Wanaomwamini Lowassa wampe uongozi wa CHADEMA

Ngoja atakaposhindwa next week tuwaone hawa wapenda mabadiliko watataka aiongoze chadema kuelekea mabadiliko muhimu!
 
Ni lazima kuitumia silaha inayolingangana na kuzidi nguvu ya adui vinginevyo ni kushindwa
 
Wiki moja ijayo watakuwa na mzozo mkubwa sana wanachama na M/kiti wao na M/kiti na Lowassa wake ..mwanzo wa mwisho wa Lowassa
 
Bila kumjaribu na kumpima katika chama tunaweza vipi kumpa uongozi wa nchi tukaamini kuwa chama kitaweza kumdhibiti wakati tunajua jinsi gani alisumbua na kuvuruga chama chake ambacho ni tawala tena akiwa mbunge tu?

Aibu iliyoje eti chama kimeshindwa kumdhibiti mwanachama Hahaha....

Kufuli umelipima?
 
Ukapimwe nini waliopimwa wamefanya vituko hivyo vipimo havihitajiki mabadiliko muhimu sana
 
Afya sio ishu, JK aliangua jukwaani kama hana akili nzuri na amekaa miaka 10.

Nani kakwambia ikulu wanabeba zege?
Hujasoma na kuelewa comment yangu!

Nimesema achilia mbali udhoofu wake kiafya na kifikra, Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.
 
MOJAWAPO ya mambo ya kutisha zaidi kutoka katika historia ya kisiasa ya nchi yetu ni hii hamasa ambayo baadhi ya ndugu zetu wamekuwa nayo ya kumshabikia Lowassa wengine wakiapa kabisa kuwa wanataka awe Rais wetu................Bila kumjaribu na kumpima katika chama tunaweza vipi kumpa uongozi wa nchi tukaamini kuwa chama kitaweza kumdhibiti wakati tunajua jinsi gani alisumbua na kuvuruga chama chake ambacho ni tawala tena akiwa mbunge tu?

Chanzo:
RaiaMwema

Nadhani kuna kitu unataka kusema,
- Watu wasipige kura?
- If A is wrong then B is right?
Manake nadhani unaacha watu njia panda, Kampeni za kiukweli ni za kusema kwa nini fulani, na sio kwa nini SIO fulani, na kuacha watu hewani.

Hebu wape watu mbadala kwa ufasaha.

Ule mud wa kupiga kura kwa mazoea kuwa "" haya huyo huyo, kwa kuwa hatumuelewi mwingine"" "zimwi likujualo halikuli likakwisha" "mtakuwa kama sadamu husein wa Misri"
yamepoteza mvuto
Jipambanue na hizo siasa unazodhani sio za kiwango ulete za ukweli, bado kuna watu tunatafuta point ya kutufanya tumchague rais.
A B C D---
Posti za kuwanadi wagombea ziko chache sana, ila za kuwakandia ndio zimejaa.
Ila nashukuru sana Huyu mama Anna anaheshimika sana, ningemaind sana kama na yeye angekuwa anatukanwa humu.
Wanawake JUUUUU!!!
 
Wewe kama mtanzania una haki kusema usemavyo lakini kumbuka hii nchi si yako peke yako kila mtu ana hiari yake. Kama vile CCM na madudu yote bado ina wapenzi basi na CDM nayo ina wapenzi na watampigia kura Lowassa.
Maamuzi ya mwisho niya mpiga kura. Semeni yootee tukutane Oct 25.
 
MOJAWAPO ya mambo ya kutisha zaidi kutoka katika historia ya kisiasa ya nchi yetu ni hii hamasa ambayo baadhi ya ndugu zetu wamekuwa nayo ya kumshabikia Lowassa wengine wakiapa kabisa kuwa wanataka awe Rais wetu.

Tunaaminishwa kuwa sasa harakati za mabadiliko zimepata kiongozi anayeweza kuziongoza kweli kweli na kuwa kiongozi huyo siyo tu anaweza kuziongoza bali pia anapaswa kuziongoza. Na katika hili ndugu zetu hawa wanajaribu kuwaaminisha kuwa nafasi pekee ya mtu huyo kutuongoza ni urais na katika hili wanaonekana wametia pamba masikioni.

Ndugu zetu hawa wanatushangaa inakuwaje sisi wenzao ambao wengine tulijipambanua kuwa ni watu tunaotaka mabadiliko sahihi, makini na ya kweli leo hatujadandia hili treni na hatujatoroka twende huko aliko na sisi tuwepo. Wanatushangaa – hawashangai tunavyowashangaa wao kutushangaa – ati imekuwaje leo “nafasi” hii ya mabadiliko imetokea na sisi ambao tulidai sana mabadiliko hatuirukii na kuishangilia.

Jibu lake mojawapo ni kuwa hawataki kuamini kuwa sisi tunatambua au tumetambua ulaghai ulipojitokeza. Tumeelewa siasa katika kipeuo chake cha chini kabisa – ulaghai wa kisiasa. Tumetambua kuwa nafasi ya mabadiliko ya kweli imepoteza pale ambapo watu tuliowaamini kuongoza harakati hizi walipoamua kugeuka na kubinafsisha mabadiliko kiasi kwamba tunaogopa kama Lowassa akishinda chama kitakachoongoza kitakuwa ni Chadema au Lowassa.

Dalili zote zinaonesha (nazilionesha mapema tu) kuwa Lowassa siyo kiongozi wa kuweza kusimamiwa na chama cha siasa. CCM pamoja na nguvu zake zote na uwezo wake wote ilishindwa kumsimamia Lowassa na kumdhibiti kiasi kwamba ilibidi itumie kichinjio maalumu kummaliza kisiasa na kuwaachia wengine wahangaike naye.

Wenye kuamini kuwa Chadema chenye udhaifu wa uongozi sasa kitapata shida sana kuweza kumdhibiti mtu ambaye hata hivi sasa tu kampeni yake inaonekana kuwazidi nguvu kuisimamia. Kuna tetesi kuwa ni watu wa Lowassa hasa ndio wenye kuisimamia kampeni hiyo na hata wakongwe wa chama wakitaka baadhi ya mambo inabidi wawapitie watu hawa. Fikiria itokee ashinde uchaguzi; kuna wana Chadema watakuja mbele ya wananchi na machozi kutuambia “tulifanya makosa tulipoisaliti damu isiyo na hatia”. Wakati huo itakuwa wamechelewa.

Lakini kwa vile tunawapenda ndugu zetu wa Chadema na hasa wale ambao wameshiriki kwa kiasi kikubwa kuchochea mabadiliko ushauri wangu kwa Watanzania wapiga kura na wanaotaka kweli kuisaidia Chadema na wanaompenda sana Lowassa awaongoze basi wafanye jambo makini na la lazima na mimi nitawaunga mkono – wampe Lowassa uongozi wa Chadema kwa kumkatalia Ikulu ili akiongoze chama hicho.

Kwa vile watu wanaamini Lowassa kweli amekuwa ni mtu wa mageuzi na amekubali ajenda za mabadiliko njia pekee ya kumpima itakuwa ni kumpa uongozi wa chama cha siasa akijenge na kukiandaa kwa kufuata maono yake (tunaambiwa anajua matatizo yote ya Watanzania na ana utatuzi wake). Sasa ili tuweze kumuamini njia nzuri ni kumpa uongozi wa Chadema kwa kumkatalia Ikulu.

Na kwa vile Freeman Mbowe mwenyekiti wa sasa wa Chadema anamuamini sana kiasi kwamba aliamua kummilikisha Lowassa harakati za mabadiliko basi njia nzuri ya kuonesha imani hii ni kuwa baada ya Lowassa kushindwa tu itabidi ajiuzulu ili ampishe Lowassa Uenyekiti – sidhani kama Lowassa atakubali kuwa Katibu Mkuu; na Mbowe achukue nafasi ya Dk. Slaa kuwa Katibu Mkuu na pamoja waijenge tena Chadema (wakisaidiwa bila ya shaka na wake zao ambao leo ni wanaharakati).

Watanzania na wanachadema wenye kuwaamini viongozi hawa wanapaswa kumchagua mgombea mwingine (sijali sana kama atakuwa Magufuli) ili Lowassa aoneshe huo umahiri wa uongozi wake kwenye kukiongoza chama. Ni kweli anaweza kuwa kiongozi wa chama na Rais kwa wakati mmoja kama alivyo Kikwete lakini hapo atakuwa anatumia urais kuiongoza Chadema. Akinyimwa urais ndio wana Chadema watajua ni kwa kiasi gani Lowassa aliwapenda sana na kuungana nao.

Wazo la yeye kujiuzulu baada ya kushindwa Uchaguzi Mkuu wiki ijayo itabidi likataliwe na wana Chadema wote na ikibidi maandamano yafanyike nchi nzima kumuomba awaongoze Chadema kwa miaka mitano ijayo.

Ndugu zangu akiiongoza Chadema kwa miaka mitano ijayo na ikaimarika na kuponywa majeraha ya kujitakia ya mwaka huu nina uhakika akigombea mwaka 2020 hata mimi nitampa kura yangu na kumuunga mkono kwani atakuwa amethibitisha kweli yeye alifanya uamuzi wa kuingia Chadema kwa ajili ya kuongoza harakati za mabadiliko na nina uhakika ataonesha uongozi ambao utaiinua Chadema kwa miaka mitano ijayo kuliko uongozi wa watu wengine waliokuwepo kwa muda mrefu. Hata mimi nitamwombea kura 2020.

Bila kumjaribu na kumpima katika chama tunaweza vipi kumpa uongozi wa nchi tukaamini kuwa chama kitaweza kumdhibiti wakati tunajua jinsi gani alisumbua na kuvuruga chama chake ambacho ni tawala tena akiwa mbunge tu?

Chanzo:
RaiaMwema

Lowasa out!!!

Jizi
Gonjwa

Out!!!
 
Kuna limtandao alilitengeza alipokuwa huku ndo hao wengine unawaona wanatoka sasa kumfuata kiongozi wao na bado mengine yanakuja kumfuata. Vurugu yote iliyokuwa inasumbua huku inahamia kule. Baada ya hapo huku patabaki salama. Hili limtandao kama litatoka lote doo..!! cc uuhuuuu..... Itapumua
 
Watu wanashabikia shetan
Kweli pete ya Freemasons anayoivaa inazid kuwapumbaza watu

Lowasa out!!!!!!!!
 
Adui yetu mkubwa ni MKOLONI MWEUSI ccm. Hata wawekemo JIWE mimi nalipigia kura.
 
Back
Top Bottom