Wanaopiga wake/waume zao punguwani!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Hi, all! Kila nikichangia hii mada na wadau sehemu ninazopita huwa najikuta niko peke yangu.
1. Napata mshahara wangu na mke wangu anajua napata kiasi gani. Tunatumia wote kila mmoja kulingana na mahitaji yake.
2. Siwezi na wala sifikirii kumpiga mke wangu maana nampenda sana. Huu ni mwaka wangu wa 5 na sijawahi kumpiga.
3. Kukitokea issue huwa tunaeleweshana na hatugombani na wala hata mtu wa chumba kingine hawezi kujua unless aone tu moods zetu kwani mkielezana kitu na kama mumeelezana kwa kina mtu atakuonekana baridi kwa muda (sku mbili/tatu au wiki) kabla ya kurudia hali ya kawaida.
4. Sina nyumba ndogo na wala sitarajii kuwa nayo maana ni kukosa uaminifu katika ndoa na kunaweza kusababisha maambuzi ya magonjwa ya zinaa na hata kufikwa na mauti. Kukosa uaminifu katika ndoa ni sawa na unafiki maana ni lazima uwe mwongo. Ukichelewa huko kwa nyumba ndogo utasema "ulikuwa na safari ya kikazi". Uwongo wa namna hii ni mbaya sana maana nilimsikia mmoja akimdanganya mwenzake wa ndoa kwa simu kuwa "ndio wanakaribia Morogoro" wakati alikuwa Mbagala Rangi 3. Sikuamini!
5. Kuoa siyo kununua mke/mwenza hata kama umetoa mahari. Mke/mwenza wa ndoa siyo mali/kitu cha kuhifadhi kwenye mfuko na unaweza kukitumia unavyopenda. Wengine hata wanadiriki kumtia mke/mwenza wao kilema na hata kumwua kwa kisingizio cha "wivu wa mapenzi." Na mara nyingi wanaofanya haya siyo waaminifu wao wenyewe.
6. Nasema haya kwa sababu leo nimeshuhudia jamaa akimtwanga mke wake mangumi. Kisa? Mke wake alienda kumchukua baa waende nyumbani baada ya kuona muda umepita bila kufika na jamaa huyu anakunywa kila siku na sijui kama ana "any future"!
7. Kama mtu unampenda huwezi kumpiga, kumwumiza, kuwa na wasiwasi naye na wala kumwua! Kama wewe ni mmojawapo wa haya mataahira badilika kuanzia muda huu! Jifunze kuwa non-violent na inawezekana!
 
Wanaopiga wanawake hawawezi kazi na badala yake wanajihami kwa ngumi, I am not married but I will never set my fist on a woman, akizingua sana bora nimpeleke kwao tu, nimepewa mkanda wa KARATE na nimeambiwa never hit back until in defensing your self, how comes nimpige mwanamke?
 
Hongera kwa kupeleka utawala bora nyumbani ila uwe makini maana hizi nyumba zetu zina mambo.
 
Wanaopiga wanawake hawawezi kazi na badala yake wanajihami kwa ngumi, I am not married but I will never set my fist on a woman, akizingua sana bora nimpeleke kwao tu, nimepewa mkanda wa KARATE na nimeambiwa never hit back until in defensing your self, how comes nimpige mwanamke?

Huna nafasi nzuri ya kuzungumzia hili kwasababu haupo ndani ya ndoa. Tafadhali kua uyaone.
 
Kwanza hongera kwa kupata mke ambaye mnasikilizana. Kuna sababu flani flani ambazo zinasababisha watu kupigana kunakupiga kwa kumuonya baada ya kumuelewesha lakini akarudiarudia mara zote kosa hilohilo kiasi cha kukutia hasirana kuona kama anakudharau. Pia kuna unyanyasaji wa kijinsia mfano huyo jamaa aliyempiga mkewe kisa kamwambia waende nyumbani aache pombe. Sasa ndg sijui unazungumzia kupiga kupi? Maana sio kila jambo baya litakalokosewa na mkeo utamuacha kama mchangiaji hapo juu alivyochangia. mf Amechukua kadi yako bank katoa fedha alafu hana maelezo hazionekani na hasemi kafanyia nini, utamuacha? labda ukimfumania unaweza kumwacha. Pia wakati mwingine mtu kupigwa inategemea na yeye mwenyewe amejitune vipi, kuna wanawake pasua kichwa acha, ana vituko kiburi, umbea, anaongea kama jiriku na mwenye tabia za kutawala. Ndg zangu bila kuongopa ni wachache sana ambao ndoa zao zina miaka 5 na zaidi hawajawahi hata kupigana vikofi. Mshukuru sana muumba wako lakini ngoja siku ugundue huwa anakucheat walah waweza ua mtu na ulivyo mwaminifu hivyo? teheteheteheeee.
 
Yap, siko ndani ya ndoa lakini still naweza kujua namna ya kum handle mwanamke kuliko hata aliye kwenye ndoa, kuwa kwenye ndoa haimaanishi kwamba unajua sana jinsi ya kuishi na mwanamke, hujiulizi kwa nini wanandoa wanaenda kushauriwa kwa padri ambaye hajawahi oa?, Mapenzi ya kutiana ngumi yalishapitwa na wakati, It's not bravery a man to fight with a woman, kama wewe unajua sana kupiga nenda kapigane na wanaume wenzio, mkeo kama ni kichwa ngumu hata umpige vipi, haisaidii, sana sana utamtia kilema bure.
 
Wacha wawapige .. Sisi tusiopiga tutawachukuaaa
Umeona eeeh, hivi kwanza mwanamke unampiga wapi?, maa'ke kila nikimuangalia mwanamke sioni pa kupiga, unajua mkuu, mimi ni mtu wa mazoezi&a m very energetic, nikikutupia konde, hata kama mwanaume kama hujakaa stable lazima uende chini, sasa nikimtupia mwanamke si murder case hiyo?, nikishindwa kabisa basi, mwanamke hatakaa aone kofi langu.
 
Kwanza hongera kwa kupata mke ambaye mnasikilizana. Kuna sababu flani flani ambazo zinasababisha watu kupigana kunakupiga kwa kumuonya baada ya kumuelewesha lakini akarudiarudia mara zote kosa hilohilo kiasi cha kukutia hasirana kuona kama anakudharau. Pia kuna unyanyasaji wa kijinsia mfano huyo jamaa aliyempiga mkewe kisa kamwambia waende nyumbani aache pombe. Sasa ndg sijui unazungumzia kupiga kupi? Maana sio kila jambo baya litakalokosewa na mkeo utamuacha kama mchangiaji hapo juu alivyochangia. mf Amechukua kadi yako bank katoa fedha alafu hana maelezo hazionekani na hasemi kafanyia nini, utamuacha? labda ukimfumania unaweza kumwacha. Pia wakati mwingine mtu kupigwa inategemea na yeye mwenyewe amejitune vipi, kuna wanawake pasua kichwa acha, ana vituko kiburi, umbea, anaongea kama jiriku na mwenye tabia za kutawala. Ndg zangu bila kuongopa ni wachache sana ambao ndoa zao zina miaka 5 na zaidi hawajawahi hata kupigana vikofi. Mshukuru sana muumba wako lakini ngoja siku ugundue huwa anakucheat walah waweza ua mtu na ulivyo mwaminifu hivyo? teheteheteheeee.

Suppose unayosema yakifanywa na wewe, utapigwa pia au unampiga kwa sababu yeye hawezi kukupiga. Maana binafsi naona ni mazoea mabaya mtu kumpiga mtu mzima hata mtoto mdogo. Ni kwa nini ukikosea unaomba radhi na mkeo akikosea anapigwa. Hebu jiulize ni mara ngapi umefika nyumbani umechelewa na kutunga uwongo - oh nilikuwa kazini oh nanihii na nanihii. Lakini yeye achelewe kufika nyumbani atalala hapo. Ndugu zangu tubadilike. Tuwapende wake zetu na wanawake wawapende waume zao na wote tuwapende watoto wetu. Tunaweza kujifunza na inawezekana. Mimi siwezi kumpiga mke wangu na wala mtoto wangu maana naamini kama ninachomwambia hasikii hata nikimpiga hatasikia. Nilisoma shule ambayo sheria ilikuwa kutopiga wanafunzi na hii imenifundisha ku'control' my anger (anger management) na nimefaulu kwa asilimia 99.99
 
Kwanza hongera kwa kupata mke ambaye mnasikilizana. Kuna sababu flani flani ambazo zinasababisha watu kupigana kunakupiga kwa kumuonya baada ya kumuelewesha lakini akarudiarudia mara zote kosa hilohilo kiasi cha kukutia hasirana kuona kama anakudharau. Pia kuna unyanyasaji wa kijinsia mfano huyo jamaa aliyempiga mkewe kisa kamwambia waende nyumbani aache pombe. Sasa ndg sijui unazungumzia kupiga kupi? Maana sio kila jambo baya litakalokosewa na mkeo utamuacha kama mchangiaji hapo juu alivyochangia. mf Amechukua kadi yako bank katoa fedha alafu hana maelezo hazionekani na hasemi kafanyia nini, utamuacha? labda ukimfumania unaweza kumwacha. Pia wakati mwingine mtu kupigwa inategemea na yeye mwenyewe amejitune vipi, kuna wanawake pasua kichwa acha, ana vituko kiburi, umbea, anaongea kama jiriku na mwenye tabia za kutawala. Ndg zangu bila kuongopa ni wachache sana ambao ndoa zao zina miaka 5 na zaidi hawajawahi hata kupigana vikofi. Mshukuru sana muumba wako lakini ngoja siku ugundue huwa anakucheat walah waweza ua mtu na ulivyo mwaminifu hivyo? teheteheteheeee.

Unampiga ni ngoma hiyo??? Na ni nani kakupa mamlaka ya kumpiga mtu mzima, kisa ni mkeo? Hakuna sababu yoyote chini ya jua inayoweza kukufanya umpige mke wako. Unadhani kama ni mkorofi wakati hujamuoa atakuja kuacha wakati umemuoa???? Hii ndio maana mnaambiwa, acheni kukurupuka tu na kuoa mwanamke ni mwanamke au kuolewa na mwanaume ni mwanaume. Chunguzaneni kwanza ili mambo ya kukwazana yasiwepo. Sasa ukiangalia hapo kwenye red, utaoa mwanamke wa namna hiyo wa nini? Na hii ninamaanisha, unapochukua muda na kumjua mwenzako kabla hamjaoana itasaidia kuelewa weakness yake iko wapi na jinsi ya kui-handle maana kila mtu ana weakness zake. Au hata kumsaidia jinsi ya kuishinda hiyo weakness. Na pia kama ni maswala ya kutokuelewana, si mna wadhamini nyie? kinachokufanya umdunde ni nini? Na ukiona habadiliki mwache!!!
 
halafu ajiulize, akimpiga ndio ataacha ukorofi? nani anasema samaki anakunjwa akishakaangwa?
Mimi naona anapiga sio kwa ajili ya kumrekebisha bali kwa kujipunguzia hasira au frustration yeye mwenyewe; lakini kipigo hakijawa suluhu ya tabia ya mtu mzima sana yaweza jenga woga tu na kwa kiasi kikubwa shuki.
 
Back
Top Bottom