Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi

Hakuna ubishi

Kama Miungu hiyo haipo na wewe unakubali na huwezi kuthibitisha haipo for the same principle hata mimi nasema Mungu wako hayupo
Usijichanganje, tunachofanana ni kupinga na sio hoja ya kupinga.

Katika uislamu mungu ni mmoja, hivyo hiyo miungu mingine ni batili, au na wewe unatumia hoja hii? umeshakuwa muislamu?

Hivyo mimi kupinga uwepo wa miungu mingine sio hoja ya wewe kupinga mungu ninayemuamini bali ni ukaidi.

Hebu lete hoja.
 
Ili nisipinge Mungu wako nitakuomba unithibitishie uwepo wake, ukiweza nitamkubali
 
Ili nisipinge Mungu wako nitakuomba unithibitishie uwepo wake, ukiweza nitamkubali
Atakwambia thibitisha kama mungu yupo.

Sasa kama dalili alizoziweka mungu mwenyewe kuthibitisha uwepo wake hazijakukinaisha kuamini, unadhani hoja gani itakayokukinaisha.

Muktadha wa kupinga kwao ni kwamba mungu hayupo, hivyo hoja za kuthibitisha uwepo wake zote ni batili, lakini hata kama mungu yupo na hizi ndizo dalili alizoziweka kuthibitisha uwepo wake, basi ndio tayari wameshazipinga, maana hawakubalianinazo, hivyo ni wapingaji.
 
Ili nisipinge Mungu wako nitakuomba unithibitishie uwepo wake, ukiweza nitamkubali
Hili bandiko linaezea uwepo wa wakana mungu, hivyo jikibali maana hata Quran inathibitisha uwepo wako.

Au hadi hili nalo unapinga?
 
Wanaokana mungu huwa wanahoja mbalimbali katika kupinga uwepo wa mungu, pia huwa wanakosoa mafunzo ya dini ili kutilia mkazo zaidi katika hilo.

Lakini ukweli ni kwamba, sio kama hoja zao zinathibitisha kutokuwepo kwa mungu, hapana.
Bali hoja zao zinathibitisha kuwa wao ni wapingaji, hivyo hakuna andiko wala muujiza utakao wafanya waamini, sembuse hizi hoja ambazo huwa wanarumbana na watu Kila kukicha.

Na hivi ndivyo walivyo tangu enzi na enzi, hoja zao ni zilezile, na hata katika Quran, imeelezwa jinsi hawa watu walivyowakaidi.

Walipoonyeshwa miujiza waliita uchawi, maneno ya Mwenyezi Mungu waliyaita hadhithi za kutunga, mitume waliwaita wachawi, machizi n.k.(rejea; Quran 6:7,10:2,15:6, 46:17, 44:14, 40:56).

Na katika kudhihirisha zaidi ukaidi wao, walifikia hadi kusema kumwambia Mwenyezi Mungu, eti kama kweli hii (yaani yale aliyokujanayo mtume) ni haki kutoka kwako basi tuteremshie mawe kutoka mbinguni, au ututeremshie adhabu yenye kuumiza.(rejea; Quran 8:32).

Hii inaonyesha ni kiasi gani hawa watu ni wakaidi maana wangetaka kujua, wangeomba kuongozwa ila kwakuwa ni wakaidi wakaomba kuangamizwa.

Atakwambia thibitisha kama mungu yupo.

Sasa kama dalili alizoziweka mungu mwenyewe kuthibitisha uwepo wake hazijakukinaisha kuamini, unadhani hoja gani itakayokukinaisha.

Muktadha wa kupinga kwao ni kwamba mungu hayupo, hivyo hoja za kuthibitisha uwepo wake zote ni batili, lakini hata kama mungu yupo na hizi ndizo dalili alizoziweka kuthibitisha uwepo wake, basi ndio tayari wameshazipinga, maana hawakubalianinazo, hivyo ni wapingaji.

Kwahiyo tatizo sio ubora wa dawa ya sikio katika kutibu, bali tatizo ni kuwa hili ni sikio la kufa, hivyo halisikii dawa.
2022-03-23-00-08-22-539.jpg
 
Kuna vitu ukifikiria hupati majibu kabisa mfano kumu judge Mungu
Wakana mungu pia ni watu waliokosa direction, ndio maana hujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.

Hivi kama mtu ameupinga muongo uliotoka kwa mola wake, unadhani ni wapi atakapopata muongozo?

Hivyo ni lazima wajuilize maswali kama yasiyo na majibu.

Na walivyo wakaidi hutumia ujingawao(wa kutomjua mungu) kama hoja.
 
Mungu yupo

Alishusha Qur'an
Biblia iliandikwa kwa uoni wa Manabii kutoka kwake
Yupo kila pahala
Anamjua kila mtu

Swali langu ni
Ilikuwa nini asijithibitishe tangu awali kwa wazee wetu waliotangulia ili kujithibitisha kuwa apaswaye kuabudiwa ni yeye pekee badala yake huko kumfahamu yeye kukaja kupitia mawakala wa Ukoloni!?
 
Atakwambia thibitisha kama mungu yupo.

Sasa kama dalili alizoziweka mungu mwenyewe kuthibitisha uwepo wake hazijakukinaisha kuamini, unadhani hoja gani itakayokukinaisha.

Muktadha wa kupinga kwao ni kwamba mungu hayupo, hivyo hoja za kuthibitisha uwepo wake zote ni batili, lakini hata kama mungu yupo na hizi ndizo dalili alizoziweka kuthibitisha uwepo wake, basi ndio tayari wameshazipinga, maana hawakubalianinazo, hivyo ni wapingaji.
Kusema kuna dalili kaziweka, huo sio uthibitisho hiyo ni assumption yakuonesha unavyotaka ku fabricate uthibitisho
 
Hili bandiko linaezea uwepo wa wakana mungu, hivyo jikibali maana hata Quran inathibitisha uwepo wako.

Au hadi hili nalo unapinga?
Kuelezea na kuthibitisha ni mambo mawili tofauti

Naweza nikakuelezea hapa habari za Hogwarts kupitia kitabu cha Harrypotter lakini je hiyo itakuwa nimethibitisha shule hiyo ipo?
 
Kuelezea na kuthibitisha ni mambo mawili tofauti

Naweza nikakuelezea hapa habari za Hogwarts kupitia kitabu cha Harrypotter je hiyo itakuwa nimethibitisha shule hiyo ipo?
Basi sawa Quran inaeleza uwepo wa wakana mungu, hivyo inatambua uwepo wao.

Jikubali.

Na wewe ni uthibitisho ya kuwa wakana mungu wapo kama walivyotajwa katika Quran.
 
And when Our Verses (of the Quran) are recited to them, they say: "We have heard this (the Quran); if we wish we can say the like of this. This is nothing but the tales of the ancients."(8:31)

Hii nayo ni miongoni mwa hoja zao, lakini tangu Quran imeteremshwa mpaka leo hawajawahi kuleta mfano wake.
Mifano mingi Tu...sema vichwa ngumu hamkubaligi
 
Basi sawa Quran inaeleza uwepo wa wakana mungu, hivyo inatambua uwepo wao.

Jikubali.

Na wewe ni uthibitisho ya kuwa wakana mungu wapo kama walivyotajwa katika Quran.
Sio Quran tu, vitabu vingi vimeeleza uwepo wa wapinga Mungu lakini bado huvikubali kuwa ni vitabu vya kweli

Nini kinachofanya kitabu chako kiwe special kuliko vingine?

Kuthibitisha Mungu yupo ndio kwamba umeshindwa kabisa?
 
Hauwezi kumjua mungu bila DINI.
Ndo maana kulikuwa na mitume na manabii waliotumwa kuleta neno la kumjua mungu.
Ndo maana kuna watu waliowapinga hao mitume na manabii waliadhibiwa kwa adhabu Kali ya Mungu
Ndio ujinga unapoanzia
Kuamini simulizi/ngano za watu wachache waliotokea pale mashariki ya kati,

Tumelishwa vitu vya ovyo sana
 
Neno mungu umelitumia kwenye mkitadha gani?

Kumbuka kuna maneno kama haya

1.mungu
2. Mungu
3. MUNGU

TAFADHALI NIJULISHE MAANA UJUMBE WAKO NI MZURI SANA
 
Back
Top Bottom