Wanaopanda kutuhubiria na kutuombea katika Mabasi sisi na wao nani wana dhambi zaidi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
Nasikitikika ni kwanini huu Utamaduni wa Kijinga kama siyo wa Kipumbavu kabisa unaachwa na sasa umeshika kasi hapa nchini Tanzania kwani kiukweli unatuboa na kama Wahusika wasipoliangalia kwa umakini kuna dhahama inaweza kuja kutokea huko mbeleni.

Ni kweli Binadamu aliye kamili tunatakiwa kumjua Mwenyezi Mungu na hasa kupata mafundisho yake ili aweze kuishi kulingana na yale maandiko na hatimaye kuwa na Jamii njema na yenye Ustawi mzuri.

Lakini tabia hii ya Wahubiri tena hasa wa Kikristo ( ambapo nami pia ni Mkristo niliyetukuka kabisa ) ya kupanda katika kila basi la Mikoani na kuanza kutupigia Makelele kwa kutuhubiria huku wakizunguka basi zima kiukweli Kinakera mno.

Sasa cha ajabu zaidi siku hizi hawa Wahubiri hawapandi tu katika Mabasi ya Mikoani bali tunakumbana nao mno katika Madaladala tena Basi likiwa limejaa kabisa lakini bado tu huyo Mhubiri anang'ang'ana kupishana na Abiria ili azunguke basi zima kutuhubiria na kutuombea tuliomo mule.

Hivi nyie Wahubiri mnaotusumbua kwa mahubiri yenu ndani ya Mabasi ya Mikoani na katika Madaladala nani kawaambieni kuwa sisi hatuombi na hamtumjui Mwenyezi Mungu? Nani aliyewaambieni kuwa kila aliye ndani ya Basi la Mikoani na Daladala ni Mkristo? Hivi nyie Wahubiri kwani mkitafuta tu Uwanja wenu maalum muendeleze hayo Mahubiri yenu kwani hamuwezi kuwapata Watu hadi mje kutusumbua, kutupigia makelela na kutupandisha tu hasira ndani ya Mabasi ya Mikoani na Madaladala?

Mheshimiwa Kamanda Mpinga tafadhali sana lifanyie hili Kazi haraka sana kwani yawezekana Watu wengi wanakereka na hili ila wamekosa tu platform ya kuliongelea ila Mimi kwakuwa nina platform hii na nikiamini kuwa hata Wewe pia ni Member mzuri tu wa JF pamoja na Watendaji wako ni matumaini yangu makubwa kuwa utalitafutia ufumbuzi wa haraka kwani nisikufiche Kamanda LINATUKERA MNO ABIRIA na wengine mikono yetu huwa ni myepesi mno kutoa hukumu au kupiga Vichwa kama vya Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe pindi tupatapo Hasira au Kukereka.

Nimalizie tu kwa kusema nilichokigundua hapa ni kwamba yawezekana hawa Wahubiri wanaopanda kutwa katika Mabasi ya Mikoani na Madaladala kutuhubiria kisha kutuombea wakidhani sisi Abiria ndiyo wenye dhambi nyingi basi pengine wao Wahubiri ndiyo wanatakiwa kujihubiria na kujiombea sana wenyewe kwani wanasababisha dhambi kuwa ya KUTUKERA sisi ABIRIA kitu ambacho kinatupelekea KUCHUKIA hivyo kumkosea Mwenyezi Mungu.

Sipingi NENO la Mungu bali kilio changu hapa ni utaratibu tu mbovu na wa ki hovyo hovyo unatumika kulifikisha hilo neno la Mungu kwa Walengwa ambao kwa kiasi kikubwa sana huwa WANAKEREKA na KUBOREKA nalo.

Binafsi nimewachoka na naomba kuwasilisha.
 
Sawa mkuu, ila sidhani kama hao wahubiri huwa wanahubiri hadi kweny private cars, Mungu akusaidie upate usafiri wako ili uepukane na hiyo unayoiita kero

Hata vidole tu havilingani hivyo usishangae Mimi kubobea kunakotukuka katika kupanda Daladala na Mabasi ya Mikoani na Wewe ukizoea kupanda Private Car, Ndege na Cruise Ships.
 
Gentanycine....una kueaga n'a hoja kuntu,Hehehe..
Any wale Jamaa wengi wao ni wazushi tu
Kuna mmoja nlikuwa namuonaga sana kwenye bus ya abood akihubiri....Kuna Siku nkakutana naye kiwanja fulani anakata maji balaa...nkamfuata na kumuliza Vp mchungaji....akastuka mwishowe akaniambia Yote maisha tu

Ova
 
Hata vidole tu havilingani hivyo usishangae Mimi kubobea kunakotukuka katika kupanda Daladala na Mabasi ya Mikoani na Wewe ukizoea kupanda Private Car, Ndege na Cruise Ships.
Mi mwenyewe mchimba chumvi tu, private cars naziona kwa jirani tu ndio maana nikasema Mungu akusaidie
 
Wewe ni Mkristo uliyetukuka na hapo hapo hutaki kusikia Injili? Una taahira wewe sio bure.

Labda tukirudi kwenye hoja ya msingi: KERO, hapa kuna tatizo. Ni vyema watu kuyafuata mahubiri kwa hiyari yao na sio kujumuisha watu bila ridhaa yao.
 
Bora hata hao wanapiga kerere alafu hawapati chochote kuliko wale wa kwenye masunagogi wanatupigia kerere na kutuomba sadaka bila kusahau fungu la kumi..wakidai kwamba zinaenda Kwa Mungu...
 
Hao wahubiri wakiwa wanafanya kazi hiyo ya Mungu kwetu hawamaanishi kwamba sisi tunadhambi coz mwenye kujua unadhambi n Mungu tu.
Back to the point
""" mkuu waheshim Sana hao watu hata Mimi nilikuwa Kama wewe ulivyo sasa lakini siku moja niliamua kuwasikiliza wakati nikiwa kwenye basi natokea Kampala kuelekea Nairobi. Wakati jamaa amemaliza kuhubiri akaanza kuomba na kukemea Kama ndani ya gari kuna watu wenye dhamira ovu washindwe katika jina la Mungu, basi akamaliza tukatoa sadaka. Sasa tumefika Nairobi ( maana tuliingia usiku ilibidi tulale kwenye gari). Baada ya muda naona askari Kama kumi hivi wameingia kwenye gari wakiwa na silaha Kali, wakakamatwa abiria wawili waliokuwa na bunduki( wenyeji wanasema huwa wansubiri tukifika maeneo ya porini wanaliteka gari).


Amini kwamba kwa maombi ya yule muhubiri kuwakemea kwa jina la Mungu walishindwa kufanya uhalifu ule wakajikuta wamelala mpaka wanakuja kukamatwa.

HITIMISHO
usimdharau yeyote anayekuja kutoa mahubiri mpe sikio lako kumsikiliza kwa umakini na ukiguswa toa sadaka.
 
Back
Top Bottom