Wanaotaka kujifunza lugha ya Kichina, UDSM

Jul 25, 2014
7
0
Habari zenu wana JF.

Nimeona watu wengi kwenye majukwaa mbalimbali wakitamani kujifunza lugha ya Kichina. Wenye nia hiyo wanakaribishwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Confucius Institute. Madarasa yetu ni ya jioni (miezi miwili), madarasa ya asubuhi kila siku kwa wiki 2, optional course kwa undergraduate, Intensive Chinese language kwa wale wanaotaka kwenda kusoma nchini China, Summer camp huko Zhejiang Normal University wiki 3 na chinese language for Children(inafundishwa Mlimani na Sunrise Primary school.

Program zingine ni scholarship za muda mfupi na,muda mrefu kwenda kusoma lugha huko China, Chinese language competition na Chinese language test (HSK,HSKK, BCT,YCT n.k)

Kwa sasa tunaendelea kupokea maombi ya watu 100 wanaotaka kwenda nchini China kwa mafunzo ya wiki 2 mwezi Septemba. Kwa taarifa zaidi pitia hapa www.udsm.ac.tz, unaweza kuni-PM au kutuma barua pepe kupitia ci@udsm.ac.tz

Asante sana.
 
Crush course ni tshs 100,000,000/=

Hiyo figure ya cost ya course imetisha sana.... Japo hujaja na point of correction ili watu wajue bei halisi ni ngapi... Above all mie co mwanafunzi ila ni mjasiriamali ninayependa sana kujua lugha ya kichina. Please nilikuwa nataka kujua mchanganuo kama ni evening class ni kuanzia sa ngapi na mwisho saa ngapi? Je course ipo kwa special intake? Au mda wowote mtu anaweza kujiunga? Kama ni kwa special intake, when will next intake start? Nashukuru mkuu.....
 
Back
Top Bottom