Msonjo
JF-Expert Member
- Oct 13, 2019
- 1,378
- 2,394
Wanaokana mungu huwa wanahoja mbalimbali katika kupinga uwepo wa mungu, pia huwa wanakosoa mafunzo ya dini ili kutilia mkazo zaidi katika hilo.
Lakini ukweli ni kwamba, sio kama hoja zao zinathibitisha kutokuwepo kwa mungu, hapana.
Bali hoja zao zinathibitisha kuwa wao ni wapingaji, hivyo hakuna andiko wala muujiza utakao wafanya waamini, sembuse hizi hoja ambazo huwa wanarumbana na watu Kila kukicha.
Na hivi ndivyo walivyo tangu enzi na enzi, hoja zao ni zilezile, na hata katika Quran, imeelezwa jinsi hawa watu walivyowakaidi.
Walipoonyeshwa miujiza waliita uchawi, maneno ya Mwenyezi Mungu waliyaita hadhithi za kutunga, mitume waliwaita wachawi, machizi n.k.(rejea; Quran 6:7,10:2,15:6, 46:17, 44:14, 40:56).
Na katika kudhihirisha zaidi ukaidi wao, walifikia hadi kusema kumwambia Mwenyezi Mungu, eti kama kweli hii (yaani yale aliyokujanayo mtume) ni haki kutoka kwako basi tuteremshie mawe kutoka mbinguni, au ututeremshie adhabu yenye kuumiza.(rejea; Quran 8:32).
Hii inaonyesha ni kiasi gani hawa watu ni wakaidi maana wangetaka kujua, wangeomba kuongozwa ila kwakuwa ni wakaidi wakaomba kuangamizwa.
Atakwambia thibitisha kama mungu yupo.
Sasa kama dalili alizoziweka mungu mwenyewe kuthibitisha uwepo wake hazijakukinaisha kuamini, unadhani hoja gani itakayokukinaisha.
Muktadha wa kupinga kwao ni kwamba mungu hayupo, hivyo hoja za kuthibitisha uwepo wake zote ni batili, lakini hata kama mungu yupo na hizi ndizo dalili alizoziweka kuthibitisha uwepo wake, basi ndio tayari wameshazipinga, maana hawakubalianinazo, hivyo ni wapingaji.
Kwahiyo tatizo sio ubora wa dawa ya sikio katika kutibu, bali tatizo ni kuwa hili ni sikio la kufa, hivyo halisikii dawa.
Muendelezo
www.jamiiforums.com

Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi - 2
Wanaopinga uwepo wa Mungu, ukiwauliza kuhusu asili ya huu ulimwengu na jinsi ulivyo katika mpangilio ambao hauna dosari ndani yake, watakwambia ni nature au coincidence. Mimi mtu akinambia hivi swali la kwanza linalokuja akilini mwangu, ni je, hiyo nature inaakili(ufahamu)?. Kinacho mpambanua...
Wanaopinga uwepo wa mungu ni.....-3
Leo natoa na salamu. Kutokea pale nilipoishia. Kwa mwenyeakili atagundua kuwa huu ulimwengu na vyote vilivyomo, havikujiumba vyenyewe bali kuna alieviumba ndio maana vipo katika mpangilio uliopangika sawa sawa. Swali nani aliyeuumba na akauweka katika mpangilio huu? Aliyeumba ulimwengu na...