Wanaoolewa ndio Chanzo...

Wanaoolewa ndio Chanzo...

kisasangwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
292
Reaction score
56
Nimejaribu kuchunguza sana kwanini gharama za harusi siku hizi zinakua juu na kufanya watu wachoke hata kuchangia nikagundua yafuatayo

Wanawake waolewaji ndio chanzo

1. Wanataka mashindano…. Kaona harusi ya Fulani ilikua vile so nae anataka yake ifunike. Rafiki yake alikuwa na kitchen party, sendoff na harusi , nae anataka hivyo hivyo. Nguo ya harusi, pete na mapambo shogake alitumia mil 6 ye anataka amfunike kwa 8.

2. Wanataka kila mtu ajue. Most of wanawake wanatamani kuolewa, wengine wanataka tu ile kujulikana nae aliwahi kuolewa so wanataka bonge ya party ili iwe masimulizi hata kama ataachika.

Jamani nimeshuhudia mimi dada mmoja alikomaa na mzungu wa watu ili tu aolewe na kuwatambia wenzake. Akakomaa na michango na mikopo ili kufanikisha zoezi. After miezi 3 mzungu karudi kwao, yeye kabaki hapa mwaka sasa, akiulizwa anadai alishaolewa so ameondoa nuksi. Hapa ndo napojiuliza hivi kwani kina dada mkiacha tabia ya kupenda vya ghali hata kama hamviwezi mtapungukiwa nini.

Matokeo yake ni kwamba mnafunga ndoa ya kifahari afu after miezi mnatofautiana huku hamjalipa hata madeni mlokopa kujazia michango. Watu wanakaa hata mwaka bado wanadaiwa kisa harusi. HIVI KWANI FAHARI YA NDOA NI KUFANYA SHEREHE KUUUUBWA?

Waoaji wenye washaanza kustukia wanachakachua wanasepa.

Siku hizi hata engagement party zinachangiwa lol… mtu anataka jiparti kuubwa mbaya pale kijana anaposepa na kuacha mtu na kidole chake.

Jamani wanawake hebu badilikeni. Hizi tamaa na matamanio yasiyo mpaka yanasababisha hata kutoolewa mapema manake mtu akiona unampangia gharama kibao anakimbia. Sasa utakimbiwa na wangapi kisa tamaa za kufanya mambo makuuubwa hata pale usipoweza?
 
Mwe hii research yako umefannyia wapi?
 
kwa wanafanya mchakato wa kuolewa, walioolewa na waliokimbiwa na waliokua wawaoe....
 
nadhani sample size ilikua watu wawili.... LOL:whistle::whistle::whistle::whistle::whistle::whistle::whistle:
 
mi nashangaa..mbona kuna wanaume wanapooa wao ndio hutaka mambo ya juu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom