengewe,unajua watu wangapi ambao wamejipatia ajira hapo ? Ukiacha watanganyika,hadi uganda wamepata ajira,kenya,rundwa,acha zako wewe,huyo bakhresa aje leo zanzibar nakuapia katashuka kibiashara zaidi ya kupanda kwa sababu zanzbari ni kituo cha biasahra na yeye ni mfanyaji wa biashara mzoefu,na naaamini wateja wake watakuja zanzibar,na kwanini wasije ? Sisi tunatoka zanzibar tunaenda malasia kununua mchele iweje wao hapo pua na mdogo karibu tu ?

  Mkuu naona huna hoja,zanzibar ikitoka leo ndani ya muungano basi tutapiga hatua haraka mno,na Sitta na Mizengo pinada wanaogopa mfumo wa serikali tatu kwa sababu wanajua zanzibar itapiga hatua haraka,kwa maana hiyo wazanzibari watafaidika na uchumi wao,na nyinyi watanga tanga la nyika,mutabakia mukilana wenyewe,kutokana viongozi wenu ni wezi,majambazi,hapo juzi tu jiulize bajeti yenu iliyopitishwa wewe imekugusa vipi ?

  Maisha yako unalipia,maji,umeme,maji machafu,matibabu,elimu,public services zote unalipia,jiulize unafaidika vipi wewe ndani ya mfumo huo ? Nyinyi watanga la nyika,muna marasilimali kibao,mbona hamufaidki ? Wanaofaidika ni viongozi wenu majambazi,kila siku ma skendo ya mikataba mibovu.

  AAAAAAAAAAMKAA KIJANA.

  WAKATI UMEFIKA,SISI WAZANZIBARI,TUNAPIGANIA HAKI YETU,WALA HATUWACHUKII NYINYI,SISI TUKIFANIKIWA TUWAWEZA HATA KUWASAIDIA NYINYI KWA NINI TUSIWASAIDIE ? pigania haki yako na wewe ndani ya serikali ya muungano,moja ni utaifa wako,ambo ni tanganyika,pili bajeti ikuguse na wewe,kwani rasilimali zile za ngoro ngoro ni za watanzania wote sio za wabunge wala kikwete,wala pinda wala 6ta,wala ccm yoyote na zenu wenyewe.

  ACHA KIBURI CHAKO WEEWE,MAISHA YAKO HUYAJUI NA HUJUI NINI UNAFANYA WALA UNACHOKIDA
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kilichoondoka ni Jina la tanganyika hata wanandoa wanapooana kuna uwezekano mkubwa wa mke kupoteza jina na ubini wake hasa ikiwa ndoa hiyo kuna mmoja kisilimu (batizwa) na Mapinduzi.. Matumizi ya jina hayana maana ya kuwepo kwa nchi mbili wala mke kutumia ubini wa mume haina maana amepoteza utu wake..
   
Loading...