Wanaopewa mikopo vyuo vikuu wabanwa

Wanaopewa mikopo vyuo vikuu wabanwa

DOFFA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
425
Reaction score
233
stella-manyanya_210_120.jpg

Mh.Eng.Stella Manyanya-N/Waziri wa Elimu,utamaduni na Michezo.

SERIKALI iko katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuwapa kipaumbele inatimia.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabianchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Hatua hiyo inatokana na serikali kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi, hivyo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki kama ilivyo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano na serikali.

Manyanya alisema kuja na mtazamo na makubaliano hayo, yatakuwa kutumikia katika fani hiyo kwa kipindi fulani; na anapotoka aruhusiwe kwani sasa wapo wanapopangiwa huripoti na kuondoka bila kufanya kazi hizo.

Alisema suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.

Alitoa onyo kwa wanafunzi wanaosomea masomo hayo ya kipaumbele, kama hawana wito wa kufanya kazi hizo kuacha.

Alitoa mfano wa walimu wa sayansi ambao serikali inatoa fedha ili kusaidia wanafunzi katika shule za wananchi hususan vijijini, ambako hakuna walimu wa sayansi, hesabu na mengineyo.

Aliwaasa wanafunzi hao kuwa kama nia yao ni kupata mikopo tu, pesa hizo siyo nzuri kwao kwa sasa.

Akizungumzia ulipaji mikopo hiyo, Manyanya alisema wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.

Alisema serikali itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi wakimaliza masomo hawafikirii kulipa.

Alisema sasa lazima, wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa. Alisema kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mikopo huo kuwa wa kwanza kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi, zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hosteli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais John Magufuli alisema hadi sasa serikali inadai Sh trilioni 2.6 ambazo zilikopeshwa kwa wanufaika mbalimbali wa elimu ya juu, lakini hadi sasa hawajarejesha na hiyo inaleta changamoto kwa waombaji wapya.
 
Serikali iboreshe maslahi tu na iachane na ukandamizaji .

Watu wapitie JKT halafu baada ya hapo hamna mikopo au ndio ukipata upitie serikalini maslahi duni ila tunakata Mkopo wetu .

Waweke mazingira mazuri yatakayowavutia watu kufanya kazi serikalini sijui tume ya utumishi huwa inakua inafanyaje hapa ila kuna jitihada zinahitajika to attract the best brain.
 
Kweli aisee
 
Mmewabana wapi na ajira hamtaki kutoa

Walimu intake mbili wako wanazagaa,wataalam wa afya intake zaidi ya moja wapo private sector wengine nje ya nchi,mnaongea nini sijui nyie
 
Hivi si ndio huyu alisema juzi kuna watu wanapewa mikopo halafu wanaenda kununulia luninga!
Hawa wanawake buana!
 
Hawa viongozi kuna haja ya kuwapima akili zao.
Hivi mimi nmegraduate madicine MUHAS, nimesotea for almost six years lakin unasota kitaa no job.
Napata kazi private organization wanadai watakuja kunibana, hizi n zaidi ya zile siasa uchwara.
Nitafuten mimi kwanza nipo Hospitali kubwa ya private na hamna ujanja wa kunitoa huku, chezeen vilaza wenzenu.
 
Tusijivike upofu,
HIVI AJIRA ZENYEWE HUKO SIRIKALI ZIKO WAAAAPIIII???????????????????????????
 
kwanini Tusiratibu maandamano nchi nzima tunasubiria nini.9

swissme

Swissme maandamano watu watauawa kwa wingi. Amin aliua indiscriminately na hii hapa inakuja. You need another approach for sure
 
Pale unapoamua kujitekenya ili wanaokuzama waoene ukicheka, mbona tangu mmesitisha ajira kila mtu anakuja na yake ili asikike kuwa Anaweza kuongea ili tumsikie. Wakati mwingine muwe mnakaa kimyaaa seee.
 
stella-manyanya_210_120.jpg

Mh.Eng.Stella Manyanya-N/Waziri wa Elimu,utamaduni na Michezo.

SERIKALI iko katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuwapa kipaumbele inatimia.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabianchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Hatua hiyo inatokana na serikali kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi, hivyo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki kama ilivyo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano na serikali.

Manyanya alisema kuja na mtazamo na makubaliano hayo, yatakuwa kutumikia katika fani hiyo kwa kipindi fulani; na anapotoka aruhusiwe kwani sasa wapo wanapopangiwa huripoti na kuondoka bila kufanya kazi hizo.

Alisema suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.

Alitoa onyo kwa wanafunzi wanaosomea masomo hayo ya kipaumbele, kama hawana wito wa kufanya kazi hizo kuacha.

Alitoa mfano wa walimu wa sayansi ambao serikali inatoa fedha ili kusaidia wanafunzi katika shule za wananchi hususan vijijini, ambako hakuna walimu wa sayansi, hesabu na mengineyo.

Aliwaasa wanafunzi hao kuwa kama nia yao ni kupata mikopo tu, pesa hizo siyo nzuri kwao kwa sasa.

Akizungumzia ulipaji mikopo hiyo, Manyanya alisema wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.

Alisema serikali itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi wakimaliza masomo hawafikirii kulipa.

Alisema sasa lazima, wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa. Alisema kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mikopo huo kuwa wa kwanza kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi, zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hosteli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais John Magufuli alisema hadi sasa serikali inadai Sh trilioni 2.6 ambazo zilikopeshwa kwa wanufaika mbalimbali wa elimu ya juu, lakini hadi sasa hawajarejesha na hiyo inaleta changamoto kwa waombaji wapya.
wa.ji.nga nyie wahusika. leo mnasema kua walimu wa sayansi ni kipaumbele huku mmewaacha mtaani wakizurura bila kazi kwa roho zenu mbaya. mm nasema kweli, mtaniajiri ili nipate mtaji, sitadumu kwenye kazi yenu ya kulipana hela ya mboga. kwanza ajira zenyewe mpaka mtu atake kufa ndio mummpe, alafu leo mnamuita kipaumbele. malofa sana nyie
 
Huyu Mama Ni Taira Wa Kwanza Kabsa Anaongea Sababu Maneno Yanampelepweta, Hivi Ni Wahitimu Wangap Hamtaki Kuwaajiri Mpaka Sasa Wako Mtaani , Hawawezi Kuwasubir Nyie Vilaza Muwaijir Baada Ya Miaka 25 Ijayo. Wacheni Wapge Kazi Sekta Binafisi.
 
Back
Top Bottom