Wadau hbr zenu, kumekua hakuna haki sawa kwanza hapa tanzania, kwenye upataji wa travelling document i.e passport. swali la msingi, je passport siyo haki ya kila mtu kua nayo kama ID's zingine? Pili ni upande wa visa, wazungu huja hapa kwetu kwa mashart nafuu sana. Lakini ukijaribu ww kuomba visa ulaya au nchi zingine utaona joto lake.
Sasa mimi nasema hv! kila mtu anahaki ya kusafiri sehem yyte duniani regardless of watever. Pia nipo tayari kutoa msaada wowote iwapo umepata shida kupata passport au visa bila mafanikio. Nitatoa msaada huo free of charge, hii ni harakari ya kutokomeza hali ya unyanyapaa kwa waliyonayo maafisa uhamiaji na mabalozi wa nchi za ughaibuni kuwakwamisha wananchi wetu kusafiri.
Wazungu walikuja huku karne izo bure bila visa, wakachukua dhahabu na rasilimali watu wengi sana. Ni lazima wazirudishe kwa njia moja au nyingine.
Wenu katika harakati.
Visa pagumu sana ila ina uma yaani wazungu wana jaza fomu za visa ndani ya ndege nakumbuka ilikuwa nimepanda ndege kutoka Sweden ile tunakaribia Tanzania wakaanza kupewa fomu za visa wajaze kweli hakuna usawa...
nitakupataje mkuu?
Visa pagumu sana ila ina uma yaani wazungu wana jaza fomu za visa ndani ya ndege nakumbuka ilikuwa nimepanda ndege kutoka Sweden ile tunakaribia Tanzania wakaanza kupewa fomu za visa wajaze kweli hakuna usawa...
Kwenye passport nilipata shida zaidi ya miezi 2 kila nikienda narudishwa. Baadae nikampata mdau mmoja ambae anaofisi yake maeneo ya mjini, nikampa laki na 50 akanijazia upya, akamaliza kila kitu. Then akanipa elfu 50 ya kulipia uhamiaji na namba ya simu ya afisa wa pale, pamoja na bahasha ya kaki ambayo niliifungua mbele nikakuta kaweka elfu 40 kwa ajili ya huyo afisa. Kufika nikamcheki huyo afisa akaandika kitu juu ya fomu yangu, nikaenda nayo kwenye foleni nikapitisha ikapita nikafata process zote baada ya siku 10 nikapata passport yangu.
Ndugu huhitaji kutoa pesa yote hiyo kupata passport. Unahitaji tu kufata taratibu zote husika. Kama kua na docs zote, kama vile cheti cha kuzaliwa, Id yako, affidavit ya mzazi, barua utambulisho kutoka (serikali mtaa/kazini/shuleni-chuoni), barua ya sababu ya safari. Au kama mfanyabiashara attach tin na leseni yako hapo. Passport ni shs elf 50 tu. Ukiwa unamiss docs au mashart kutotimiza ndio hapo unakaribisha rushwa kuchkua nafasi.